Sunday, 1 February 2015

Re: [wanabidii] RAIS AJAYE ASIPOTOKA CCM, NCHI ITAYUMBA - KIKWETE

Kauli ya Rais ni ya wale walio na mtazamo kuwa nchi hii inatawaliwa kwa kejeli, ushawishi wa maneno mengi kuliko vitendo, laghai na vijembe vya aina ya mipasho . . . .  Tanzania ipo ktk mwelekeo wa Mantiki, ambapo kila jambo litatimia kwa mithili ya vipimo na viwango vya Mizani . . . huu ni wakati ambao wapo Watanzania wengi sana wenye vigezo binafsi ambavyo ni halisi, imara na vya uhakika ktk uongozi na sio majigambo na kejeli ktk majukwaa


Sent from my LG Mobile


------ Original message------

From: 'Abdul Karim' via Wanabidii

Date: Mon, 2 Feb 2015 6:21 PM

To: wanabidii@googlegroups.com;

Subject:Re: [wanabidii] RAIS AJAYE ASIPOTOKA CCM, NCHI ITAYUMBA - KIKWETE


Nchi iyumbe mara ngapi wakati mpaka sasa nchi inaenda kama lori la mkaa lililokata centre bolt!
 

From: 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii >
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, February 2, 2015 12:39 PM
Subject: Re: [wanabidii] RAIS AJAYE ASIPOTOKA CCM, NCHI ITAYUMBA - KIKWETE

Nchi itayumba???
Sasa imetulia???. Inaenda vizuri??? Hii kali kweli! Ninaamini nchi inaweza kuzama kabisa kama CCM itatoa rais atokanaye na mtandao. Uwezekano wa kupata Rais kutoka CCM ambaye anaweza kwa kuanzia akaunda serikali ndogo na kupunguza marupurupu ya wanasiasa ambayo ndiyo yamelifikisha taifa hapa ni mdogo. Uwezekano wa kumpata rais kutoka CCM ambaye hatatokana na fedha za ESRCOW ni mdogo sana. Uwezekano wa kupata rais kutoka CCM anayeweza kuwauliza watangulizi wake na familia zao waeleze walikopata mali hizo ni mdogo. Na hayo ndiyo yanaliyumbisha taifa tayari.
Basi tukae kwa namna mpya na kukubaliana namna ya kumpata rais. Kupitia kampeni hizi hatutampata tunayemtaka wa kulifaa taifa hili.
Elisa
--------------------------------------------
On Mon, 2/2/15, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] RAIS AJAYE ASIPOTOKA CCM, NCHI ITAYUMBA - KIKWETE
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, February 2, 2015, 10:39 AM

RAIS
AJAYE ASIPOTOKA CCM, NCHI ITAYUMBA - KIKWETE
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Kikwete
amewaagiza viongozi wa chama hicho kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinashinda
katika uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba
mwaka huu.Dkt Kikwete ametoa agizo hilo katika
uwanja wa Majimaji mjini Songea ambapo zimefanyika sherehe
za maadhimisho ya miaka 38 ya chama hicho.Akimnukuu mwalimu Nyerere, amesema
kuwa Rais wa Tanzania anaweza kutoka chama chochote lakini
Rais bora ni lazima atoke CCM hivyo amewataka viongozi wa
chama hicho kuhakikisha wanafanya mikutano na kuwatembelea
wananchi ili kujua matatizo yao kama anavyofanya Katibu Mkuu
wa Chama hicho Abdulrahman Kinana.Aidha ameonya kuwa wana CCM
wanatakiwa kutambua kuwa endapo CCM haitashinda, nchi
itayumba na huenda CCM isibaki kama ilivyo, kwa hiyo ni
jukumu lao kuhakikisha CCM inaendelea kubaki madarakani kwa
kila jitihada.Amewataka wawe
makini wakati wa kuteua wagombea hususani katika nafasi ya
urais ili wapate mgombea mwenye uwezo wa kuendelea kujenga
umoja ndani ya chama na taifa kwa ujumla, na pia mwenye
uwezo wa kuongoza Tanzania na watanzania wakamkubali."Msifanye makosa katika kupata
mgombea, chagueni mgombea atakayekubalika na mwenye uwezo,
hata kama yupo lakini hajajitokeza, siyo vibaya kumshawishi
kama mimi nilivyoshawishiwa…" amesema Kikwete.Amewataka viongozi wa chama hicho
kuwashawishi wanachama wote kujiandikisha katika daftari la
kupiga Kura kwa mfumo wa BVR ili waweze kushiriki uchaguzi
huo wakiwa na vitambulisho vipya.Amesema "Kwa mahesabu yaliyopo CCM
ina wananchama zaidi ya Milion 6, tukiwaongeza na hao kama
milioni 2 hivi, itakuwa million 8, tayari tutakuwa na mtaji
wa Kura million 8 za kuanzia, na hao million 8 kila mmoja
ana mpenzi, akimshawishi mpenzi wake kuipigia CCM tutakuwa
na kura million 16, ambapo tutaweza kumshinda mtu
yoyote……"Ameongeza kuwa
"CCM ni chama cha kuongoza dola, siyo chama cha michezo
wala muziki, mambo ya muziki Kapten Komba anatosha, yupo na
Diamond pia, wanatosha hao, lakini sisi tuhakikishe CCM
inaendelea kuogoza dola"



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment