Friday, 1 May 2015

Re: [wanabidii] Mwl hakuwahi kumkataa Lowassa tuache kutunga uongo

SIFA 13 ZA MWANACCM ANAYEFAA KUSHIKA NAFASI YA RAIS, KANUNI ZA UCHAGUZI TOLEO LA MWAKA 2005 NA MAREKEBISHO YAKE YA MWAKA 2010.

 

1.Awe na uwezo mkubwa wa kuliongoza Taifa kwa kuzingatia uzoefu wake katika uongozi wa shughuli za Serikali,Umma na Taasisi

.2.Awe Mwadilifu,asiyetiliwa shaka juu ya matendo ya uadilifu mbele ya uso wa Jamii ya Watanzania na awe mwenye Hekima na Busara.

3.Awe na angalau kiwango cha Elimu ya Chuo Kikuu au Elimu inayolingana na Hiyo.

4.Awe mwenye upeo na uwezo mkubwa wa kudumisha,kuimarisha na kuendeleza Muungano wetu,Umoja wetu Amani na Utulivu wetu na Mshikamano wa Kitaifa.

5.Awe Mtu mwepesi wa kuona mbali,asiyeyumbishwa na mwenye uwezo wa kufanya uamuzi wa busara kuhusu masuala nyeti na muhimu ya taifa kwa wakati unaofaa.

6.Awe na upeo mkubwa na usiotiliwa shaka kuhusu masuala ya Kimataifa ili aweze kuwa kiungo imara kati ya nchi yetu na Dunia yote kwa ujumla.

7.Asiwe Mtu mwenye Hulka ya Udikteta au Ufashisti bali awe mtu anayeheshimu na kulinda Katiba ya nchi,Sheria,Utawala bora,Kanuni na Taratibu za Nchi.

8.Awe mtetezi wa wanyonge,wa haki za binadamu,mzingatiaji makini wa maendeleo ya raia wote na asiwe na tamaa ya kujitafutia umaarufu wa mtu binafsi.

9.Awe mstari wa mbele katika kuzifahamu,kuzieleza,kuzitetea na kuzitekeleza Sera za CCM na Ilani ya CCM ya Uchaguzi.

10.Awe mpenda haki na awe mtu jasiri katika kupambana na dhuluma na maovu yote nchini.

11.Asiwe ni mtu ambaye anatumia nafasi yake ya uongozi kujilimbikizia mali.

12.Kwa jumla awe ni mtu anaye kubalika na wananchi,,na

13.Awe mtu makini katika kuzingatia masuala ya uwajibikaji wa viongozi/watendaji na asiyevumilia uzembe katika utekelezaji wa majukumu/wajibu waliokabidhiwa ili kuinua nidhamu ya Kazi.Tija na Ufanisi.




--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment