Wednesday, 8 March 2017

Re: [wanabidii] MWIGULU: MWENDENDO HUU WA POLISI, UNAKUHITAJI KUFANYA ZAIDI.

Elisa,
Hapo ndipo tunapopishana. Polisi hana mamlaka yoyote ya kuzuia maandamano ya raia, hata wanafunzi. Walichofanya wanafunzi wa Simiyu ni haki yao kabisa polisi hawakuwa na mamlaka ya kuingilia kati
na kuwazuia. Kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha kwamba maandamano yanafanyika kwa amani si kuyasimamisha na kuyazuia. Ni uvunjaji wa haki za  binadamu/raia.
em

2017-03-08 14:27 GMT-05:00 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Wakati rais akiwaapisha watendaji wake siku moja hivi karibuni, aligusia mwenendo wa raia kutoheshimu vyombo vya dola. Mifano aliyotoa ni watu kuitwa Polisi wakaongozana na kwaya na wengine kuosha magari. Nakubaliana na rais wetu kuwa vyombo hivi vinahitaji kuheshimiwa. Ukaribu wa watu Fulani na viongozi wetu wa juu kwa sababu mbalimbali ulitufikisha hapo. Mtu mwenye hela alijua hata akivunja sheria hawezi kukamatwa. Sasa Tanzania hakuna mwenye uhakika huo tena. Ni vibaya sana kwa raia mmoja kujihakikishia hilo kwamba hata akimuonea raia mwenzake hakuna taasisi ya kumshughulikia. Hii ndiyo huleta watu kuchukua sheria mkononi mwao.

Njia nyingine na muhimu ya lazima kwa vyombo hivi kuheshimiwa, ni vyombo vyenyewe kujiheshimu na kuheshimu nafasi zao.
Matukio mawili hivi karibuni yaliyotendwa na askari polisi wetu ni mfano mmojawapo wa jeshi hili kutojiheshimu na kwa kweli lisitegemee kuheshimiwa hata rais angeagiza.
Mkoani Pwani Polisi wamevamia kijiji cha wafugaji na kuanza kuswaga ng'ombe na kuwapeleka Polisi. Wafugaji bila kubisha wakakubali ng'ombe wapelekwe. Lakini wakataka ng'ombe hao wahesabiwe ili ijulikane ni ng'ombe wangapi wanachukuliwa. Polisi hawataki. Wanaamua kurusha risasi na kuua. Anakuja Mkuu wa Wilaya na kukana kuwa askari hao walikuwa hawakutumwa katika eneo husika maana sio eneo lenye mgogoro. Ni eneo la wafugaji. Wananchi wanadai hatua zichukuliwe kwa askari hao. Hakuna hatua zinazochukuliwa Mkoa mzima, mpaka waziri wa mambo ya ndani alipofika ndipo akaagiza askari hao wakamatwe.
Hebu tuone viashiria hivi; na kama ndio mfumo tuone kama raia wa Tanzania wako salama kweli:
1.      Askari anakwenda eneo lisilo na mgogoro na bila kuagizwa na wakubwa wake wa kazi, anakamata mali za raia.
2.      Raia wanakubali lakini wanataka kuhakiki mali inayokamatwa. Askari wanakataa. Wanaamua kuua raia hao.
3.      Mkuu wa Wilaya anadhibitisha Polisi hao wamefanya kitendo cha kihalifu; (kwa sababu hawakutumwa huko kukamata mali za raia hao).
4.      Mkoa mzima ambao una Mkuu wa wilaya, OCD, RPC na Mkuu wa Mkoa hakuna anayeona na kutumia madaraka yake kuwakamata askari hao. Maana yake wako huru na wanaweza kufanya hivyo hata kijiji kingine.
5.      Amri ya kuwakamata Polisi hao inakuja kutolewa na waziri.
Hivi katika mazingira haya raia wajione wako salama??? Tanzania ina mokoa karibu 30. Mikoa kumi ikipata tatizo linalohitaji askari akamatwe mpaka waziri aisungukie yote? Nataka Mwigulu ajijibu (asitangaze jibu). Sisi tunataka kupata jibu kwa jambo atakalolitenda.
Mwigulu kuagiza askari walioua wakamatwe, amemdhalilisha RPC. Kumsheshimu RPC wake alipashwa kumtimua kazi. Nitatoa mfano. Kuna tajiri mmoja alijenga kituo cha mafuta barabarani Mwanza. Waziri Magufuli (alikuwa hajawa rais), akamwagiza Mkuu wa mkoa kukibomoa kituo hicho. Mkuu wa mkoa akakataa. Magufuli (Inasemekana) alimpigia simu na kumwambia Mkuu wa Mkoa asikilize taarifa ya habari ya saa kumi atatajwa mkuu wa Mkoa mpya atakayefanya kazi hiyo. Simu ilipokatwa Mkuu wa Mkoa (inasemekana) alikwenda kusimamia kituo kuvunjwa na kwa masaa kilikuwa hakipo tena. Tunataka tuone kinachotokea ambacho inasemekana Mwigulu alifanya (kwa RPC) wake; kama Magufuli alivyofanya kwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati huo.

Kituko cha pili ni cha wanafunzi wa Simiyu. Wanafunzi wanasema shule yao ilikuwa inashindwa. Ameletwa mwalimu kwa juhudi zake sasa matokeo ya mitihani yanaonyesha mabadiliko. Mwalimu huyo anahamishwa. Wanafunzi wakaamua kuandamana. Wamebeba makaratasi. Polisi wakaja kuwazuia wasiandamane. Ni haki kabisa kuwazuia. Ilitarajiwa Polisi waweke ukanda na kuwatangazia wasimame hapohapo na kuwahoji wanataka nini. Sasa wanakuja na zana kana kwamba watu wanauana na namna ya kuwatawanya ni kuwavurunda.
Zimetoka picha mtandaoni zikionyesha Polisi "wanamdhibiti" mwanafunzi. Huyu anavuta huku, huyu anavuta huko, huyu anapiga ngwara. Mtu unajiuliza Polisi walikuwa wanafanya nini hasa? Nani alikuwa anawaongoza wenzake kufanya hivyo? Huyu mwanafunzi angeambiwa "panda gari hilo" angepanda. Angebisha Polisi wawili walitosha kumshika na kumlaza chini na kumuweka Pingu. Ukiiangalia picha hiyo hukosi kujiuliza kiwango cha elimu kinachotolewa kwa Polisi wetu huko chuoni! Kuna mtu aliwahi kusema huwa wanafundishwa ukakamavu na gwaride tu. Ukilinganisha picha hizo na usemi huo huwezi kumkatalia aliyesema wanajifunza gwaride na ukakamavu tu. Hakuna busara ya kuwashugulikia wahalifu inatolewa. Hakuna aina ya maandamano na namna ya kuyadhibiti. Hakuna elimu ya mahusiano na raia wema ili kazi yao iwe nyepesi. Kuna mtu anauza viroba jirani yangu. Mpaka sasa najiuliza nimwambie nani? Vituko hivi ndani ya makala yangu sithubutu kumwambia Polisi. Nakubaliana na mengine yanayosemwa juu yao. Mambo haya hayawezi kuacha kutonesha vidonda myoyoni mwetu juu ya matendo ya Polisi. Mauaji ya Mwangosi; Kuburuzwa ndani Lipumba wakati amewambia Polisi kuwa anakwenda kuwatawanya watu waliokuwa hawajui kuwa mkutano umekataliwa; na mengine mengi tu.
Ninakumbuka kusikia radio ujerumani wakielezea elimu ya Polisi wao. Wanasema Polisi akikutana na mtu amelala barabarani cha kwanza wanadhani ana kisukari, au kifafa au magonjwa mengine, kabla ya kufikiri ni mlevi. Polisi wana vifaa vya kupima kuhakikisha ana shida gani. Wa kwetu watapiga mateke na kusema ni mlevi. Mwigulu. Kati ya mambo ya kutopuuza ni elimu inayotolewa kwa asiakri wetu. Madaraka na wajibu wa Polisi wetu. Lakini niseme; Nitashangaa kama RPC wa Pwani ataendelea na kazi.
Elisa Muhingo
0767 187 507
elisamuhingo@yahoo.com

  
           --
       
          
       
     
           Send Emails to wana...@googlegroups.com
       
          
       
     
            
       
          
       
       
         Kujiondoa Tuma Email kwenda
       
          
       
       
         wanabidii+...@ googlegroups.com 
       
     
          Utapata Email ya
       
     
           kudhibitisha ukishatuma
       
          
       
     
            
       
          
       
       
         Disclaimer:
       
          
     
       
           Everyone
      posting to this Forum bears
        the sole
       
          responsibility
       
           for any legal
      consequences of his or
        her postings,
       
         and
       
     
          hence
       
           statements and facts must be
      presented
        responsibly.
       
     
         Your
       
           continued membership signifies that
        you agree to
       
         this
       
           disclaimer and pledge to abide by
      our
        Rules and
       
          Guidelines.
       
          
       
       
         ---
       
          
       
           You received this
      message because you
        are subscribed
       
         to
       
     
          the
       
           Google Groups "Wanabidii"
        group.
       
          
       
       
         To unsubscribe from this group and
       
      stop receiving
       
       
       emails
       
           from
      it, send an email to wanabidii+...@
       
      googlegroups.com.
       
       
        
       
           For more
      options, visit
       
          https://groups.google.com/d/
        optout.
       
          
       
       
     
       
       
       
     
        --
       
        Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
       
         
       
     
        Kujiondoa Tuma Email kwenda
       
        wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
       Utapata Email ya
       
      kudhibitisha ukishatuma
       
         
       
       
      Disclaimer:
       
        Everyone
      posting to this Forum bears the sole
     
      responsibility
        for any legal consequences
      of his or her postings, and
       hence
        statements and facts must be presented
      responsibly. Your
        continued membership
      signifies that you agree to this
       
      disclaimer and pledge to abide by our Rules and
        Guidelines.
       
        ---
       
       
      You received this message because you are
  subscribed
    to
       the
        Google Groups
      "Wanabidii" group.
       
        To unsubscribe from this group and stop
      receiving emails
        from it, send an email
      to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
       
        For more options,
      visit
     
      https://groups.google.com/d/optout.
       
     
        
     
   
    --
    Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
   
    Kujiondoa Tuma Email kwenda
    wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
    Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
   
    Disclaimer:
    Everyone posting to this Forum bears the sole
   responsibility
    for any legal consequences of his or her postings,
  and
   hence
    statements and facts must be presented responsibly.
  Your
    continued membership signifies that you agree to
  this
    disclaimer and pledge to abide by our Rules and
   Guidelines.
    ---
    You received this message because you are subscribed
  to
   the
    Google Groups "Wanabidii" group.
    To unsubscribe from this group and stop receiving
  emails
    from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
    For more options, visit
    https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment