Saturday 14 February 2015

[wanabidii] ILITOKEA HAIKUANDIKWA

ILITOKEA LAKINI HAIKUANDIKWA....
AFISA Ubalozi wa Tanzania aliyekuwa akihidumu Liberia na kurudishwa nchini baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa Ebola kule Liberia alipata fursa ya kumshukuru Mungu kwa shukrani maalum katika ibada ya Jumapili ya Kanisa la KKKT Azania Front. Alishuhudia mbele ya waumini jinsi Mungu alivyomponya Ebola kimiujiza. Alipomaliza akamkabidhi Maiki Mchungaji ili akakae,Mchungaji akakataa na kumuelekeza yule bwana ampe Mzee wa Kanisa. Mzee wa kanisa akasema kwa ishara ya kidole kuwa ampe katibu wa Kanisa;katibu wa kanisa akasema kwa nguvu 'Mimi na maiki wapi na wapi jamani mpe yule Mzee Shedele msoma matangazo ya kanisani' Mzee Shedele akasema keshamaliza kusoma matangazo hivyo hahitaji kipaza sauti hadi misa ya jumapili ijayo; kuona vile Mchungaji akaona bora aepushe usumbufu akamwambia yule muumini kuwa hiyo maiki ni yako kanisa limekuzawadia uitumie kutolea ushuhuda kwenye makanisa mengine utakayoenda.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment