Watu wengi huwa wananiuliza nini siri ya mafanikio ya kiuchumi/utajiri? Jee ni vigumu kuwa tajiri au ni rahisi? Jee kuna njia ya mkato? Katika makala hii nitatoa majibu.
Siri ya mafanikio ya kiuchumi au Utajiri ni kuwa na ndoto za kufanikiwa (kuwa tajiri) Ninapenda kila mtu awe na ndoto hii kwani inawezekana. Kisha aweke malengo yaani ni kiasi gani cha utajiri anachokitaka na kwa muda gani. Malengo yanatakiwa yawe makubwa mfano kuwa milionea (kumiliki mali zenye thamani ya bilioni 1.7 ambayo ni sawa na dola milioni 1.) Muda ambao unapaswa kujiwekea ni kuanzia miaka 5 hadi 10. Tafuta fursa ya biashara au mradi wa kufanya kufikia malengo yako. Fursa ya biashara ni kuwa na bidhaa au huduma inayotakiwa na watu wengi. Kwa kuangalia historia ya matajiri wengi wamefanikiwa kwa kujishughulisha na fursa zifuatazo;
- Kumiliki biashara zinazotokana na jambo wanalolipenda (hobi)
- Kuwekeza kwenye majengo( Real estate)
- Kuwekeza kwenye kununua hisa
- Biashara ya madini (Dhahabu)
- Biashara ya mafuta (Petroli)
- Biashara ya kampuni ya simu
- Biashara ya mabenki
- Ushauri wa biashara
- Biashara ya magazeti
- Kufanya Biashara kupitia mtandao wa internet
Fursa zote nilizozitaja hapo juu nitazizungumzia kwa kirefu kwenye makala zangu zinazofuata.
Hakuna njia ya mkato kwa mtu anayetaka kupata mafanikio. Malengo yako yanatakiwa yachukue muda wa miaka 5 hadi 10. Uwe na mtizamo wa muda mrefu. Mawazo ya kupata utajiri wa haraka haraka kwa njia za Freemason, ushirikina kutumia viungo vya Albino, kuuza madawa ya kulevya ni makosa ya jinai ambayo yanaweza kukusababishia matatizo ya kufungwa jela. Kitu kingine Unachotakiwa kukifanya ni kutafuta mwalimu, mtu aliyefanikiwa na mwenye upendo wa kuwafundisha watu. Mfano mwandishi wa makala hii huwa anatoa huduma hii. Tuonane wiki ijayo.
Mwandishi wa makala hii ni Mkurugenzi wa Kampuni ya CPM Business Consultants, Mjasiriamail,Mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara , Kupata ushauri wa biashara, Ili Kupata mafunzo ya ujasiriamali bila malipo kwa email bofya hapa kujiunga;http://tinyurl.com/mshauriwabiashara au Piga simu namba 0784394701
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment