Kwenye simu yangu nimepokea ujumbe unasema hivi:
''RADIO DOUTCHE VELLE YA MJINI COLON UJERUMANI JANA ILITANGAZA DAWA ZA DICLOPA NA DICLOPHENAC NI HATARI KWA MATUMIZI YA BINADAMU. IMEGUNDULIKA VIDONGE HIVYO HUSABABISHA KANSA YA INI NA UBONGO, UGONJWA WA MOYO NA KIHARUSI VIDONDA VYA TUMBO AU KIFO CHA GHAFLA. WATUMIE sms hii UWAPENDAO ili wasitumie dawa hizi''.
Mimi nikamjibu hivi:
''Nashukuru. Madawa yote duniani ni mabaya isipokuwa ile uliyoandikiwa na mganga maana amehakikisha usalama wako ktk kuitumia. Anajua dawa zilizokubaliwa na serikali na zilizokatazwa. Ni hatari kuumwa ukaenda famasi kununua dawa. Nenda hospitali, mwambie dalili ulizonazo, yeye aseme unaumwa ugonjwa huu, aandike dawa. Ukipata madhara mrudie. Ukinunua famasi huwezi kupata cheti chenye jina lako. Wanakwepa kuwajibika na madhara yatakayotokea kwa matumizi ya dawa waliyokuuzia. Mganga anawajibika''.
Ninauleta ujumbe huu humu ili wengi tujue/tukumbuke ukweli huu.
Hizi Pharmacy kwa uhakika lengo lake si kuuza madawa kwa kila aliyeamua ila ni kumuuzia mgonjwa dawa zilizoandikwa na Daktari. Nakumbuka mwanzoni hizi tuliziita Dispensing Pharmacies. Duka za kutolea dawa zilizoandikwa na daktari. Nakumbuka kuna dawa ambazo ungeingia duka la dawa usingeuziwa kabisa dawa Fulani bila maandishi ya Daktari. Utandawazi umetusahaulisha taaluma zetu sasa madawa yanauzwa kama karanga na nguo au soda.
Yako mambo mengi ambayo mganga anapoandika dawa anayafikiria kabla ya kuamua kuiandika dawa.
Kuna kiru kinaitwa maudhi ya pembeni (Side effects: Tunakumbuka Chloroquine. Ilikuwa inaudhi kwa mtu kuwashwa mwilini kana kwamba unachomwa na pin. Hii tulimtahadhalisha mgonjwa au wakati mwingine tulimpa Phenegan na kumwambia hii itakuletea usingizi hivyo meza ukifika nyumbani.
Kuna kitu kinaitwa Toxic Effect. Dawa ikizidi kipimo inakuwa sumu. Wakati mwingine tunampima uzito mgonjwa au tunaimarisha afya yake kwanza kabla ya kumpa dawa Fulani ili isimdhuru.
Kuna kiru tunasema Contra indication. Mama angeweza kuulizwa kama ana mimba au la ili atumie au asitumie dawa Fulani. Mwakati mwingine tunasema usitumie Kileo. Huo ndio ulikuwa mwanzao wa wahuni kubuni Malta. Ina harufu ya pombe ila haina kileo.
Kuna kitu tunaita Drug Interaction. Kuna madawa Fulani hustahili kuyatumia kama unatumia vitu Fulani sababu ni kuwa ama dawa inaweza kuongezeka nguvu ikakuua au ikadhoofishwa uwezo wake isikutibu. Kuna dawa ukizitumia usitumie maziwa mpaka baada ya muda Fulani.
Mtu unapoona mganga anasema chukua cheti ukachukue dawa Fulani ndani ya muda huo ameyapitia hayo yote.
Hebu tujaribu kusoma karatasi ya maelekezo inayokuwa ndani ya madawa. Zamani wakati pharmacy zetu zina nidhamu ya kazi walilazimika kuondoa karatasi hiyo ili mgonjwa azingatie aliyoeleza na mganga tu. Siku hizi hawatoi. Ukisoma utakuta imeandikwa: Dose: as directed by a Physician. Dawa hailiwi kama sukari guru au asali-utaacha ukishiba. Hapana. Inaliwa kama mganga alivyoona inakufaa baada ya utaratibu mrefu.
Nasisitiza kuwa ni hatari mtu kuumwa ukaenda pharmacy na kununua dawa. Mtembelee mganga akutibu. Wala usiende na kumwambia Docta naumwa malaria. Wewe sema naumwa kichwa nina homa kali natapika. Mwache yeye aseme ni Boleria Duttoni. Au Malaria, au Neurosis nakadhalika hayo yote yanaweza kuja na vidalili hivyo.
Elisa Muhingo
0787187507
Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment