Thursday, 8 December 2016

[wanabidii] NINI TOFAUTI KATI YA MALENGO YA SHULE NA VYUO BINAFSI NA ZILE ZA SERIKALI?

Kwa mtazamo wangu sioni fotauti ya kimalengo kati ya shule na vyuo vya binafsi na vile vya serikali. Kama ilivyo Hospitali za Umma na binafsi zote lengo ni kuhudumia Wananchi wa Tanzania ili waitumikie Tanzania. Kwa nini sasa unawekwa ubaguzi wa wazi namna hii? Kwa nini shule/vyuo /hospitali za binafsi zinaonekana ni biashara wakati ada zinazolipwa zinatumika kulipa wafanyakazi na kuhudumia watoto/wagongwa? Hizi taasisi zilianzishwa kuziba pengo au upungufu wa huduma za elimu na afya kwa vile serikali pekee haiwezi kubeba mzigo wote huo. Najiuliza kwa nini serikali itoze ada ya mitihani ya taifa kwa kila mtoto wa shule za binafsi? kwa nini serikali ibague wakopaji wanafunzi mikopo ya elimu ya juu ili hali wote ni watanzania na watalipa mikopo hiyo (busara hapa ni kutenga bajeti ya kukopesha wote wenye sifa na wanaohitaji mkopo huo) bila kubagua mkopaji kasomea shule gani. Kwa nini wamiliki wa shule/vyuo/hospital wabebeshwe kodi ya SDL na mapato wakazi ikibaki ziada wamiliki wanunue vifaa tiba na kufundishia ukizingatia wawekezaji hawa wazalendo wanaisaidia serikali kuondoa upungufu? shule/vyuo vinakopeswa na TEA (Mfuko wa Elimu Tanzania) ni kwa nini inawekwa Riba? ikiwa lengo ni kuwezesha kupunguza pengo lililopo la huduma hiyo muhimu?Hayo ni machache tuu kuna kero nyingi ambazo wahusika mnatakiwa kumsaidia Mh. Magufuli badala ya kumwachia abebe kila kero peke yake... Wahusika mumshauri mkuu wa nchi maana Rais wetu ni msikivu.

Na nyie watumishi wa TRA muwe wabunifu wa vyanzo vipya vya Kodi, kwani mnapoenda ziara za mafunzo nje ya nchi huwa mnajifunza nini? kweli ni lazima mtoze kodi katika elimu na afya kwa wawekezaji binafsi? Je ni hivyo hivyo mnatoza kutoka taasisi za selikali? kama siyo kwa nini iko hivyo?
Ninayo mengi ila sitaki kuwachosha....... Nawasilisha

0 comments:

Post a Comment