Monday, 25 May 2015

Re: [wanabidii] MKUTANO WA EDWARD LOWASSA NA WAHARIRI

Hajasema atafanyaje na rushwa na ufisadi?
--------------------------------------------
On Mon, 5/25/15, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] MKUTANO WA EDWARD LOWASSA NA WAHARIRI
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, May 25, 2015, 4:54 PM

Waziri
Mkuu aliejiuzulu Edward Lowassa amesafirisha wahariri wakuu
wa vyombo vyote vya habari toka Dar es salaam na kufanya nao
mkutano maalum leo nyumbani kwake mjini Dodoma. Katika
mkutano huo kwa ufupi Lowassa amesema yafuatayo;1.
Amesema Hahusiki lolote na sakata la Richmond na ndio sababu
hata kamati ya Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji.
Amesisitiza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la
kamati ya mwakyembe na spika wa bunge kipindi hicho Samwel
Sitta. Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake
katika kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa
kumchafua. Amechukua muda mrefu kuzungumzia hili la Richmond
na amesema atalisema zaidi Arusha wikendi
hii.2. Anaamini kila mtangaza nia
ana makundi ya kumuunga mkono. Yeye katika mkutano huu na
wahariri leo ameambatana na Nazir Karamagi, Peter serukamba,
Diana chilolo, Hussein Bashe na wengineo huku wengi wakiwa
ni waliojeruhiwa katika serikali ya awamu ya nne akiwemo
Aliekuwa DC Igunga Elibariki Kingu. Pia aliyekuwa mkurugenzi
wa HakiElimu Elizabeti Misoki ametangazwa rasmi kuwa
Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano katika timu ya
kampeni ya Lowassa. Amehoji kwani akina Karamagi wana tatizo
gani na kwani wao sio binadamu?3. Lengo kuu atakaloanza nalo ni Elimu na sio Kilimo
kwanza cha serikali ya JK. Amesema serikali ya JK ilikosea
kuanza na kilimo na kuweka kando elimu. Ametangaza kuwa sera
yake ni Elimu Kwanza.4.
Kuhusu pesa anasema anapata michango ya rafiki zake na
ataendelea kupokea michango hii wakati wote wa harakati zake
na haina madhara yotote.5.
Anasema hatahama CCM na asiyemtaka yeye CCM ndie aondoke
ndani ya chama kwani yeye ana uhakika wa kupata nafasi
kuwania urais.6. Amesema
hatalipa kisasi kwa lolote lililomtokea katika siasa.
Amemwachia Mungu kwani yeye ni mcha Mungu.7. Amesema Arusha itawaka moto
tarehe 30 mwezi huu na kuwataka watanzania kutega sikio
kwani ataanika kila jambo kuhusu mustakabali wa nchi hii na
mipango yake ya kuiinua nchi kiuchumi katika miaka kumi
ijayo.Hayo ni kwa ufupi.
Wahariri wakuu katika media zote kupitia Jukwaa la Wahariri
walikuwepo, na Absalom Kibanda (New Habari) na Nevil Meena
(Free Media) ndio walikuwa waratibu wakuu wa mkutano
huu.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment