Monday, 4 May 2015

Re: [wanabidii] SERIKALI INABEMBELEZA PENZI KWA MADEREVA?

Nachelea kusema Happy kuwa mfano uliotumia umekupoteza na makala yako ikaenda tenge.
Bila kupitia mfano wowote habu wafiririe madereva hawa na madai yao.
Tuanzie la kurudi shule kila baada ya miaka mitatu na kulipa karo hiyo. Wewe ni mtaalamu wa habari. Mara ngapi kunatokea mabadiliko katika taaluma yako na unaweza ku-coop bila kulazimika kwenda shule? Mimi ni tabibu na toka nimetoka shule sijawahi kuitwa kwenda shule ili niweze kuwaandikia wagonjwa dawa. Kuna mabadiliko makubwa na madawa niliyoyasoma enzi hizo hayaonekani tena. Haya mapya nimeyajua tu ndani ya utendaji. Mimi ni dereva. Nilijifunzia manual kuen desha gari. Ninaweza kuendesha hizi semiautomatic (automatic hazijaja). Kwa nini madereva walazimike kwenda shule kila kurenew liseni?
Kwanza nini maana ya kurenuw liseni? Ni kwenda TRA kulipia na kupewa liseni mpya. Hiki ni kitendpo cha unyanyasaji
Ajali zina sababu nyingi na moja wapo ni speed kubwa kwa uzembe wa madereva. Sasa serikali imeweka kipimo cha speed 80 kwa saa. Kwa sababu hiyo watalazimika kulala njianai. Wanataka mikataba yao iwasaidie kupata pa kulala wanapokuwa njiani ili wasilazimike kulalia usukani ambayo inachosha zaidi na kuwezekana kusababisha ajali. Wenye magari wanaona hiyo inawagarimu Hawataki.
Mikataba yao ina shida. Mwenye gari anaweza kubadilisha madereva kila mwaka na huyu hana mpango wa kumpa mafao. Wanalalamika na hilo. Wanataka waajiri wao wawe na utaratibu utakaowanufanisha.
malalamiko yao hayo wameahidiwa kushughulikiwa na mchakato umeanza. Neno hilo lina miaka saba toka limetamkwa na hakuna kinachoendelea.
Walipojaribu mgomo Kova na waziri walikuja na lugha laini. Waliporudi kazini kila kitu kikaishia hapo.
sasa wameamua kugoma.
Hebu tuandikie makala nyigine ikiadress matatizo hayo na uwalaumu kama utaweza. Ikikushinda wahurumie. Zungumzia pembeni huenda serikali na waajiri wao wakakuelewa.

--------------------------------------------
On Mon, 5/4/15, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] SERIKALI INABEMBELEZA PENZI KWA MADEREVA?
To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, May 4, 2015, 1:39 PM

SERIKALI INABEMBELEZA PENZI KWA
MADEREVA?

Na Happiness Katabazi

KWA wale wote waliopo au wanatoka kuingia Kwenye mahusiano
ya kimapenzi basi watakubaliana mwanamke au mwanamme Katika
mahusiano mmoja Kati Yao wakati mwingine at afanyiwe Vituko
Vya aina gani na mwenzi wake basi uvumilivu Vituko hivyo
ukiwemo Usaliti kwasababu eti anabembeleza penzi,mahaba
kutoka kwa Mpenzi wake.

Nimelazimika kutumia mfano kwasababu makala yangu ya Leo
nitazungumuzia uwendawazimu unaofanywa na baadhi ya madereva
wa mabasi ya kawaida na yaendayo Mkoani ambao pindi
wanapojisikia wanatangaza kuanzisha migomo haramu ya 
kutoa huduma ya usafiri na wakitishia kidogo serikali
inafyata Mkia.

Leo ni Mara ya pili madereva Hao watagoma ,mgomo wa kwanza
ulikuwa ni Aprili Mwaka huu ambao ulileta Usumbufu wa Hali
ya juu kwa wananchi ambao wanatumia huduma hiyo.

Katika makala hii naamanisha serikali ni Mwanaume na
madereva na Wamiliki wa mabasi ni wanawake Katika mahusiano
hayo ambayo nimeyapachika ni kama mahusiano ya kimapenzi.

Katika mahusiano haya ni wazi Mwanaume (serikali) anaonekana
amelewa na mahaba mazito anayopewa na Mpenzi wake huyu
ambaye ni Madereva na ndiyo maana mwanamke amekuwa sasa
anataka kujifanya ana sauti ndani ya nyumba hii(ndani ya
nchi), lolote analotaka kufanya hata Kama yanavunja Sheria
za nchi anafanya kwasababu anaamini Tayari mumewe (serikali)
hapindui.

Na kweli serikali ilisema madereva waende shule wa kasome
,matumizi ya vitochi (mwanamke ) yaani madereva wakaja juu
na mgomo juu ,mume yaani serikali akafyata Mkia na serikali
ikamtuma Waziri wa Kazi na Ajira ,Gaudencia Kabaka na
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Katika
Kituo cha Mabasi ya Ubungo, kwenda Kumbembeleza Mke wake
yaani madereva na Waziri Kabaka akamruka futi Sita Usawa wa
choo ,Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Kuwa lile agizo
alilolitoa kwa madereva wakasome ni lake na Si la serikali.

Na Kamanda Kova na yeye akaagiza madereva na makonda
waliokuwa wamekamatwa waachiwe Mara Moja na kweli
walipachiwa na madereva Wakarudi kutoa huduma mtaani na
kujiona wao ni washindi na serikali imesalimu amri Kwao na
wanajitapa ukikaa nao madereva na makonda Hao.


Kwa tabia hii ya migomo nalazimika Kusema Kuwa ipo siku
Ombaomba 'Matonya' wa mitaani wataamka nao watasema wanagoma
kwasababu tumekataa kuwapatia Fedha wanazotuomba huko
mitaani tunapokutana nako wamekaa huku wakiwa wamekaa chini
na vibakuri au wanatembea na serikali Itatuma viongozi wake
kwenda kuwasikiliza.

Lakini Mbona makundi mengine ya Ambayo yalikuwa
yanaandamana, kuanzisha migomo likiwemo kundi la Wahitimu wa
JKT ,Februali Mwaka huu walivyoonza kuleta Chokochoko
,haraka sana walishughulikiwa na sasa hawasikiki tena?

Au hawa madereva na Wamiliki wa mabasi ni watoto wa mwisho
Kuzaliwa na serikali ndiyo mAana serikali inawadekeza HIvi?
Maana Inasifika Kuwa mtoto wa mwisho kuzaliwa ndiyo uwa
kipenzi cha wazazi na umekerwa sana.

Polisi Kazi yako kulinda Raia na mali zao na Kupambana na
wahalifu sio kufanya Doria kwa waliogoma.Waliogoma Leo siyo
wote ni wachache kwanini serikali isiwafutie leseni hawa
watu?

Nasema HIvi sumu haionjwi,madereva hawa ni wazi wanaonja
sumu.

Kwani madereva wanagoma kutoa huduma mwaka huu tena Katika
Kipindi hiki cha uzandikishaji wa Daktari la kupiga kula
,Fukuto la kuelekea uchaguzi uchaguzi Mkuu Oktoba Mwaka huu
kinafukuta Kwani limekaribia?


Kwani madereva Hao hawakugoma Mwaka Juzi ,Mwaka Jana au
tufanye Januari Mwaka huu?Hivi Mwaka Jana suala la wao
kutakiwa kwenda chuoni kusoma na kupata mikataba hali
kuwepo?

Isiwe hawa madereva wanatumiwa na wanasiasa wanaotoka ndani
ya CCM na vyama vingine kufanya huu uwendawazimu
Wanaojifanya Ambao unasababisha wananchi wanaotumia huduma
ya usafiri huo wa sipende kufanya shughuli za kuzalisha
uchumi wa nchi na mwisho wa siku uchumi wa nchi utetelekea
ili mambo ya hapa nchini Kwenye Ramani ya Kimataifa
yaonekane ni ovyo ovyo hasa tunapoelekea Katika Uchaguzi
Mkuu Oktoba.

Tusipowadhibiti sasa HIvi hawa wahuni wasiotaka kujiendeleza
kielimu kwa visingizio Vya kijinga ambavyo vimesababisha Leo
wanafunzi wa sipende mashuleni wafanyakazi wengine washindwe
kwenda makazi ni na watu wengine washindwe kwenda
kulitumikia taifa Lao kwasababu ya kukosa huduma ya
usafiri.

Ikitokea siku ya Uchaguzi Mkuu wakagoma ,Wapiga kura
watafikaje Katika Vituo Vya kupiga kura ili wapige
kura?Tujifunze Kwenye migomo iliyopita kwanini hatutaki
kujifunza?

Suala la Usafirishaji ni nyeti mabasi yanabeba wafanyakazi
wa kila Sekta  na watendaji wa serikali .

Hivyo kitendo cha kuendesha mgomo wa mabasi  kufanya
watendaji wa serikali wa kila Idara kutufanyakazi  kwa
maana hiyo  serikali siku hiyo ya mgomo inakuwa na
baadhi ya watendaji wake ambao hawajafika ofisini kwasababu
ya kukosa huduma ya usafiri kwasababu eti madereva
wamegoma.

Nyie madereva uchwara wateja wenu ni sisi abiria siyo
serikali, sasa Kama ni abiria na wao wanagombana na
serikali  kwanini madereva wanatuadhibu sisi abiria kwa
kutunyima Kwa makusudi huduma ya usafiri?

Mnachotufanyia ni sawa na Mchunga Ng'ombe ambaye siku zote
anakuwa anatembea nyuma ya Ng'ombe
anaowaswaga   Kuwapeleka Kwenye Josho 
sasa yule Ng'ombe aliyetangulia Mbele agome kuingia
kutumbukia ndani ya Josho na kugoma kwake kutasababisha wale
Ng'ombe waliokuwa nyuma yake kushindwa kusonga Mbele.

Maana yake ukitaka Mchunga Ng'ombe akitaka kumchapa bakora
yule ng'ombe wa kwanza aliyegoma , ni wazi mchungaji
hatoweza kumfikia haraka yule ng'ombe aliyegoma na matokeo
yake mchungaji ataanza kuwachapa  Ng'ombe waliokuwa
Mbele yake ili aweze kumfikia Yule Ng'ombe wa Mbele
aliyegoma kuingia Kwenye Josho.

Kwa Tafsiri nyepesi hapa kosa aliyofanya Ng'ombe wa Mbele
anaadhibiwa Ng'ombe wa nyuma ambaye Hana hatia.

Hivyo Kama madereva wana ugomvi na serikali (Ng'ombe wa
Mbele) kwanini  madereva wanakuja kutoadhibu abiria
ambao ni Ng'ombe wa nyuma ?

Hii dhana  ya Ng'ombe wa Mbele Kutenda kosa halafu
Ng'ombe wa nyuma ndiye adhibiwe ni dhana ya kipuuzi sana na
haikubaliki kwa watu wenye akili timamu na ambao hawana
utapiamlo wa akili.

Madereva wa usafiri wa umma wakumbuke wanaogoma kutoa
usafiri wa umma wakae wakijua wanadhibu pia hata ndugu na
Jamaa zao maana nao ni abiria na hasa pale
wanapousisha  Makundi ya wahuni kuwafanya vitendo Vya
kihuni
madereva ambao hawataki kushiriki mgomo huo.

Ni wendawazimu tu wanaweza kuendesha mgomo wa mabasi kwa
mtindo huo mnaoutumia. Maana Leo Waziri Mkuu Mizengo Pinda
amekubali Leo mchana kukutana Na Nyie mzungumze lakini Nyie
Tayari mmeishagoma na mmeleta madhara Kwa abiria ,watu
tumeshindwa kwenda Kanizini,madarasani na shughuli nyingine
mbalimbali kwasababu ya kukosa usafiri.

Kwani mngetuma wa wakiishi wenu Katika mkutano huo wa Pinda
halafu Nyie mngeendelea kutoa huduma ya usafiri Kama kawaida
huku mkisubiri Yale makubaliano yatakayokuwa yamefikiwa
Katika Kikao chenu na Pinda ,mngechubuka Ngozi?

Hilo ni sawa na mshitakiwa aliyetenda kosa la kuua kwa
kukusudia halafu mwisho wa siku anakiri kosa Hilo.Hata
akikiri kosa haisaidii chochote Kwani Kukiri kwake Hakuwezi
kurudisha Uhai wa marehemu.

Ni serikali gani inao uwezo wa kuwafungia baadhi ya madereva
wanaosababisha ajari kizembe lakini serikali hiyo hiyo
inashindwa kuwabana madereva kwenda kusoma vyuoni?

Lakini nimejiuliza sana kuhusu Kauli ya Waziri Kabaka
aliyoitoa Mbele ya madereva siku walipogoma Katika mgomo
kwamba lile agizo la madereva kutakiwa kwenda chuoni kusoma
zaidi siyo agizo la serikali ni agizo la Mkuu wa Chuo cha
Usafirishaji, hivi chuo cha Usafirishaji Si ni mali ya
serikali?

Binafsi namuunga mkono Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji wa
Taifa, kwa agizo lake la kuwataka madereva warudi vyuoni
wakasome zaidi mAana Hakuna ubishi baadhi ya matendo
yanayofanywa na baadhi ya madereva Kama kujihusisha na ulevi
wa Pombe, mirungi wakati wa Kazi ni wazi Kabisa Kama
madereva hawa watarudishwa vyuoni wakapewe elimu ya kisasa
ni wazi wengine wakaachana na matendo hayo ya ulevi ambayo
yanashusha heshima ya Kazi Yao.

Kwani madereva Hao hawakugoma Mwaka Juzi ,Mwaka Jana au
tufanye Januari Mwaka huu?Hivi Mwaka Jana suala la wao
kutakiwa kwenda chuoni kusoma na kupata mikataba hali
kuwepo?

Hivi serikali hii haina Mbadala wa kupata mabasi ya usafiri
ili yatumike kutoa huduma kwa wananchi wake hadi wananchi
wake wanateseka kwa kukosa huduma hiyo kutoka hawa madereva
ambao kwanza mgomo wao haupo halali kisheria na bado
serikali inaendelea kucheka nao?

Na ninachokiona hapa tangu mgomo wa kwanza ni serikali
inachokiangalia ni Kutafuta utatuzi wa mgomo kwa Kipindi
kifupi tu siyo utatuzi wa muda mrefu.

Nasema hivyo kwasababu haiingii akili ni Aprili tu ,mgomo wa
kwanza uliotikisa nchi umetokea serikali ikajitokeza
kuzungumza nao lakini Leo tena wamegoma tena?

Na Mbaya zaidi hawa Wamiliki wa vyombo Vya usafiri ni Kama
sasa wao ndiyo wapo juu ya Sheria na wao ndiyo kila kitu
wakiamua kugoma bila kufuata Taratibu wanagoma Hakuna wa
kuwachukulia Hatua. Uhuni huu hadi lini?

Ifike mahali sasa serikali itafute njia nyingine ya kuweza
kumiliki mabasi yake yenyewe ili kuondokana utegemezi wa
huduma ya usafiri itolewe na watu binafsi.

Madereva wako Wengi tu mitaani hawana ajira tena wasome
Katika vyuo Vya VETA,kwanini serikali inawabembeleza
madereva wanaotesa wananchi wake?

Kisheria Tunaambiwa pande mbili zinazolumbana zinapoamua
kwenda Kwenye meza ya Usuluhishi basi kila upande Unatakiwa
Kwenda Katika meza hiyo ikiwa na nia safi ya kutoka ufumbuzi
wa tatizo.

Sasa Leo Pinda tumeambiwa anaenda kuzungumza na hao wenye
mabasi ,lakini sote ni mashuhuda upande wa watoa huduma ya
usafiri wanaingia Kwenye kikao hicho  wakiwa hawana nia
safi Kwani Tayari tangu asubuhi wamezuia vyombo vyao Vya
usafiri visitoe huduma na siyo Siri Mimi ni miongoni mwa
waathirika wa mgomo huu.

Niitimishe kwa Kusema hivi, sisi Kama wananchi Tumechoshwa
na hii tabia ya migomo hasa mgomo huu wa madereva
,umetuchosha kabisa na hatuoni serikali ikionyesha Ukali kwa
kuwachukulia Hatua Kali hawa madereva Kama serikali
ulivyokuwa Kali KWA kuwachukulia Hatua wanafunzi wa vyuo
vikuu, wahitimu wa JKT na migomo ya madaktari.Tumechoshwa na
uhuni huu.

Na hawa madereva wanaendelea kutufanyia uhuni huu sisi
abiria tusiyo na hatia kwasababu Tayari wameishabaini
wakitikisa serikali ,serikali na Jamii inatikisika ndiyo
maana wanaendelea na siku zote (Ukicheza na Nyani utavuna
Mabua), sasa Leo tuna vuna Mabula kweli kwasababu serikali
imewachekea sana hawa madereva Kwani ilikuwa na uwezo wa
kisheri  wa kuwachukulia hatua Kali ikiwa ni pamoja na
kuwafutia leseni.

Naishauri serikali isibembeleze penzi la aina hii yaani
huduma ya usafiri kutoka kwa mwanamke huu wa aina hii ambaye
ni madereva kwani ni wazi hapo hakuna mahaba tena ya dhati
zaidi ya mwenzi mmoja kujifanya yeye ndio yeye na anamdharau
mume wake serikali na watoto wa serikali ambao ni abiria
ambao wananyima huduma ya usafiri na mwanamke huyo ambaye ni
madereva.

Mapenzi gani hayo kila kukicha mmoja anajifanya yupo juu ya
mwenzio na anajichukulia maamuzi anayoyataka yeye ambayo
yanaumiza watoto?

Umefika wakati sasa wa Mwanaume yaani serikali kusimama Kama
mwanaume na kutoa maamuzi ambayo yatofautisha nani ni
mwanaume na ni nani ni mwanaume.

Kwa mtazamo wangu mimi namshauri Mwanaume(serikali) , itoke
kwenye ulevi wa kulishwa Dawa za kupumbaza wanaume katika
mapenzi ambazo wenyeji wa Mkoa wa Kagera wanaita ( Shuntama)
na Wenyeji wa Mkoa wa Iringa wanaita Limbwata.

Huyo mwanamke aliye naye sasa yaani madereva wa usafiri wa
umma siyo mwanamke wa kuendelea Kuishi naye ndani ya nyumba
Kwani kupitia matendo yake hayo ya kuvunja Sheria za nchi ya
kuamua kugoma kutoa huduma ya usafiri  ni wazi
ameishalichoka penzi Lako sasa wakati umefika wakumpa talaka
aende kuolewa na Hao mabwana wapya aliyoyapata ambao
wanamtia wazimu wa kuanzisha migomo haramu kila kukicha
ambayo inatesa wananchi wao.

Na serikali itakuwa ni Baba wa ajabu sana kuendelea
kukumbatia Mke wa aina hii yaani hawa wa Madereva hawafahi
kabisa kuendelea Mke wa serikali. Serikali ikachumbie
mwanamke mwingine mwenye elimu,adabu,mzalendo kwa taifa hili
asiye kubali kuingiza siasa uchwara Katika Biashara yake
imuone atupatie huduma ya usafiri ya uhakika .

Ni taifa la ajabu sana hili eti tuna madereva ambao hawataki
kwenda vyuoni kujiendeleza.Mungu atusaidie sana.

Mungu Ibariki Tanzania

Chanzo: Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Mei 4 Mwaka 2015



Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment