Saturday, 13 June 2015

Re: [wanabidii] huyu ndiye pinda anayeutaka urais wa Tanzania

Mzava, big up. Wewe unawaza kama mimi. Eti mbona hawa watu wanajua watanzania na matatizo yao sasa kuliko wakati wowote? Mbona wakiwa wanakalia hivyo viti vikubwa sikuona hata moja aseme ukweli kwamba watanzania wana matatizo mojambili tatu na kutoa way foward kama wanavyojaribu japo kwa mbali au kwa juujuu kusema watatusaidia? Hivi hawa si wengi ni wale waliogopa kuwajibika kwa kuogopa kuadabishwa na kutuacha na matatizo lukuki? Hivi hawa si ndio ambao uki wapelekea tatizo la kiutendaji la watu wa chini yao hurudi kukusema kulekule na ukapata moto zaidi?Hivi hawa sio waliogonga meza kule bungeni na kupitisha hoja zingine zilizo tuumiza wakigonga meza huku wengine walikua wamelala wakati hoja inajadiliwa? Hawa si wale waliobebana bila kujali wanafanyia nini Tanzania?
Imefika muda sasa watanzania tupime na kuchuja viongozi wenye viwango wanatoa hoja na mipango inayetekelezeka kwa kifupi wanaojua ninini wanafanya. maana wengune wamekumbwa tu na mkumbo kwamba kwa kua wamekua wakibebwa basi wanaweza kuwania urais. Na ia watueleze waliifanyia nini tanzania walipopewa nafasi.
--------------------------------------------
On Fri, 6/12/15, 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] huyu ndiye pinda anayeutaka urais wa Tanzania
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, June 12, 2015, 8:31 AM


Mbona
wanazidi kuongezeka? NEC itakuwa na utata kuchagua. Kwa sasa
tunahitaji Rais zaidi ya Kagame dictator wa hali ya juu.
Pia, Waziri Mkuu awe mkali asiye mwoga. Kutokana na kuwa, TZ
ina kila kiyu nchini lakini hata extension staff  hawafanyi
kazi. Yupo kijijini hana mobilization yoyote, ana hair
saloon, duka la dawa, dula la mitumba, bodaboda au bajaji
anauza mchele hafanyi kazi ipasavyo. Mwingine anakaa
Tarafani sio Katani eti nyumba za umeme hakuna ambapo kwa
wazazi wake kijijini ukerewe au msolwa nyumba yao hovyo na
wala hana maji, choo bora wala umeme. Vijijini aliko unakuta
kuna nyumba nzuri za kupanga, kodi shs 5-10 kwa mwezi na
wengine wana solar wanaonyesha video au taa za betri. Hawa
wanataka PMO dictator aziambie wizara zifukuze wafanyakazi
wasioishi katika maeneo yao bali wanakaa miji midogo au ya
wilaya kwa visingizio mbali mbali.

Inawezekana kuboresha kilimo, nyumba, ufugaji
kama extension staff watatiziza wajibu wao. Ukifika wewe
mgeni kwa wiki moja ukawezesha kuhamasisha wanakijiji na
kujenga choo cha shule ukajitolea kuchoresha design na
kuilipia na kikajengeka hata darasa-utaona ile hela
uliyojitolea inaingizwa ktk bajeti ya kijiji au kata wanadai
warejeshewe; viongozi (M/Kiti kijiji, Diwani, Mbunge)
wanatumia kuonyesha hiyo kama ndio mradi wao
walioufanikisha-WIZI MTUPU na UZANDIKI. Tupo tupo tu
tumebweteka.

Aje PMO na
Rais wake wawezeshe kujengwa nyumba za police, FFU, JWTZ
askari wake wasikae mitaani bali ktk nyumba za kambi. Hii
itawezesha ufanisi wa kazi zao na kuwalinda. Askari hawezi
kupambana na majambazi, kukimbizana na kubotana na
wafanyabiashasha waliovamia eneo, au boda boda waliofanya
vurugu halafu akarudi kukaa ktk nyumba ya kupanga mtaani
manzese au eneo la uraiani. Anamkamataje mtoto kibaka,
jambazi ambaye baba yake ni land lord wake? Kisha-arudi
kulala hapo? Ni wazi atauawa. Nyumba zile za wakoloni za
railway, police za vibanda ambazo paa zake za bati au vigae
zimeshikiliwa na matofari juu ya paa, zinavuja, vyoo
vimelala upande havifai kutumika; sare zao za kuvaa
zinawabana na viatu vimelala upande-hakuna ufanisi hapa ni
kufanikisha rushwa kutokana na frustration za kazi na maisha
magumu. Mtumieni Mr Mchechu awajengee nyumba bora, kuwawekea
canteen ya kula na kunywa kwa apendae ili waache kunywa
pombe na raia na kuwa kundi moja bar na uniform
zao. Wawe na maduka yao ya bei rahisi na
marufuku yeye kununua jumla akauze gengeni. PMO an Rais
atakayerudisha JKT kuanzia baada ya kumaliza sekondari na
kuhakikisha wanalima yale matuta ya kilometa moja kwa mkono
na trekta ili tuwape vijana utambuzi na kupenda kilimo sio
kuona bodaboda tu na kuuza vyupi vya mitumba, vipochi ndio
ajira, kujenga ari ya utanzania kuipenda nchi sio kufurahia
ujambazi na maandamano. Viongozi wasionyeshe huruma kwa
kulia hadharani bali kuweza pia kuwabana watendaji na
kuhakikisha wahalifu kesi zao hazichukui miaka.

Mzazi/mlezi anabaka mwanae
kisha ndugu wanamuwekea dhamana na kumtoa au kukataa kufika
mahakamani kutoa ushahidi;  mzazi anashiriki albino ambae
ni mwanae/ndugu kukatwa viungo au kuuawa halafu kesi ichukue
karne inakuwaje? Mume anamwagia maji ya moto mkewe kisha
ukoo upo kesi inasuasua; bibi mlezi/mama, baba anamchoma
moto mtoto, anamfungia ndani ya box ndugu wanajua kuwa mtoto
wa mwenzao kafichwa ndani hawamuoni ije mpaka jirani ndio
wafichue siri-kamata hao ndugu wa karibu, mke na mume funda
ili masuala haya yaishe. Boresha vituo vya ustawi wa jamii
na malezi ya watoto yatima hao waliobaki wakalelewe. Idara
ya Social Welfare na vyuo vyake, vituo vyake
vifufuliwe-vimekufa hata taasisi za kulea wazee zipo kama
mabanda ya Mbwa-WHY na PMO mwenye huruma yupo au alikuwepo?
Vituo vya kulea wenye UKOMA ndio balaa-Why???? Tuna JKT,
JWZ, NHC kwa nini nyumba zisiwe bora, magodoro, vyoo na kuna
vyandarua vya bure? Kwa nini JKT, Magereza isilime mashamba
yao na ya
mamlaka nyingine wakalisha vituo
vya yatima, wazee na wenye ukoma? SIKIELEWI!! Halafu mtu
anajitokeza kuwa mgombea Urais! Kama asemavyo Mzava
hapa-atuonyeshe alichokifanya katika miaka 40 alipokuwa
madarakani!! Nami ninatangaza nia kumbe ninaweza kuchaguliwa
bila ya kuwa na nilichokifanya!! Watu wanauza nyumba
Kariakoo, Ilala na kuhamia Jangwani, Mchikichini maji ya
kinyesi mpaka juu ya paa-PMO, Mkuu wa Wilaya, Mbunge, Diwani
WAPO. Viwanja mijini mfano Dar, Moro etc vilipimwa tena kwa
mkopo wa wahisani. Mkaanzisha centre for housing studies,
Vyuo vya ardhi, Idara za upimaji na ramani (baadae Nyerere
centre for climate change, centre za taarifa za Ardhi)
lakini bado miji inavamiwa, maeneo yaliyopimwa watu
wanazidisha kuvuka mipaka ya viwanja, kufunga njia, maeneo
wazi yanajengwa, kuweha garages, parking za magari binafsi
au bajaji, kila nyumba ina bar na watu wazima kukojoa hovyo
watoto wanaona-miji imekuwa makorokoro kinyaa-PMO na waziri
wake
wanaangalia na Idara husika.

Wananchi wakipewa ardhi pa
usalama wanauza na kurudi ambako nyumba hazijabomolewa.
wanavamia misitu na mbuga za hifadhi-tunaangalia. Kiwanda
kinamwaga maji machafu Local GVt inaangalia. NEMC ipo, vyuo
vya maofisa wa mazingira na wizara ya mazingira na degree za
mazingira na wasomi wake-USIMBOMOLEE huyo mwache-order fro
above. Kama ni uwaziri Mkuu sasa Apewe Mh LUKUVI  ili tule
kisago cha uhakika kila kona tuweze kuvuka hapa pa USIASA
tulipokwama. Tunataka utendaji tuliouona. Hati za ardhi ziwe
na muhuru wa non-transferable without permission from Lands
Dept-ili kuzuia uuzaji holela wa ardhi wafanyao ndugu zetu
kisha kuhamia maeneo hatarishi na maisha kuendelea kuwa
mabaya na kutesa watoto wakati hela wamechezea (milioni mia
+ kisha unahamia mashimo ya machimbo ya mawe, mchanga,
matopeni kando ya mito, wetlands). Tunamheshimu Mh Pinda kwa
yote aliyofanya lakini Urais-tunahitaji dikteta zaidi ya
Kagame yeye mpole!! Watanzania tunahitaji kusukumwa sasa
kwa
bakora. Ila usiasa utaleta maandamano
na mapigano wakati issue inaonekana. Vyama vingi maana yake
sio kupinga hata mazuri nao upinzani waonyeshe pia
waliyofanya mazuri sio migomo na kashfa na lawama tu wakati
kwano hujafanya kitu ila unakula bata, mikufu  minene ya
dhahabu ya bei ya mamilioni, ulaya kufanya manunuzi kijijini
watu wanashinda wanalewa gongo na bangi mpaka ndoa
zinavunja!!??

--------------------------------------------
On Fri, 12/6/15, 'mohamed mnzava' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

Subject: Re:
[wanabidii] huyu ndiye pinda anayeutaka urais wa Tanzania
To: "wanabidii@googlegroups.com"
<wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, 12 June, 2015, 7:02

Hapa

tumepata taarifa za mtu ambaye yaonekana wazi kuwa
amebebwa
na Taifa hili kwa kipindi cha
zaidi ya miaka 40 ya maisha
yake . . .  .
.
Jambo la
msingi la
kujiuliza ni kuwa Je katika miaka zaidi ya 40 ya
kuwepo katika nafasi za juu za madaraka yeye
kwa
binafsi AMEFANYA MAMBO GANI YA MSINGI
NA FAIDA aidha katika
kutatua matatizo SUGU
yaliyopo kwa mtanzania wa kawaida? . .
.
.  haswa katikaKupunguza
UMASIKINI,
UJINGA, MARADHI NA UBADHIRIFU NA
RUSHWA?
Yeyote
ambaye anajipendekeza
kutaka apewe dhamana ya uongozi ni
lazima
tumuulize na atupatie majibu ya Tija zake katika
kutatua MATATIZO SUGU ya mtanzania wa
kawaida.
Bila
kutupatia majibu hayo ni dhahiri kuwa HANA
jipya, ni
yuleyule

Aidha
AHADI alizotoa katika Bunge na nje ya
bunge bado
hajazitekelezwa. Mifano:
  -
Kuzuia mauaji ya
maalbino   -
Kuondoa au kupunguza
matumizi ya magari ya kifahari kwa

watendaji wa serikali nk. 



   



 
   On Friday, June 12,
2015 1:09
AM, 'mpombe mtalika' via Wanabidii

<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

   

  Mizengo Pinda alizaliwa
Agosti 12, 1948 mkoani Rukwa (atafikisha miaka
67 Agosti
mwaka huu). Pinda ni Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania tangu
mwaka 2008.Wazazi wa Mizengo Pinda wote

walikuwa wakulima kwa hiyo kijana pia alifuata nyayo hizo
huku akifanya jitihada kubwa kwenye masomo
yake na
kufanikiwa kuhitimu shule ya msingi
na sekondari, akifaulu
vizuri kila
alikopita.

Baada ya
masomo yake ya sekondari, Pinda
alijiunga
na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusomea Shahada ya
Sheria (LLB) mwaka 1971 hadi 1974. Baada ya
kuhitimu,
alijiunga katika utumishi kwenye
Wizara ya Sheria akiwa
Mwanasheria wa
Serikali na alikaa katika utumishi huo tangu
mwaka 1974 hadi 1978.Mwaka 1978, alifanya kazi
akiwa
"Ofisa Usalama wa Taifa" akiwa
Ikulu hadi mwaka 1982,



Rais wakati huo, Mwalimu

Julius Nyerere alipomteua kuwa katibu wake binafsi
(Katibu
wa Rais) nafasi aliyoishikilia hadi
mwaka 1985.
Baada ya Mwalimu Nyerere
kung'atuka na
kuikabidhi nchi kwa Ali
Hassan Mwinyi, Pinda alitakiwa
kubaki
kuendelea kumsaidia Mzee Mwinyi na alikubali wito
huo. Akaendelea kuitumikia Ikulu chini ya
utawala wa Mwinyi
hadi mwaka 1992.

Mnamo
mwaka
1995, Pinda alijaribu kugombea ubunge katika Jimbo la
Mpanda Mashariki lakini alishindwa katika
hatua ya kura za
maoni na ikampasa kurejea
kwenye kazi yake ya awali
Ikulu.
Baada ya Mkapa kuteuliwa kurithi
Ikulu mwaka 1995, alimteua Pinda kuwa karani
wa Baraza la
Mawaziri. Wadhifa
alioushikilia kuanzia mwaka 1996 hadi
2000.
Pinda amemuoa Tunu na wamepata watoto wanne; Janet,
Jenifer, Hardwick na Narusi.


MBIO ZA UBUNGE
Mwaka
2000,
Pinda aliachana na utumishi ndani ya
Serikali na Ikulu
akajitupa jimboni Katavi
kusaka ubunge kwa mara nyingine,
safari hii
alipita ndani ya kura za maoni za CCM akafanikiwa
kuwashinda wapinzani na kuwa mbunge. Nyota ya
Pinda ilizidi
kung'ara mwaka 2001, pale
Rais Mkapa alipomteua kuwa Naibu
Waziri wa
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)
akifanya kazi chini ya waziri wake, Brigedia
Jenerali Hassan
Ngwilizi, hadi mwaka 2005.
Mwaka 2005, Pinda aliwashinda
Sebastian
Bedastus wa TLP na Albert Damian wa CUF na

kuchaguliwa kwa mara ya pili kuwa Mbunge wa Katavi na
aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa waziri kamili
wa Tamisemi.


Bahati ya Pinda kisiasa

iliruka angani wakati wa "ajali ya kisiasa" ya Edward
Lowassa iliyoacha nafasi ya uwaziri mkuu wazi
kutokana na
kashfa ya Richmond, Rais
Kikwete alimteua Pinda kuwa Waziri
Mkuu.
Jimboni Katavi mwaka 2010, Mizengo Pinda alishinda
uchaguzi kwa "kupita bila kupingwa" na
aliteuliwa tena
na Rais Kikwete kushika
wadhifa wa Waziri Mkuu hadi sasa.

MBIO ZA URAIS
Pinda ni
mwanasiasa aliyeamua kwa dhati
kuachana na
mambo ya ubunge na kujitosa miguu miwili kwenye
kinyang'anyiro cha urais. Wanasiasa wengi
hujaribu
kugombea urais huku wakiwa
wanautaka ubunge, hutupa ndoano
kwenye
urais lakini wanapiga hesabu za ubunge ikiwa watakosa
ridhaa ya uteuzi, hawa ni aina ya watu ambao
huamini kuwa
wanapaswa kusalia madarakani
kwa njia yoyote ile, Pinda si
mmoja wao.

Hivi

ninapoandika, Pinda amekwishawaaga wana Katavi tangu
mwaka
jana na amekuwa akijiweka hadharani
na kuendelea na mikakati
ya chini kwa chini
ya kuingia Ikulu.
Hata

hivyo, kutangaza nia kwake kumekuwa na maoni tofauti
kutoka
kwa wananchi hasa ikizingatiwa kuwa
wengi wanamfahamu vizuri
kwa uimara na
udhaifu wake na kila mmoja ana sababu yake.

Oktoba, 2014 akiwa nchini Uingereza alieleza
kuwa amejitokeza kugombea urais ili pamoja na
wenzake
walioanza harakati, Watanzania
wapate muda wa kuwapima.


Mwandishi wa BBC alipomhoji
kama na yeye ni
miongoni mwa watu wanaotaka kuvaa viatu vya

Kikwete alisema, "… umesikia kama nimo? … basi
tukubali hilo na yeye Waziri Mkuu yumo. Hao
wote
waliojitokeza pamoja na Waziri Mkuu
aliyejitokeza ni katika
jitihada za kusema
hebu Watanzania nitazameni je, mnaona
nafaa
au hapana?"

NGUVU
YAKE
Pinda ana nguvu ya
asili, ni kiongozi
mtulivu na msikivu.
Mawaziri wakuu wengi waliopita hapa
nchini
si watu wa 'chapchap', Pinda yuko tofauti,
ukimpigia simu muda wowote ambao yuko karibu
nayo atapokea
na atakusikiliza nini
unasema, atakushauri hatua zipi
zichukuliwe
au atakuomba muda afuatilie suala husika kwa
mawaziri wake. Mara nyingi husikiliza zaidi
kuliko kuongea,
hii ni sifa muhimu mno kwa
kiongozi yeyote yule anayehitaji
madaraka
makubwa.

Jambo la
pili linalompa nguvu ni kutojikweza. Pinda si
mtu wa makuu
wala mbwembwe, ni mtu
asiyejikweza na kila mara anaishi
maisha ya
kawaida tofauti na mawaziri wakuu wengi duniani na
hata baadhi ya waliopita hapa Tanzania. Yeye
mwenyewe
hujiita "mtoto wa mkulima" na
aina ya maisha anayoishi
yanafanana na
"ukulima".

Jambo la
tatu ni "usafi wa kisiasa".
Ukiondoa
kashfa ya Escrow ambayo almanusura imuondoe katika
wadhifa alionao hivi sasa, Pinda hakuwahi
kutuhumiwa
kuhusika na ubadhirifu wowote
ule serikalini. Hata Escrow
kwa kiasi
kikubwa tuhuma zilimwendea kwa sababu tu ya nafasi
yake ya Waziri Mkuu lakini si kwa sababu
alishiriki kukwapua
fedha hizo.
Pinda ana nguvu ya asili ndani
ya CCM, kwa sababu ni waziri mkuu anayemaliza
muda wake,
siyo jambo la ajabu kuwa ana
watu wengi wanaomuunga mkono
ndani ya chama
hicho.

--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email
kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:

Everyone posting to
this Forum bears the
sole responsibility for any legal

consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your
continued
membership signifies that you
agree to this disclaimer and
pledge to
abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message

because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.

To unsubscribe
from this group and stop
receiving emails from it, send an
email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit

https://groups.google.com/d/optout.

     


--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda


wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:


Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and hence

statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree
to this
disclaimer and pledge to abide by
our Rules and
Guidelines.


---


You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii"
group.

To unsubscribe
from this group and stop receiving emails

from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.


--
Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment