Sunday 15 February 2015

[wanabidii] Fwd: Kisiwa- Gereza.



Sent from my iPad


Subject: Kisiwa- Gereza.

                                     Kisiwa- Gereza.
                (Dr. Muhammed Seif Khatib )

      Visiwa ni vipande vya ardhi vilivyoinuka juu ya bahari na kustawisha ardhi
yake kwa ardhi yenye rutuba,matumbawe,mawe au majabali.Vipo visiwa
viotavyo juu ya maziwa na mito ya maji baridi. Visiwa kwaasili yake huwa
haviishi watu ila wanyama,ndege na wadudu wakiwemo nyoka na chatu.Watu
hutoka bara iliyokaribu na visiwa na wageni 'wavumbuzi', maharamia au wakoloni.Kwa
sababu hiyo ya kijiografia na historia visiwa vingi duniani vinavyokaliwa na watu huwa
na wenyeji na wageni.Mara nyingi wenyeji walo wengi hutawaliwa na wageni wachache
walowezi na wakoloni.Baadhi ya visiwa  hapo zamani vimegeuzwa magereza kwa amri ya watawala.Ustaarabu wa sasa na maendeleo kumefanya visiwa vingi kuwa ni vivutio vya
watalii.Visiwa sasa ni vitegauchumi.Visiwa sasa hutoa ajira kwa wakaazi wa visiwa.Visiwa
leo ni burdani na pumbazo za wale wenye fedha.Visiwa leo ni bustani ya pepo ya dunia.Katika karne ya ishirini na moja pasi getarajiwa visiwa kuwa gereza au jela.! Hata
kama vipo visiwa vilivyokuwa magereza sasa ni historia tu.Unguja kipo kisiwa chenye
kuitwa Kisiwa-Gereza. Kisiwa hiki mwaka 1860 Seyyid Majid bin Said ali kitembelea na
kuwapa Waarabu wawili wakimilki.Kisiwa kikawekwa kuwa gereza kwa wale wanaokaidi
amri ya kuzuia biashara ya utumwa.Mwaka 1893 kisiwa hiki kilinunuliwa na balozi wa
Kingereza Lloyd Mathews.Gereza halisi lilijengwa mwaka 1894.Ni bahati hakuwahi
kufungwa mtu kisiwani ingawa jina limeselelea hadi leo. Mwaka 1923 kisiwa hiki
kiligeuzwa kuwa eneo la kuwatenga wale wote  wanaopata ugonjwa wa homa ya manjano.
Hivvyo hospital ikajengwa mwaka huo. Kisiwa hiki kina urefu wa mita 800 na upana
wa mita 230. Lakini duniani vipi visiwa vyengine vilivyogezwa gereza na kuwafunga wale
wanaoaminka kavunja sheria au kutaka madaraka kwa nguvu. ,Baadhi ya visiwa hinvyo ni  Alcatra(1934-1963),Robin, Devil , Rika na vyengine.Hata hivyo hakuna
kisiwa ambacho watu wote au wengi wao wamegeuzwa wafungwa na wao wenyewe bila
kutambua kuwa ni wafungwa? Ni kisiwa kimoja tu duniani ambacho watu wa kisiwa
hicho ni wafungwa.Gereza lao ni kisiwa chote.Kuta za gereza ni kingo za maji ya kisiwa.
Wanafanya wayatakayo ndani ya kisiwa na kuonekana wapo huru. Hakuna askari wa
kuwachunga lakini hawatoki nje ya gereza.Wakulima wanaenda mashambani asubuhi na
kurudi majumbani bila kuchungwa.Wavuvi wanavua, si wa jarife, juya,mishapi au madema
bila kufatwafatwa lakini wafungwa.Wafanyakazi wanaenda makazini si madakitari,
manasi,walimu,makarani,askari polisi na wengine ni wafungwa.Wakwezi, wachuma karafuu, wapiga mijelbi hujitafutia riziki zao kila uchao bila kizuwizi lakini wote ni wafungwa.
Ndoa zinafungwa,sherehe zinafanywa lakini washiriki wote juu ya furha yao ya katika
fungate lakini wote wamo gerezani bila kujitambua. Misiba na maafa inayowafika watu
ndani ya jela ya kisiwani.Kifungo hakiwabagui viongozi wa dini, serekali au siasa wote
wamo vifungoni. Ungetarajia wasomi wanaoishi kisiwani humo wangekuwa na upeo
wa kuona silisila zinazowakaba wao wasomi na jamii yao yote.Madhali mtu anaishi katika
kisiwa mawazo,fikira na akili yake inakuwa matekwa ya matashi ya mtu mmoja tu. Ni kisiwa gani hicho ambacho wale wote wanaoishi humo ni wafungwa? Ni kisiwa cha
Pemba kiliomo ndani ya Zanzibar.Sababu zipi ziliwafanya Wapemba wawe wafungwa
ndani ya kisiwa uhuru? Wamejazwa chuki kwa kupitia kiongozi mmoja wa chama cha
siasa mwenye uchu wa madaraka. Nini wameambiwa? Pemba imetupwa na serekali
Ya Mapinduzi ya Zanzibar.Hakuna maendeleo pesa yote ya karafuu yao inajenga
Unguja.Madaraka ya kuongoza nchi yameshikwa na watu wa Unguja.Umasikini wa
Wapemba unasababishwa na Waunguja. Wakati fulani baadhi ya Wapemba wakataka kujitenga.Wakaandika barua huko Umoja wa Mataifa ili wapewe Pemba yao huru.
Haya yote yamewaingia kichwani,akilini na
moyoni mwao na kuwa wafungwa wa mawazo hayo potofu.Hawasikii la muadhini
wala la mtekamaji msikitini.Matokeo yake Wapemba wote hawana uwezo tena wa
kifukiri wenyewe na kuamua mambo yao wanayoyaamini.Kiongozi wao ndiye Nabii
wao ndiye Mungu wao.Nini matokeo yake ni chama chake ,kimechukua majimbo yote ya
ubunge na uwakilishi pamoja na udiwani. Ungetarajia Pemba ingekuwa pepo!.Sasa
serekali ni ya Umoja wa Kitaifa, mawazir wao wamo serekali ni na yeye mwenyewe
ni mtu pili katika uongozi wa kitaifa.Jee Pemba imejaa mito ya asali na maziwa?Chama
chao ndiyo chenye wanachama wengi huko Pemba, hupishana kama siafu kwa wingi. Huko
hakuna masikini? Huko ni kisiwa kuitakatifu?Huko hakuna uhalifu? Serekali ya Mapinduzi ya Chama cha Mapinduzi kimewamomboa tokea wakati wa Afro.Shirazi na leo wanaweza
kwenda watakako duniani.Unajua kiasi gani Wapemba wanapata kwa kuuza karafuu kwa
kila msimu? Ni mabilioni kwa mabilioni ya fedha.Fedha hizo wanapewa watu wa Unguja.
Ni wao wana.ipwa lakini haziweki bengi Pemba.Fedha zinajenga maghorofa Dar es Salaam.
Tanga,Arusha na Unguja. Unajua majumba ya ghorofa yalojenggwa Chake,Wete,Mkoani  
kama ya.ivyojengwa Kikwajuni,Michenzani,Mpapa na kadhalika. Viwanja vya kisasa
vya watoto kipo Pemba Tibirizi na Unguja Kariakoo. Uwanja wa mpira wa kisasa upo
Gombani Pemba na Aman pia Unguja. Barabara za lami zimetandikwa Pemba yote na Unguja karibu yote. Umeme wa Pemba unataka Pangani kuzama baharini na kuibukia Pemba.Ule Unguja umeanzia Morogoro na kuibukia Fumba huko Unguja.Maji ya kunywa na kutumia majumbani yale ya Pemba hutoka Pemba na kubaki Pemba na ya Unguja hutoka
Unguja na yakatumika Unguja.Unguja hakuna viwanda vya saruji,chuma,mabati na mbao.Unguja nununua bara na Pemba hununua bara.Yapo mambo mengine ni ya kihistoria
hakuna wa kuyabadalisha leo.Unguja na Pemba ni visiwa tofauti, Sultan Seyyid Said ndiye
aliyeviunganisha kwa makali ya upanga wake.Siyo nchi moja, siyo shirikisho siyo Muungano.Waunguja na Wapemba walikuwa raia waote wa mtu mmoja tu Seyyid Sultan.
Pemba kuwa karibu na Tanga na Unguja karibu na Dar es Salaam wakati Unguja na
Pemba zipo mbali.Beit el Ajaibu kujengwa Unguja na kuwa isijengwe Pemba si uamuzi
wa watu wa Unguja. Ni Sultan Barghash yeye ameamua hivyo. Nadhani Wapemba sasa
wanahitajika kuwa uhuru kimawazo,kifikra na kiakili.Wasikingwe fukwe za bahari katika
kulikimbia gereza lilowazingira kwa kisiwa chote.Wafikri wenyewe,watafakari wao
wenyewe na waamuwe wao wenyewe.Watafautishe vitu kirangi,kiumbo,kiharufu na kitabia.
Wapo Wapemba wachache walojitambua na kuamua kulikimbia Gereza la Kisiwa cha Pemba.Hawa wapo Huru!











E








Sent from my iPad

0 comments:

Post a Comment