Saturday, 2 May 2015

Re: [wanabidii] OIC na AZIMIO LA ABUJA LINAPOPOTOSHWA KUENEZA CHUKI BAINA YA WATANZANIA


Dada yangu pendo kwanza kabisa nikushuru kwa maandiko yako lkn napenda kukuasa unapojifunza jambo usiweweke chuki ndani ya moyo wako dhiki ya yule unayetaka kusikiliza hoja zake, ukifanya hivyo hutaweza kujifunza. pili uislam upo tofauti zana na dhana na yanayotokea leo hii.
 

Pamoja na kuishi na kufanya ibada kama swala, zaka, hija, kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani na ibada nyingi tu,  lakini uislam  pia umetufundisha naama ya kuishi kati ya baba na mtoto., haki mtoto kwa baba pamoja na haki ya baba kwa mtoto.

Hivyo kwa haki ya mume na mke pamoja mke kwa mume. Pia namna ya kuishi kwa haki na majirani ambao ni waislm na waisio waislam.

Hali kadhalika uislam umetoa muongozo wa kuishi katika nchi ya kiislam inayofata sharia za kiislam,  pia imetoa muongozo wa kuishi ktk nchi ambayo si ya kiislam na viongozi wake waislam na hawafati sharia za kiislam.

Hali kadhalika kuna muongozo wa wa kuishi katika nchi ambayo si ya kiislam na viongozi wake si waislama na miongozo yote hiyo inatufundisha kuishi kwa haki kabisa kwa utulivu amani na bila vurugu yeyote ile.

Uislam unatufundisha ujasili wa haki na si ujasiri wa kijinga wa kuwatia watu barabarani kwa kwa ajili ya maandamano au kufanya uasi na kusababisha maafa kwa Jamii.
Tena uislam unafundisha kutowatii Viongozi wa kiislam wapoamrisha maasi, au vurugu hata kama ni mashekhe hatutakiwi kutii.

Tunaona yanayotokea leo na sehem mbalimbali dunia, ni watu wanaovaa makoti ya dini ya kislam haliyakuwa wana agenda zao za kisiasa ambazo zipo tofauti uislam , uislam haurusu kuvaa bomu na kwenda sokoni na kujilipua wengi wanafanya hayo kwa matakwa yao ya kisiasa, uislam kama uislam hauruhusu kumchukia jirani yako hata kama si muislam ikiwa hana nia ovu ya kukudhuru na tunashukuru mungu mambo hayo yote hapa lkwetu hayapo.

Hata mtume aliishi na wasio waislam kwa amani kusaidiana kwa shida na raha pia hata mtume pia alikuwa na jamaa ambao si waislam katika Jamii yake hatukusikia vurugu wala chuki inayozungumzwa leo.

Kinachotokea katika dunia ya leo ni watu kubeba ajenda zao binasfi na kuzivalisha kote la uislam kwa manufaa ya kisiasa , kiuchumi na kadhalika.

Mwisho ni wasihi ndugu zangu pale linapotokea jambo lolote kabla ya kunasibisha na uislam tuangalie kwanza je uislam unazungumziaje hilo jambao halafu tunatakiwa kufanya uchunguzi kwa kina juu ya jambo hilo... 

Kwa mfano usije kumuona mtu kava kanzu kalewa na kukujoa barabarani, ukauhukumu uislam kwa kusema angalia waislam walevi mpaka wanakojoa barabarani, kwanza angalia uislam unazungumzia nini ulevi na uchafuzi wa mazingira halafu ndi utapata jibu.

Ndugu zangu sisi sote ni watanzania hatuna nchi nyingine zaidi ya hii tusiruhusu chuki za kidini kwa njia yeyote hilo kwa vurugu za kidini na chuki zake hazina mshindi,

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment