Mwnangu Happy, hapa ulipofika unajidhalilisha,unadhalilisha waaalimu wako wa shule ya msingi, sekondari na taaluma ya uandishi wa habari unaomtaka mwanahabari kuvaa miwani ya uchambuzi.
Ananilea Nkya
E-mail:
ananilea_nkya@yahoo.com--------------------------------------------
On Mon, 2/23/15, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <
wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] WAHITIMU MAFUNZO JKT KUMBUKENI MLIKULA KIAPO CHA UTII
To: "WANABIDII" <
wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, February 23, 2015, 6:15 AM
WAHITIMU MAFUNZO JKT KUMBUKENI
MLIKULA KIAPO CHA UTII
Na Happiness Katabazi
FEBRUALI 15 Mwaka huu, wahitimu wa Jeshi la Kujenga
Taifa(JKT), kupitia Mwenyekiti wa Umoja wao huo,George Mgoba
aliutangazia umma Kuwa ikifika Leo Februali 23,23 na 25
Mwaka huu, wahitimu wa Mafunzo ya JKT watafanya
maandamano ya usiku na mchana kushinikiza
kuonana na Rais Jakaya Kikwete ili awasikilize matatizo
yanayowakabili ikiwemo ukose tu wa ajira.
Mgoba ambaye vyombo Vya Habari Vya Juzi na Jana
vimeripoti habari iliyowanukuu watu wake wa karibu
ambao walidai Mgoba Amelazwa Katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili kwasababu alitekwa na watu wasiyojulikana
na kumjeruhi na kumasababishia maumivu makali mwilini
Mwake.
Na Tayari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Jana amenukuliwa na vyombo Vya Habari akisema amepata
taarifa za tukio Hilo na Ofisi yake inafanya uchunguzi na
uchunguzi ukikamilika atatoa taarifa.
Kwa Kuwa kisheria Jeshi la Polisi ndiyo lenye jukumu la
Kutolea taarifa matukio ya Uhalifu, hivyo sote Hatuna budi
kusubiri taarifa hizo za uchunguzi zitakazotolewa na jeshi
la Polisi Kama ni kweli alitekwa na kufanywa unyamana wa na
kwanini watu Hao walifikia Hatua hiyo ya Kutenda hivyo
Kama inavyodaiwa.
Pole sana Mgoba Kama kweli umekutwa na mkasa huo.Pole sana
ila naamini Kama kweli umefanyiwa unyama huo wahusika
watabainika na watachukuliwa Hatua kwasababu Jeshi la Polisi
ni Chombo makini na kina uzoefu mkubwa wa kuchunguza matukio
ya kihalifu tena zaidi ya tukio Hilo watu wanalodai
umetendewa na washitakiwa uwa wanakamatwa na kufikishwa
mahakamani.
Tukiachana na hayo , Turejee Kwenye mada yetu ya Msingi
ambayo inawauliza hawa wahitimu wa JKT Leo watafanya yale
maandamano Yao Kama walivyotuaidia kwa mbwembwe nyingi licha
tayari mpiganisha vita wao (Mgoba) kaisha jeruhiwa na Katibu
wao amekamatwa Kabla ya 'vita 'kuanza?
Inaelezwa Kuwa Askari Wawapo vitani ,Askari mmoja akifa au
kujeruhiwa wale Askari waliokuwa salama morali ya kupigana
vita ndiyo inapanda na wanazidi kupigana vita kwa moyo
na Nguvu zao zote.
Sasa Leo hii inakuwaje kwa Nyie wahitimu wa JKT ambao
mlijinasibu Kuwa mmepata Mafunzo ya kijeshi mna rudi wote
mstari wa nyuma Kabla ya tarehe ya kuanza kupigana
'vita 'kuanza kwa kisingizio eti kiongozi wenu ametekwa na
kuumizwa?
Ndiyo mañana Katika makala yangu iliyokuwa na kichwa cha
Habari kisemacho: ' WAHITIMU MAFUNZO JKT MNACHOKITAUTA
MTAKIPATA SOON'.
Ndani ya makala hiyo nilieleza wazi Nyie siyo
Wanajeshi na hamjapata Mafunzo ya wanayapata Askari wa JWTZ
ndiyo mAana kwanza mipango yenu ni dhaifu, hamna nidhamu ya
kijeshi na mnadhalilisha wakufunzi wenu waliowafunza JKT na
uenda mlijifunza kupigana na mishale.
Baadhi ya watu waliojitambulisha ni wakufunzi wa Mafunzo
hayo baada ya kusoma makala hiyo walinipigia simu na
kumitolea vitisho na matusi juu, wala sikutishika na wengine
baada ya kusikia Mgoba ametendewa unyama walinipigia na
kunishukuru kwa kuwataadharisha na kwamba kilichomkuta Mgoba
limewaogopesha na hawatashiriki tena maandamano hayo Kwani
wamebaini miongoni mwa wakufunzi wa JKT wameanza kusalitiana
hivyo hawataki ugomvi na dola wala kuandamana kwanza
wanabiashara zao zinawaingizia kipato na kwamba miongoni mwa
wahitimu Hao wanaajenda za kutumiwa na baadhi ya vyama Vya
siasa kulea vurugu nchini wamewabaini.
Tangu niliposikia Jemedali wao Mgoba Kuwa ametekwa
nimejiuliza ,Jemedali gani anatekwa kirahisi hivyo
tena na watu wanaodaiwa ni wanawake?
Nimebaki na Mashaka Je taarifa za kutekwa kwake Je ni Sinema
ya Kihindi ambayo Sinema ya Kihindi ni kawaida
stelingi anakufa Badala ya kusave.
Mgoba alidai wanamafunzo ya kijeshi na wameiva kimafunzo
inakuwaje alizidiwa akili na Hao watu wasiyojulikana Kumteka
kirahisi hivyo wakati yeye ni Jemedali wa Askari wale zaidi
ya Miaka 200 ambao walijinasibu Kuwa wanamafunzo ya
kijeshi?
Yaani Jemedali gani wa 'vita' anakubali kuitikia wito
wa kila mtu anayemuita na kwenda kuonana nae?
Kama Jemedari 'Mgoba' amekubali kuitikia wito huo ambao
tumeelezwa Kuwa ni wa wanawake ni kweli basi Hao watekaji
wanawake ni kiboko na wakiamua hata Leo hii kutumia mbinu
hiyo hiyo kuwaita baadhi ya wahitimu Hao ,basi
watawadhuru wahitimu wote kwa njia hiyo ya
kidharimu.
Mininachofahamu hivi sasa kutekwa wanatekwa watu wenye
ulemavu wa ngozi Albino ambao viungo vya ni dili kubwa na
serikali na Jamii kwa ujumla Inaangaika kutokomeza
mauji hayo.
Wengine nao baada ya kusikia taarifa Kuwa Mgoba katekwa
wakasema amejiteka Hakuna wakumteka na asitake 'kucompite'
na albino na kwamba anataka kuaribu vichwa vya habari vya
magazeti na kwamba eti Mwenyekiti wa Chama cha Malbino
akimsikia hata mwelewa kabisa kwasababu wanaotekwa ni Albino
na taifa lipo vitani kulaani mauji na utekwaji wa
Albino na siyo watu wasiyo na ulemavu wa Ngozi Kama
Mgoba .
Wengine wakasema Angekuwa ametekwa na kutupwa katika
machimbo ya madini kama Geita wangesema
wafanyabiashara wa madini walikuwa wanataka kufanyia mwili
wake mambo ya kishirikina lakini Mgoba anadai katekwa na
kutupwa msitu wa Mkoa wa Pwani ambako hakuna machimbo ya
madini kuna machimbo ya Kokoto ,wanapata mashaka na taarifa
hizo.
Wasiwasi wangu kwa wahitimu wa mafunzo ya JKT ambao
mnajifanya mnakiherehe na mpo juu juu kama ngoma za daku
katika huo umoja wenu wa kujifanya mnaakili zaidi kuliko
wale askari wanaolifahamu ndani nje majeshi yetu.
Jitambueni kuwa nyie bado mi watoto wadogo sana, subirini
maelekezo kutoka kwa baba yenu (serikali) ,mkitaka
kulazimisha kupewa mnachokitaka mtaonekana ni mamluki.
Askari mdogo yaani mwenye Cheo cha chini siku zote anapokea
maelekezo na amri kutoka kwa afande wake anayemzidi cheo na
anatakiwa atekeleze maelezo hayo.
Hayo mambo ya kulazimisha na vitisho mnayotaka kufanya
siyo mazuri, Kwani Nyie bado ni watoto wadogo mnataka
Kubeba Mzigo mzito ambao hamuuwezi Kuubeba.
Kwanini watu wasianze kuamini mnatumiwa na mabwana Zenu
kufanya hayo Mlivyokuwa mmepanga kuyafanya? Siku 'mkifinywa'
mtawataja hao mabwana zenu wanaowatumia kufanya hayo
mliyokuwa mmepanga kuyafanya Leo.
Mkae mkijua mkivuka mstari serikali itawashughulikia na Hao
mabwana Zenu wanaowatumia siku mkianza kushughulikiwa
wasianze Kulalamika Kuwa Jeshi la Polisi limetumia Nguvu
nyingi kuwadhibiti wahitimu Mafunzo ya JKT.
Nawashauri achaneni na mawazo hayo ya Kudai kupatiwa kitu
kwa mashinikizo mwisho wa siku mtakao kuja kuaribikiwa ni
Nyie binafsi siyo siyo mabwana Zenu wanaowatuma kufanya hayo
mnayoyafanya.
Mwenye masikio na asikie na atakayeshupaza shingo na
ashupaze ,ushauri wangu Ndio huo wahitimu Mafunzo JKT rudini
mtaani mkafanyie kazi ujuzi mlioupata mlipokuwa JKT na
sio kujiunga Katika umoja huo ambao nadiriki Kusema Malengo
ya umoja huo yatazamwe upya na mamlaka husika kwasababu
Tayari kupitia tamko Lao Katika vyombo Vya Habari
limeonyesha umoja huo sio wa kuachwa HIvi hivi tu bila
kutazwa kwa karibu na vyombo Vya dola.
Pole Mgoba kwa kuugua,Nina Imani waliokufanyia uhuni huo
Kama inavyoelezwa na Hao watu wako wakaribu watakamatwa na
Sababu ya wewe kufanyiwa hivyo utajulikana.
Waswahili wanamsemo wao usemao 'usiku wa deni haukawii
kukucha'.
Jumatatu Ndio Leo Imefika wale wahitimu wa Mafunzo ya JKT
ambao mlinitolea lugha za vitisho kuwa
mtaniua,mtanibaka,mkatumia njia ya kijinga kabisa ya
kunitongoza kwa wingi Kwenye Mtandao,na kunisifia Mimi ni
mwanamke mrembo mnaitaji kuonana na mimi haraka ili mnidhuru
kirahisi bila kufahamu na Mimi ni 'Mkubwa wa akili'
kuliko Nyie , nikawa nawacheka Ujinga.
Na hadi Jana usiku mkajitamba Kuwa lazima mtanidhuru na
mtaandamana na kwamba Hakuna cha kuwazuia lazima Leo
mtafanya maandamano hamuogopi Polisi Kwani kwenu Nyie
'Polisi ni Raia wakakamavu.
Sasa usiku wa deni ndiyo umeishakucha ingieni uwanjani
tuwaone na msitoe kisingizio cha Mwenyekiti wenu anaumwa
kuumwa kwake yeye hakuzui mambo mengine ya Jumuiya yenu
yasimame na msipoingia mtaani Leo kufanya hayo
maandamano yenu haramu ya usiku na mchana
nitawafananisha na 'mademu' mAana siku zote madem ndiyo
wamekuwa na sifa ya kutoa tisho vikubwa lakini wakiminywa au
kutishwa kidogo wanafyata Mkia.
Nitoe rai kwa Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi,Jenerali
Davis Mwamunyange atoe tamko la kufunga mjadala huu
unaondeshwa na wahitimu wa JKT kwani ni wazi sasa matendo
yao yanadhihirisha yanataka kucheza na ofisi ya Yake ya JWTZ
nakutaka kumwandikia rekodi mbaya ya kustaafu kwako.
Sasa ni wazi kupitia Kundi Hilo la vijana waliohitimu JKT
kuna siasa chafu nyuma yake ambazo zinadaiwa kufanywa na
Chama Kimoja cha siasa ambacho chama hicho kimekuwa ni
mahiri sana ya kuratibu migomo,maandamano hapa nchini.
JKT na JKU ni sehemu ya JWTZ na kiongozi wa JWTZ ni
wewe Mwamunyange .Leo Wahitimu wa JKT wamefanya
waliyoyafanya na wameanika nia yao ovyo ya kutaka kusaliti
viapo vyao na ukosefu sa adabu ws kuwaamlisha viongozi wao
wafanye wanavyotaka wao badala Viongozi waaamlishe
wanavyotaka wao, wasipodhibitiwa hawa siajabu kesho
tutasikia nao wahitimu JKU nao wakaibuka kwa madai kama haya
na kwa njia haramu Kama hizi za kutumia njia haramu za
kuingiza siasa chafu kwa kutumia Majina ya majeshi yetu.
Jeshi Lina Sheria na Mahakama zake (Court
Martial) .Askari anapokosea kijeshi upelekwa Katika Mahakama
hiyo na kuadhibiwa kwa mujibu wa Sheria za kijeshi. Hivyo
wahitimu Wa Mafunzo ya JKT msitake kuingiza masuala ya
kijeshi uraiani, waende wanawasilishe Madai Yao ambayo wao
wanaona ni ya Msingi kule Jeshini tujue Moja.
Uliona wapi mtoto anamtishia nyau baba yake? Nadhani wenye
mamlaka watachukua hatua Leo wamefanya
vijana wa JKT Kesho tunaweza kusikia wahitimu wa JKU
,Naomba hatua zikichukuliwe na hatua zikisha chukuliwa
ni wazi wale wanaowatuma watajitokeza kuwatetea.
Wahitimu wa Mafunzo JKT Kumbeni mlikula kiapo na
Askari yoyote anayesaliti kiapo cha utii kwa serikali yake
adhabu yake ni moja tu na iko wazi ni kifo.
Uwenda Hilo mmelisahau ndiyo maana mmeamua
kufanya hayo Mlivyokuwa mmepanga kuyafanya Leo .Acheni Kwani
ni wazi mtaumia Kwani Tanzania Inaongozwa kwa mujibu
wa Sheria na ni nchi yenye Amani na
Watanzania na vyombo vyao Vya Ulinzi na Usalama hata siku
Moja havitakubali kuwaona Nyie au Mtu yoyote anafanya
vitendo Vya kuhatarisha Usalama wa taifa hili halafu
wakawaacha salama lazima watawashughulikia kikamilifu.
Kumbukeni pia Msemo usemao'Nazi haishindani na jiwe,lazima
nazi itapasuka itapasuka.
Hivyo Nyie wahitimu wa mafunzo ya JKT ni Nazi na serikali ni
jiwe.Acheni kutumiwa vibaya na Chama hicho cha siasa kwani
mwisho wa siku mtakao umia ni Nyie sio wao kwasababu Nyie
ndiyo mnaingia mstari wa Mbele wao wanakuwa wamejificha
nyuma.
Na kwa taarifa yote mnayoyafanya yanafahamika, ila kwakuwa
mnajifanya mmenificha Gizani hamuonekani Kumbe mmenificha
Kwenye mawingu mnaonekana.
Acheni wazimu huo nendeni mkafanyekazi za kuwaingizia kipato
na kujenga taifa achaneni na tabia ya kutumia utambulisho wa
Jeshi kutumiwa kufanya saisa chafu zinazo hatarisha Usalama
wa taifa hili.
Mwisho vitisho vyenu dhidi yangu si viogopi,nilishatishiwa
sana na watu wenye mabavu zaidi yenu ila kwakuwa nafanyakazi
yangu kwa maslahi ya taifa langu na Kutenda haki na
kuwarudisha kundi ni Nyie wahitimu wa Mafunzo ya JKT
mnaotaka kusaliti Viapo vyenu Vya Utii kwa serikali ya
yetu,Mungu atanilinda na wala siwaogopi niwaakikishie nipo
imara na ni nafanya mambo yako Kama kawaida.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Februali 23 Mwaka 2015.
Sent from my iPad
--
Send Emails to
wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+
unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+
unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to
wanabidii@googlegroups.comKujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+
unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+
unsubscribe@googlegroups.com.For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment