Saturday, 7 March 2015

Re: [wanabidii] MAKADA SITA CCM HAMMO KWENYE URAIS!

Huyu katabazi anajiwekaga ktk mazingira magumu sana jamani, makada 6 ndimo kati yao kuna RaisHappy....shida yako unaandika bila kujali study yeyote kwa hulka yako tu....nani kakwambia kua 6 hakuna Rais....akitokea kati yao nahis utakimbia ukajifiche kamachum


From: 'vitalisy kisandu' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, March 5, 2015 1:10 AM
Subject: Re: [wanabidii] MAKADA SITA CCM HAMMO KWENYE URAIS!

Haya ni maneno tu,hata kwenye Kanga yanapatikana.Time will tell
--------------------------------------------
On Thu, 3/5/15, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] MAKADA SITA CCM HAMMO KWENYE URAIS!
To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, March 5, 2015, 11:15 AM

MAKADA SITA CCM HAMMO KWENYE URAIS!
Na Happiness Katabazi
IBARA ya 18(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ya Mwaka 1977 , inatoa kwa Mwananchi yoyote kutoa maoni
yako.Na Mimi
Leo katika makala hii natumia haki hiyo ya Kikatiba kutoa
maoni yangu.

Ibara Ta 21(1) ya Katiba ya nchi inatoa haki ya kuchagua au
kuchaguliwa kwa Mtu yoyote anayetaka kufanya hivyo. Nami
naheshimu haki hiyo Kwa Watanzania wenzangu hasa makada wale
Sita wa CCM wanaendelea kutumikia Adhabu endelevu ya kufanya
makosa ya kuanza kampeni za urais mapema na kuvunja Kanuni
za Chama hicho.

Makala yangu ya Leo nitajadili    mazingira ya
kisiasa na upepo wa kisiasa ulivyo kwa  makada Sita wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM)  ambao Kamati ya Maadili ya
CCM Mwaka 2014  ili wakuta  na hatia ya kuvunja
kanuni za Chama hicho na kuanza kampeni mapema za urais
Kabla ya muda mwafaka uliopangwa na Chama hicho.

Tujikumbushe  taarifa ya  Kamati ya Maadili ya
CCM  iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa,
Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye Februali 18 Mwaka 2014 
kwa vyombo Vya Habari.

Taarifa hiyo ni hii hapa :  Kati ya tarehe 13/02/2014
na tarehe 18/02/2014 kumekuwa na mfululizo wa vikao kadhaa
vya Chama kitaifa vilivyoshughulikia suala la maadili ndani
ya Chama. Vikao hivyo ni pamoja na Kamati Ndogo ya Udhibiti
tarehe 13-14/02/2014, Tume ya Udhibiti na Nidhamu 18/02/2014
na Kamati Kuu tarehe 18/02/2014.

Waliohojiwa katika mfululizo wa vikao hivi ni wafuatao:- 1.
Ndugu  Frederick Sumaye 2. Ndugu Edward Lowasa 3. Ndugu
Bernard Membe 4. Ndugu Stephen Wassira 5. Ndugu January
Makamba 6. Ndugu William Ngeleja Baada ya kuwahoji
ilithibitika kuwa baadhi ya tuhuma dhidi yao ni za kweli na
hivyo kupendekeza adhabu. Mapendekezo hayo yalipelekwa
kwenye Tume ya Udhibiti na Nidhamu na hatimaye Kamati Kuu ya
CCM ambayo ilitoa adhabu kwa wahusika. Kwa ujumla
waliohojiwa wamethibitika kuwa na makosa yafuatayo:-

  1. Walithibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa
kugombea Urais kabla ya wakati kinyume na Kanuni za Uongozi
na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i). 2.
Wamethibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya
Chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili
ndani ya jamii. Kosa hili nalo ni kwa mujibu wa Kanuni za
Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara
kadhaa za kanuni hizo.

Kamati Kuu baada ya kuthibitisha makosa hayo imewapa watu
wote sita waliohojiwa adhabu ya ONYO KALI na kuwataka
wajiepushe na vitendo vinavyokiuka maadili na iwapo
wataendelea na vitendo hivyo Chama kitawachukulia hatua kali
zaidi. Tafsiri ya adhabu ya ONYO KALI kwa mujibu wa Kanuni
za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara
ya 8(ii) (b) ni:- "Mwanachama aliyepewa adhabu ya ONYO
KALI atakuwa katika hali ya kuchunguzwa kwa muda usiopungua
miezi 12, ili kumsaidia katika jitihada zake za
kujirekebisha."

Kamati Kuu imeitaka pia Kamati Ndogo ya Udhibiti
kuwachunguza na kuchukua hatua kwa wote waliohusika kwa
namna moja au nyingine (mawakala na wapambe) kufanyika kwa
vitendo hivyo vilivyovunja Kanuni za Chama. Aidha, Kamati
Kuu imewaonya vikali Viongozi na Watendaji wa Chama na
kuwataka kujiepusha kujihusisha na matendo ya wanawania
Urais yanayovunja na kukiuka maadili ya Chama, wametakiwa
kuzingatia Kanuni na taratibu.

Februali Mosi Mwaka 2015 , Katika Sherehe za Miaka 38 ya
kukumbuka kuzaliwa  kwa CCM Mkoani Ruvuma, Mwenyekiti
wa Chama hicho taifa, Rais Jakaya Kikwete Katika hotuba yake
ya siku hiyo pamoja na mambo mengine alisema kuna wagombea
urais wazuri tu 'Presidential Material' ila hawajitambui
lakini kuna haja tuwashawishi ili wagombee uongozi.

Lakini Februali 28 Mwaka huu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM Taifa , Nape Nnauye alizungumza na waandishi wa Habari
ikiwa ni muda mfupi baad ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati
Kuu cha siku Moja kilichoketi Jijini Dar es Salaam, ambapo
pamoja na maadhimio mengine yaliyofikiwa na Kamati Kikuu ni
kusimamisha makada wake wa Tatu Professa Anna Tibaijuka
nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu, pia William Ngeleja na
Andrew Chenge nafasi ya ujumbe wa NEC na kuachia Baraza la
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iendelee
kuyafanyia Kazi mashauri dhidi ya makada hao watatu.

Na Makada wote watatu wanakabiliwa na mashauri ya Uvunjifu
wa Maadili ya umma wakiwa ni watumishi wa umma walinufaika
na Fedha za Akaunti ya Escrow  na mashauri Yao yapo
Kwenye Baraza la Sekretarieti ya  Maadili ya Viongozi
wa Umma.

Aidha Nape alisema pia Kamati Kuu imefikia uamuzi wa makada
sita ambao adhabu yao ilikiwa ni miezi 12 ambayo ilikuwa
adhabu hiyo imalizike Februali mwaka huu, kuwa bado makada
sita wanaendelea kuwa chini ya uangalizi wa kuona Kama
Adhabu waliyokuwa wamepewa waliitekeleza Kama waivyoamriwa
waitekeleze na mamlaka ya CCM kwa maana makada Hao bado wapo
Katika Gereza la CCM.

Kwa uamuzi huo wa Kamati Kuu uliyosomwa na Nape tunaweza
Kusema Kuwa uenda Adhabu ile kwa makada wale Sita ambao ni
Lowassa, Membe na wanzake ni endelevu maana Miezi 12
imeishapita Kamati Kuu ya CCM ni Chombo cha juu cha Chama
hicho Katika kufanya maamuzi Mbali mbalimbali ya Chama
hicho.

Binafsi nimekaa chini nimetafari kwa kina Kauli ile ya Rais
Kikwete iliyosema tukawashawishi watu wenye sifa za Kugombea
urais ili wagombee Kwani kuna watu wanasiasa hizo ila
hawajihafamu Kuwa wanasifa hizo ila wanaitaji kushawishiwa
na kuwaambiwa Kuwa wanasifa hizo, Pia tamko la Kamati Kuu ya
CCM.

Nimefikia uamuzi  wa kuona Kuwa wale makada Sita wa CCM
ambao bado wanaendelea kushikiliwa Katika Gereza la CCM Kuwa
hawamo Kwenye kinyang'anyiro cha Kugombea urais kupitia CCM
Mwaka 2015.

Hivi Nyie makada Sita wa CCM akili Zenu  zinawatuma
kabisa eti mtoke  gerezani ambapo mmemfungwa  na
Chama chenu baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja Kanuni
na Maadili ya Chama chenu  halafu mruhusiwe Kugombea na
muwe  rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzainia?

Ni aliyekuwa Rais wa kwanza wa Afrika Kusini marehemu Wilson
Mandela aliyepata  bahati hiyo  ya kutoka gerezani
kutumikia Kifungo ambapo Enzi hizo Africa Kusini ilikuwa
ikiongozwa na serikali ya Makaburu ndiyo iliyomshitaki .

Mandela  Ambaye alikuwa akimpigia nia Uhuru wa watu
weusi kwa ujumla hivyo alikuwa anataka watu  wapate
Uhuru na wajitawale na wale Makaburu waondoke wa waachie
nchi Yao na hatimaye alitoka gerezani na  Kuwa rais wa
nchi hiyo Kwani wananchi wote walimuunga mkono na kukubali
awe rais wao kwasababu alikuwa akiwapigania watu weusi
wanyonge watoke Kwenye mikono ya koloni Kaburu.

Lakini Nyie makada Sita wa CCM ambao  ni dhahiri sasa
Kifungo chenu ni endelevu Kwani hakijulikani kimaisha 
lini , mlifungwa gerezani na Kamati ya Maadili ya Chama
Chenucha CCM kwasababu ya mmlivunja Kanuni za chama chenu
zilizotajwa kwenye  Kanuni ya Uongozi na Maadili toleo
la Mwaka 2010 .

Mlitenda makosa hayo siyo kwaajili ya kutetea maslahi ya wa
CCM wote au Wanzania wote la hasha mlitenda makosa hayo kwa
makusudi tu kwaajili ubinafsi wenu ,tamaa ya kupata urais ni
kwaajili ya kujipanga mapema ili mkilata urais mje
mjinufaishe nyie na wafuasi wenu wa chache sana ndani ya
CCM.
Watoto wa mjini wanasema mlitenda makosa hayo ya utovu wa
maadili kwa kuvunja kanuniz za chama chenu kwa maslahi ya
matumbo yenu yaani 'Tumbo Street' siyo maslahiya Watanzania
na wana CCM wote.


Makada Sita wa CCM ambapo Adhabu yenu ni dhahiri sasa
inaoenekana ni endelevu nawashauri vunjeni kambi Zenu za
urais  na zikalisheni chini kambi Zenu mzieleze ukweli
Kuwa kwa mazingira mnayo yaona HIvi sasa kupitia Kauli ya
Mwenyekiti wa Chama chenu ,Rais Kikwete aliyoitoa Mkoani
Songea, uamuzi wa Kamati wa Februali 28 Mwaka huu, ni Dalili
za wazi kabisa kwamba Kati ya makada Sita mliopo gerezani ni
wazi Hakuna Kada hapo jina lake linapitishwa na CCM Kuwa
mgombea urais .

Waambieni ukweli wafuasi  wenu wajue kwamba mission ya
nyie kuwa marais wa Tanzania,imevurugika vibaya sana tena
wakati 'Pilau ' Ndio  limeiva linataka kupakuliwa watu
wale ili waende kuwashawishi  wanachama wengine
wanaofaha Kugombea urais Kwani Nyie makada Sita Tayari
mmeisha chafuka   na mna rekodi ya Kifungo
cha kuvunja Maadili na Kanuni za Chama chenu na hadi sasa
Kifungo chenu bado kinaendelea wakati umebaki muda mchache
CCM ipitishe jina la mgombea urais apeperushe Bendera ya
Chama hicho.

Hivi  inawaingia akili kabisa makada Sita watoke
kifungoni halafu CCM ipitishe Moja ya jina makada hao
akagombee urais kupitia CCM

Pia Nape ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa kaisha tamka  tena adharani
Kuwa CCM haitaki   mgombea urais
watakayeanza  kwa kumsugua kwa dodoki (yaani anayenuka
tuhuma chafu) na Watanzainia wamechoshwa na ufisadi na utovu
wa Maadili ya viongozi wa umma na miongoni mwa makada hao
wameisha chafuka tuhuma za ufisadi, na wengine kuhukumiwa
kwa makosa kuvunja Maadili na Kanuni za CCM na Tayari na
Kada mwingine Ngeleja licha ya kuendelea kutumia Kifungo
hicho pia mashitakiwa tena Katika Sekretatieti na Maadili ya
Utumishi wa umma kwa makosa ya kunufaika na mgao wa Fedha za
Escrow bila kufuata Taratibu za Sheria ya Maadili ya
viongozi wa umma na kusimamishwa ujumbe wa NEC na kwamba
maana hiyo hata jina lake ikitokea akapitishwa awe mgombea
urais ni wazi hawezi kuudhurulia vikao vya NEC na kujipigia
kura kwasababu amesimamishwa kuudhuria vikao Vya NEC.

Binfasi baada ya kutafakari matamko hayo na kutazama picha
inavyochezwa hivi sasa na uongozi wa juu wa CCM na baadhi ya
wananchi  na baadhi ya wafuasi wa kambi za wafuasi hao
wa makada Sita ,kwa moyo safi nawashauri Nyie makada Sita
ambao Adhabu yenu HIvi sasa haijulikani tena itamalizika
lini,msiende lee kupoteza Fedha na muda wenu bure kwaajili
yakufanya Maandalizi ya Kugombea urais .

Kwani kwa ushahidi huo wa mazingira kupitia matamko hayo
minaona   Hamtoshi Kuwa wagombea urais
kupitia CCM ,mjidiskolifai wenyewe sasa ili muweze kuinusuru
CCM  na nchi  ili CCM Iweze kufanya maamuzi 
mazuri ya kupata mgombea urais anayefaa.

Wakati umefika sasa wa Nyie makada Sita binafsi mjiulize
Kifungo gani hicho kisichokuwa na mwisho? .

Wafuasi wa kambi za makada Hao Sita nawashauri Ameni 
kambi mapema .

Mfano mzuri ni wa msomi wa sheria William Ngeleja ambaye
naye ni miongoni mwa makada Hao Sita wanaondelea kutumikia
Adhabu na Februali 28 mwaka huu,Kamati Kuu imemsimamisha
ujumbe wa NEC na wakati huo ni mshitakiwa  Katika
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kujibu makosa ya
utunjaji wa Maadili ya uongozi wa umma na Machi 3 Mwaka huu,
Ngeleja alipanda Katika kizimba cha Sekretarieti hiyo kutoa
utetezi wake.

Hakuna ubishi Kuwa Tayari Ngeleja ana rekodi  Kutiwa
hatiani kwa makosa ya uvunjaji wa Maadili na Kanuni za CCM
na bado yeye na wenzake wakina Membe ,Lowassa, Sumaye na
wengine wanaendelea na Adhabu hiyo ambayo ni wazi sasa
haijulikani tena itaisha lini na tena ameshitakiwa Kwenye
Sekretarieti ya Maadili ya Umma na wakati huo huo Kamati Kuu
imemsimamisha kuudhuria vikao Vya NEC.

Kwa watu wenye akili timamu tumebaini Kuwa Ngeleja '
Kwishineiiii ' ,Kwani hali hiyo CCM haiwezi kupitisha jina
lake Kuwa mgombea urais kwasababu amepata na Hatia na bado
Kesi ya utovu wa Maadili ya umma inamkabili.

Na kwa Hali  ilivyo sasa na CCM ilivyo nasifa Mbaya
Machoni kwa baadhi a wanachi ,CCM itafanya kila
linalowezekana limsimamishe mgombea urais wake ambaye
aandamwi na rekodi chafu za Kifungo cha utovu wa Maadili au
tuhuma za Rushwa ,Makundi yanayofanya siasa chafu dhidi ya
wenzake na anayetaka kukigawa Chama.

Na Nyie wafuasi wa makada Sita nawasii muheshimu
Kanuni   za CCM ,ili mtoe fursa kwa CCM
ipitishe mgombea urais   safi asiye na kashfa
wala Kutiwa hatiani,mfungwa,mtuhumiwa na mumuunge 
mkono ili muonyeshe  ukomavu wa siasa kwa chama chenu
na mumuenzi Baba wa Taifa, Marehemu Julias Nyerere ambaye
alisema kiongozi anaweza kutoka chama chochote kile ila
kiongozi bora ni lazima atoke CCM.

Niitimishe kwa Kusema Kuwa CCM bado inawagombea wazuri tu
wenye sifa za Kuwa wagombea urais na wala hawajaanza
kujipitisha pitisha mitaani Kama wanawake Malaya wanatafuta
mabwana.

Wawafuate  wachawishiwe wagombee urais ila Katika hawa
makada Sita ambao Tayari wameishanasa Kwenye mtego wa Nyavu
za Kanuni za Maadili ya CCM toleo la Mwaka 2010 na kuendelea
na kuandamwa na tuhuma mbalimbali ufisadi,utovu wa maadili
na hira za kila aina hawafahi Majina Yao kupitishwa na CCM
Kuwa wagombea urais wa CCM . Na huo ndiyo ukweli mchungu
ambao hampendi kuusikia masikioni mwenu.

Kwasababu baadhi ya makada hao Sita miongoni mwao wamekuwa
ni mahiri na mabingwa wa kusukia wenzao mizengwe, majungu,
fitna na kuwazushia  fitna ili wachafuke na wao wao
wanekane ni watu safi Kumbe nao ni washenzi tu wa
tabia  ambao Kutwa wanatumia wapambe wao kulandalanda
Kwenye vyombo Vya Habari na Kwenye mitandao ya kijamii
kuchafua wenzao ili Hali nao ni wachache na wanatumikia
Kifungo Katika 'Gereza la CCM'.

Naunga mkono hoja ya Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama
wa Taifa, Dk.Hans  Kitine Katika mahojiano aliyofanya
na Gazeti la Mtanzania Jumapili mapema Mwaka huu, pamoja na
mambo mengine alisema kwa mtazamo wake yeye anaona makada
wote wote wanaotajwa tajwa Kugombea urais na ambao
wanaotumikia Adhabu ya Miezi 12 hawana sifa za Kuwa Marais
wa  nchi hii kwasababu ni wahuni wahuni tu.

Kweli ni wahuni na hawafahi kwasababu Kama wameshindwa
kuheshimu Kanuni za Maadili za Chama Chao na wakazivunja na
wanaendelea kuzivunja,Majina Yao ya kupitishwa mmoja wao
Akawa mgombea urais Si ndiyo watakuwa vinara wa kuvunja
Sheria za nchi kwa makusudi kwaajili ya kutimiza mission zao
chafu au kuumiza watu kwa wakati huo?

Nafahamu makala hii haitawapendeza makada hao Sita na
wapambe wao ambao baadhi ya wapambe wa kambi hizo
wamewageuza migodi Makada hao sita ya kujipatia fedha kwa
kuwapa taarifa za uongo kuwa watapitishwa kuwa wagombea
urais kumbe uongo mkubwa wanawalia fedha zao na wafuasi
Wengine ni wanafki mchana wao wanajifanya wapo Kwenye kundi
la Kada (X)  usiku anapeleka taarifa za kambi ya kada
huyo kwa kambi ya kada (x).

Na yaona haya na wahusika wakuu wa tabia hii chafu ni makada
wengi wenye jinsia ua kiume tena ni watu wazima wenye wake
na watoto majumbani mwao ambao pia wamekuwa wakinasibu
mitaani na Kwenye vilabu Vya Pombe kwamba mgombea urais
fulani anayemuomba mkono ametumwa na Rais Jakaya Kikwete
kuchukua fomu.

Upuuzi mtupu Kwani hawaonyeshi ushahidi unaonyesha lini,wapi
na saa ngapi Rais Kikwete alikaa na wagombea Hao akiwaambia
wagombea urais na atakubali kuwaunga mkono.

Na baadhi ya wafuasi wa kambi hizo hao wamekuwa Binafsi
nawafanisha makada hao wa kiume sasa na wamawake malaya
wanaouza mihili yao ili wapate fedha.

Mwisho Nimalizie kwa Kusema Kuwa kwa mazingira ya kisiasa
tuliyonayo hivi sasa na jinsi ya Kamati ya CCM inavyoendelea
kuwashughulikia bila huruma makada wake  kwa maoni
yangu Nasema HIvi makada Sita wa CCM mliopo kifungoni Katika
Gereza la CCM hammo Kwenye Urais , mjiondoe mapema na
msitishe kumwaga Fedha kwa wapambe wenu mnaofikiri
wanawafanyia kampeni Kumbe wanawalia Fedha Zenu na Wengi
wanawaandikieni ripoti na kuzidi kuwakusanyia ushahidi Kuwa
licha bado mpo Kwenye Kifungo na uchunguzi lakini bado
mnaendelea kuvunja Kanuni za Chama kutoa Rushwa na kufanya
kampeni za urais Kabla ya wakati.

Ni Ngumu sana  majina yenu  kupitishwa  Mkawe
wagombea    urais Kwani mmejimaliza wenyewe kwa
matendo yenu ambayo yamedhibitisha hamkutana kutii Sheria na
Kanuni za Chama chenu cha CCM bila shuruti.Makada Sita CCM
hammo Kwenye urais!.

Mungu Ibariki Tanzania
0716 774494
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Machi 5 Mwaka 2015.








Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.




--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment