Sunday, 1 February 2015

Re: [wanabidii] TAMKO LA SHIRIKA LA TSSF DHIDI YA UNYANYASAJI WA KIUTU ALIOFANYIWA PROF. IBRAHIM LIPUMBA

Kama ni unyanyasaji au ukiukwaji wa haki za raia, polisi wamefanya hivyo mara nyingi sana na watu au makundi mengi tu. Naomba nikuulize wewe Fadhil kwa nini uamuae kumchagua Sheikh Ponda tu? Kosa unalowalalamikia hao TSSF na wewe unalo tena hata kuzidi hao TSSF. Siku zote waswahili husema unapomuonyesha kidole mwenzio ujue vinne vinabaki vimekuangalia wewe. Tuache kuwa na vijilalamiko visivyokuwa na kichwa wala miguu tuangalie kitu cha msingi wanacholalamikia wao kwanza badala ya kutafuta vijisababu vingine. Kwanza sina uhakika kama unafahamu ni lini hiyo TSSF ilianza hapa Tanzania pili mipaka ya katiba ya iko vipi na ina wataalamu wenye calibre zipi nk. Labda nikukumbushe baadhi ya matendo ya polisi kwa raia katika kukiuka haki za binadamu.
1. Mauaji ya wapemba zaidi ya 20 wakati wakilalamikia uchaguzi
2. Mauji ya kijana katika mkutano wa Chadema Morogoro
3. Mauji ya Mwangosi Iringa
4. Mauji ya wafanyabiashara wa Mahenge msitu wa Pande
5. Kuvurumisha mabomu na kuwacharaza viboko na mateke rai kwenye maandamano ya wapinzani
6. Mauji ya waislamu mwembechai
7. Kuwapiga na kuwaibia wanafunzi wa vyuo vikuu wakati wa migomo
8. Kuwabambikia kesi watu wasiokuwa na makosa nk

2015-02-01 21:42 GMT+03:00 fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>:

Mbona hatukuwaona kutoa matamko kwa shelkh ponda alipopingwa risasi au hana damu na nyama.

On Feb 1, 2015 8:25 PM, "Oksana Spice" <worldngojobs@gmail.com> wrote:

TAARIFA KWA UMMA
YAH: TAMKO LA SHIRIKA LA TSSF DHIDI YA UNYANYASAJI WA KIUTU ALIOFANYIWA PROF. IBRAHIM LIPUMBA, MWENYEKITI WA TAIFA WA CUF, NA UKAWA
Shirika la Kusaidia Jamii Tanzania (Tanzania Social Support Foundation) linatoa tamko la kulaani vikali vitendo vya Jeshi la Polisi wa Tanzania vinavyofanyika kwa ajili ya kuwanyanyasa viongozi, wanachama, wafuasi, na wapenzi wa vyama vya upinzani hapa Tanzania.
TSSF inaamini kwamba vitendo hivi haramu vinavyofaywa na Jeshi la Polisi wa Tanzania, ni vitendo vya kuididimiza Demokrasia ya Tanzania na pia vitendo hivi havilengi kuitunza amani bali ni kuiharibu na kuipoteza kabisa.

Shirika la TSSF linaamini kwamba, Amani haipatikani kwa kunyanyasa na kuwatesa raia, wala amani haipatikani kwa matumizi ya mtutu isipokuwa kwa mazungumzo na kuheshimu Katiba ya Nchi pamoja na makubaliano yanayoafikiwa kati ya serikali na wananchi,au taasisi yeyote katika lengo la kuhakikisha kwamba maslahi ya Tanzania na Wananchi wake yanalindwa, kutetewa, na kupatikana wakati wote.

TSSF inaamini kwamba Jeshi la Polisi wa Tanzania lilikiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vitendo na vifungu vya katiba ya Tanzania ambavyo vimevunjwa ni kifungu cha 18, 20, na 21.

Shirika la TSSF linaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya mageuzi ya kimfumo katika uendeshaji wa shughuli za Jeshi la Polisi hapa Tanzania, kufanya marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na Sheria ya Makosa ya jinai ya mwaka 1985 ili kuvipa vyama vya siasa uhuru wa kufanya kazi zake bila ya kuingiliwa au kukandamizwa na serikali au chama kilichopo madarakani dhidi ya vyama vingine.

TSSF inawaomba wananchi, asasi za kiraia, na watu wote wenye mapenzi mema kuungana kwa pamoja kwa kupinga vitendo hivi haramu na kuhakikisha kwamba demokrasia ya Tanzania inakomaa.

Imetolewa;-

Uongozi
Shirika la TSSF.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment