Friday, 9 December 2016

[wanabidii]

Tunaelekea December 2016 kipindi ambacho wengi wetu huenda mapumzikoni. Wakati huo ni wakati wa kutumia kinywaji (hususan vileo) Kwa wingi na ulaji wa vyakula vyenye asili ya Nyama (hasa nyama choma)! Vile vile ni wakati wa kukaa sana na ndugu jamaa na marafiki tukibadilishana mawazo.
Ni vizuri sana tukumbuke kuwa miili yetu ili iwe na afya inahitaji mazoezi. Wengi tunajiuliza ni mazoezi ya aina gani na Kwa kiwango gani tufanye? Shirika la afya Duniani (WHO) Kwa kukusanya na kuunganisha tafiti mbali mbali Katika mataifa mengi limeleta mwongozo ufuatao;
1. Kwa ajili ya faida ya kiafya kila mtu mzima anatakiwa kufanya mazoezi ya aerobics ya kasi ya kati hadi kasi kubwa kwa angalau dakika 150 Kwa wiki
2. Kwa ajili ya Faida zaidi kiafya; mazoezi hayo yafanyike kwa dakika 300 Kwa wiki.
3. Ili mazoezi ya aerobics yahesabike lazima uwe umefanya Kwa angalau dakika 10 mfululizo bila kupumzika
4. Kila mtu mzima lazima afanye mazoezi ya kukinzana (Resistance Training - mazoezi ya vitu vizito) angalau Mara 2 Kwa wiki.
======================
Faida kubwa Za mazoezi ni;
1. Kuunguza Mafuta ya ziada mwilini na hivyo kudhibiti uzito
2. Kuimarisha afya ya mwili na akili Katika maeneo yafuatayo;
2.1 kuongeza uwepesi (flexibility)
2.2 Kuongeza uhimilivu (endurance)
2.3 Kuongeza kasi ya kutenda mambo (Agility)
2.4 Kuongeza uwezo wa kufanya mambo mengi Kwa wakati mmoja bila kukosea (coordination)
2.5 Kuongeza nguvu na ulinganifu wa mwili (balance)
3. Mazoezi ni kinga thabiti dhidi ya Magonjwa yanayosababishwa na mfumo wa maisha kama Shinikizo la damu, Magonjwa ya Moyo, Sukari na udhaifu wa kijinsia (kukosa hamu na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa)
4. Mazoezi vile vile ni kinga thabiti dhidi ya magonjwa ya akili kama Stress na depression (Sononi)
========================
😃😃 Karibuni NTA fitness pale Shell kwa Yusufu ushirikiane na wenzako kufanya mazoezi. Ukifanya peke yako ni vigumu kufanya kwa viwango sahihi. NTA fitness kuna trainers wazoefu; Okello, Augustine, Simba na Prince Kwa mazoezi ya aerobics na mazoezi ya Ukinzani (Resistance).
Tutumie kipindi cha mapumziko kuimarisha afya ya Mwili na akili Kwa kufanya mazoezi sahihi na kwa viwango sahihi. Mwili na akili vikiimarika na Roho zetu huimarika vile vile.
Karibuni wote NTA fitness; njooni tujenge afya!
======================

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment