Thursday, 1 December 2016

[wanabidii] MKUTANO WA WAKAZI WA KIMBIJI NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI SIKU YA JUMAMOSI 3 /12/2016










MKUTANO WA WAKAZI WA KIMBIJI NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI

 SIKU YA JUMAMOSI 3 /12/2016 MKUTANO UTAFANYIKA SAA 4.00 ASUBUHI
Siku ya jumamosi tarehe3 Disemba 2016 saa 4.00 kutakuwa na mkutano maeneo ya KIJAKA ya zamani katika kata ya Kimbiji wilaya ya Kigamboni,
Mkutano huo ambao mkuu wa wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa
anatarajia kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa kata Kimbiji ambao
wana sumbuliwa mara kwa mara na  baadhi ya wanajeshi wenye nia ya kupora ardhi na viwanja vya raia kwa kutumia nguvu,malalamiko ya wananchi hao wa kata ya Kimbiji yamedumu kwa muda wa miaka sita sasa,
ambapo baadhi ya wanajeshi wanaoenda kufanya mazoezi katika eneo la Kijaka mara nyingi wamekuwa na tabia ya kuwanyanyasa wananchi na kuwaaribia makazi na kuwang'olea mazao katika mashamba yao,huku baadhi ya wanajeshia hao wakitamba kwa kusema wenyeji wa kimbiji lazima tutawaondoa!
Katika hali ya manyanyaso hayo wakazi wa Kimbiji imefikia wakati hata mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kijaka akawahi kupigwa na baadhi
ya wanajeshi hao,ripoti za manyanyaso hayo yameripotiwa katika ngazi zote
za kata hadi wilaya, vyombo
mbali mbali vya habari na wizara ya ardhi,ofisi za idara ya ulinzi ,pamoja na wakuu wa kikosi kinachojiusisha manyanyaso hayo lakini baadhi ya wanajeshi hao wanaendelea kusumbua raia kwa kuwafanyia fujo kwa lengo la kutaka kupora ardhi,ambapo katika makazi ya raia na mashamba yao wana michoro ya mipango miji.
Katika kulifuatilia na kupata ufumbuzi wa mgogoro huu wakazi wa Kimbiji na uongozi wao wamelifuatilia suhala lao hadi Wizara ya Ulinzi na kupata jibu kuwa hakuna maeneo ya jeshi katika mashamba au makazi ya raia Kimbiji,
Wizara ya Ardhi nako kumeonekana hakuna sehemu za wanajeshi katika maeneo ya raia Kimbiji ! kwa maana hii baadhi ya wanajeshi wanatumia kofia na nembo ya chombo cha taifa jeshi kutaka kuteka ardhi ya raia kwa maslahi binafsi !, Ni tegemeo la wakazi wa Kata ya Kimbiji kuwa mkutano wao na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw.Hashim Mgandilwa utamaliza kero zao na wananchi wapate kuendeleza maeneo yao.




--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment