SITTA AMEPUNGUKIWA SIFA SITA ZA UONGOZI
Na Ananilea Nkya
Watanzania tuna bahati kubwa maana kwa kupitia Bunge Maalum la Katiba angalao tumeweza kufahamu vema tabia ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samweli Sitta. Katika kutekeleza majukumu yake kwenye Bunge hilo Sitta amejibainisha wazi kuwa anapungukiwa sifa SITA alizotakiwa kuwa nazo kiongozi yeyote katika nchi yetu ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Sitta amepungukiwa sifa sita zifuatazo.
(1) Uwezeshaji wa maridhiano
Samweli Sitta ametudhihirishia kwamba hana ujuzi wala dhamira ya kujenga maridhiano pale watu wanapotofautiana. Tumeona wazi kuwa ameshindwa kujenga maridhiano miongoni wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kama alivyofanya Jaji Joseph Sinde Warioba kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Hii ni ishara kwamba Sitta akipewa uongozi wa nchi ataipasua nchi vipande vipande hata kama angeweza kuepuka kwa kujifunza kutoka kwa kiongozi aliyemtangulia. Kwa mfano angeweza kujifunza kutoka kwa kiongozi wetu mahiri na mzalendo wa ukweli, Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye aliweza kujenga maridhiano miongozi wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Hakuna ubishi kwamba wajumbe wa Tume ya Warioba waliingia kwenye tume hiyo wakiwa vipande vipande maana walikuwa na itikadi tofauti za kisiasa, imani tofauti za dini na hata viwango tofauti vya uelewa wa masuala yanayohusu nchi yetu. Lakini wote waliweza kufanya kazi kubwa tena kwa wakati na iliyopokelewa kwa kishindo cha furaha na umma wa Watanzania. Tume iliweza kufanya kazi hiyo kwa sababu bila shaka Mwenyekiti wake hakuwa mbabe. Akijinyenyekeza akamsikiliza kila mjumbe na kujifunza kutoka kwao na hivyo akafanikiwa kujenga muafaka na ndipo tume ikaweza kujinyenyekeza kwa wananchi ili kusikiliza wananchi wanataka nchi yao iendeshwe vipi. Baada ya kukusanya maoni tume iliweza kuyachakata na kuandika Rasimu kwa maridhiano tena bila kupiga kura. Hivyo, tume iliweza kutoa mfano wa kuigwa kwa umma kwamba MARIDHIANO yanawezekana na yanaweza kujengwa katika kila hatua ya mchakato wa kuandika Katiba Mpya.
Lakini baada ya Rasimu kufikishwa katika Bunge Maalum la Katiba na Samweli Sitta kukabidhiwa kazi ya kuongoza Bunge hilo kuijadili na kuipitisha Rasimu hiyo, badala ya kuhakikisha kuna MARIDHIANO baina ya wajumbe yanakuwepo, tumeshuhudia akikumbatia ushabiki wa kivyama, ubabe na unafiki na mwishowe baadhi ya wajumbe wamesusia mchakato na wamekataa kurejea Bungeni. Tena anajinasibu kwamba Katiba itaandikwa hata kama baadhi ya wajumbe hawapo Bungeni. Lo! laiti angelijua kwamba kiongozi wa ukweli angeugua moyoni hata kama ni mjumbe mmoja tu ameudhika na kukataa kushiriki kazi hiyo muhimu maana Katiba ni MARIDHIANO au MUAFAKA wa Kitaifa. Laiti pengine hajui kuwa mbabe na mnafiki hawezi kuongoza timu ikafikia maridhiano. Anapaswa kujua kwamba hata mchunga kondoo wa ukweli ikitokea kondoo wake mmoja amebaki porini kitamuuma sana na atarudi porini kumtafuta hata kama kundi la kondoo wengine elfu moja litakuwa limerejea kwenye zizi.
(2) Ujasiri wa kutetea nchi na wananchi
Kupitia kazi muhimu aliyopewa ya kuongoza Bunge Maalum la Katiba tumeshuhudia jinsi anavyoweka mbele maslahi yake binafsi na ya chama chake badala ya maslahi ya wananchi na nchi yetu, TANZANIA. Mfano alivunja kanuni za Bunge Maalum la Katiba na kumpotosha Rais wetu kutoa maoni yake Bungeni badala ya kufanya kazi yake kama mkuu wa nchi ya kufungua Bunge hilo. Hapa Sitta alipaswa kuonyesha ujasiri kwa kumshauri Rais kufanya alichotakiwa kwa wakati husika. Kwa kutokuwa na ujasiri wa kumshauri Rais kwa upendo na ukweli ameweka wazi kwamba hana chembe ya ujasiri wa kutetea wananchi na nchi yetu. Amedhihirisha kwamba yeye anaweka mbele zaidi maslahi yake binafsi na dirisha lake analopitia kutafuta uongozi (chama chake cha siasa) naanasahau kwamba Tanzania ni kiubwa kuliko sisi sote.
(3) Kulinda maadili na utamaduni wa Mtanzania
Kwa kipindi chote alichoongoza Bunge Maalum la Katiba tumeshuhudia jinsi alivyokaa kimya huku baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakirushiana matusi ya nguoni. Aidha alikaa kimya pia hata pale baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo walipomtukana, kumbeza na kumdhihaki Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba. Watu makini wanaamini kwamba waliomtukana na kumbeza Jaji Warioba waliwabeza na kuwatukana pia Watanzania wote, Tanzania na Rais wetu aliyeiteua tume hiyo kufanya kazi. Bunge Maalum la Katiba limeacha sifa mbaya sana kwa jamii kuwa viongozi wanawake na wanaume wanaweza kusimama hadharani na kuporomosha matusi ya nguoni. Lakini ni wazi kuwa kama Sitta angekuwa ni mtu anayejali na kuthamini maadili ya taifa letu, angalao angekemea wajumbe waliokuwa wanaporomosha matusi na hata ikibidi kuwachukulia hatua za kisheria.
4) Kuheshimu uhuru wa kujieleza
Tumeshuhudia Samweli Sitta akivinyooshea kidole vyombo vya habari hasa televisheni na redio za kitaifa kwa kutangaza midahalo kuhusu Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya. Alijidhihirisha zaidi hasa pale Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipotokeza hadharani kusahihisha upotoshaji mkubwa uliokuwa unafanywa kimkakati na wahafidhina wa mabadiliko kuhusu Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya. Mtu huyu akipewa uongozi wa nchi siyo tu kwa kukosa uvumilivu katika kukuza demokrasia, ataweza kuvifungia vyombo vya habari ambavyo vitakuwa vinakosoa uwajibikaji wa serikali, bali pia hata kufuta usajili wa mashirika ya kijamii yatakayokosoa utendaji wa viongozi wa nchi na pengine hata vyama vya siasa vya upinzani. Kiongozi wa namna hii ni mtu hatari kwa amani na maendeleo ya nchi yetu.
(5) Kukubali mabadiliko.
Mtu yeyote ambaye anaogopa mabadiliko chanya ni mtu hatari maana bila mabadiliko ya kimfumo na kifikra nchi yetu haiwezi kupata maendeleo ya kweli kwa zama hizi mpya. Rasimu ya Pili ya Madadiliko ya Katiba kwa mujibu wa Jaji Warioba ikipitishwa italeta mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiuongozi na hivyo maendeleo makubwa nchini. Lakini kwa jinsi Sitta alivyokimbilia kubadilisha kanuni za Bunge Maalum la Katiba katika awamu hii ya pili inadhihirisha wazi kuwa amedhamiria kabisa kukwamisha kwa makusudi mabadiliko chanya katika nchi yetu ambayo yangeletwa na Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi. Hii inadhihirisha kwamba Sitta anakumbatia uafidhina na waafidhina wanaodhani kuwa wao ni wakubwa kuliko nchi yetu.
(6) Hana huruma kwa wananchi
Sitta anajuwa wazi kwamba Katiba Mpya itakayokubalika na kuheshimiwa na umma mpana wa wananchi haiwezi kupatikana bila maridhiano ya kitaifa. Lakini tumemuona aking'ang'ania Bunge Maalum la Katiba liendelee hata pale wajumbe kadhaa wa Bunge hilo akiwepo Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alipoinuka kwa ujasiri akamshauri kwamba tathmini ifanyike kwanza kuona kama theluthi mbili inayotakiwa kupitisha vifungu vya Katiba hiyo inafikiwa. Endapo haifikiwi Bunge lisitishwe maana ni likiendelea ni sawa na kubariki kupoteza mabilioni ya fedha za kodi za wananchi ambao wanakabiliwa na hali duni ya maisha. Yeye Sitta kwa ubabe alishupaa na kusema theluthi inayotakiwa ipo na walioko nje watakuja tu.! Je kama ikibainika theluthi hiyo haipo na wasiokuwepo wasipokuja atalipa fedha za umma ambazo kila mjumbe wa Bunge hilo Maalum la Katiba anayehudhuria kikao cha sasa atakuwa ameweka mfukoni mwake zaidi ya shilingi milioni 25 ili hali wananchi wengi wakiwa hawana hata uwezo wa kula milo miwili kwa siku?
Hivyo, sisi wananchi tunapotafakari tunaona kwamba endapo nchi yetu itakuwa imekwama kupata Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba Samweli Sitta ndiye wa kubebeshwa lawama zote .
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
On Monday, August 11, 2014 1:01 PM, Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com> wrote:
Ama kweli, ukistaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni! Kama unadhani vigogo wa EPA ni mafisadi peke yao, basi ulikuwa hujamfahamu Spika wa Bunge SAMUEL JOHN TEGEZA SITTA ! Ukimsikiliza anapoongea unaweza kuamini kwamba kiongozi huyo wa Bunge ni msafi kutokana na umahiri wake wa kujivalisha sifa kemkem – Mr Misifa. Unakumbuka hivi karibuni alivyomtukana Naibu Spika eti hawezi kusimamia mambo nyeti mpaka awepo yeye mwenye Bunge? ! Kisa nini? Kupenda sifa na kumdhalilisha mwenzake mbele ya umma, halafu bado anaendelea kuliita Bunge eti ni chombo cha kidemokrasia!
Tumebaini kwamba Sitta amekuwa akijimiminia sifa nyingi ili kulinda ufisadi anaoufanya usigundulike katika jamii yetu. Ngoja nikupe tone tu la madhambi yake kwa umma ili uone ni hatua gani utachukua, na ili na yeye ajipime kwa nafasi yake. Angalia uchafu huu:-
- Anatumia vibaya fedha za umma. Amekuwa akitumia msaidizi wake kuchota mapesa kwa kisingizio kuwa ni masurufu ya safari za ndani na nje ya nchi. Kila safari ya siku moja ndani ya nchi huchukua shilingi Milioni tano (5,000,000/=), na kila safari ya siku moja nje ya nchi huchukua shilingi Milioni Kumi na Tano (15,000,0000/=). Ameshindwa kufanya marejesho ya masurufu (imprest) hayo, licha ya kupeleka risiti kadhaa za kughushi/za uongo kwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Bunge. Mpaka sasa anadaiwa jumla ya shilingi Milioni sitini (60,000,000/=) za masurufu.
- SITTA hupeleka risiti za uongo kwa Mhasibu Mkuu, zikionesha madai kutoka Oysterbay Pharmacy ya Shilingi Milioni Mbili ( 2,000,000/= ) aliyotumia kwa tiba kila wiki.
- Amekuwa akilazimisha hawara yake wa Hospitali ya Aga Khan naye alipwe posho kama wabunge anapokwenda naye Dodoma. Kwa mfano, hawara huyo alilipwa 'per diem' kuanzia tarehe 13/12/2007 hadi tarehe 31/01/2008 ( Siku 50). Huo ni Ufisadi mkubwa!
- Anaye kimada wake mwingine anayekwenda kwa jina la ASIA ambaye anaishi nyumba Na. 111 karibu na Mahakama ya Ardhi Upanga na amezaa naye. Huko mtaani kwao kimada huyo hujiita mama SITTA, na ni dada yake aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa iliyokuwa Tume ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC). Mwanamke huyo muda wote hutumia gari la Ofisi ya Bunge STK 232 Toyota RAV 4.
- Pia anaye kimada mwingine (jina limehifadhiwa) ambaye anaishi kinondoni ( Livingstone), mtaa wa Honolulu katika nyumba ya kupanga inayomilikiwa na dada yake Kawawa. Nyumba hiyo inatazamana na Nyumba Na. KH.MK/No. 337 katika mtaa huo huo. Kimada huyo hutumia gari ya kiofisi ya Spika mwenyewe STK 3002.
- Vimada wote hao hupata huduma za maji na umeme kwa gharama za Ofisi ya Bunge. Kuna kipindi mke halali wa Spika, aliwahi kulalamikia hali hiyo. Kuna siku maji yalikatika nyumbani, mke wa Spika akaomba apelekewe ' bowser' la maji na Ofisi ya Bunge. Ohooo! Watekelezaji wakapeleka maji kimakosa kwa kimada. Mama Sitta akashtukia dili.
- Kuna taarifa kwamba mnamo Mwezi Oktoba 2007, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iligundua mapungufu makubwa katika matumizi ya fedha yaliyofanywa na Spika SITTA. nimedokezwa kuwa Spika aliwanyamazisha wajumbe wa kamati hiyo, ambapo aliwatishia kutowapatia posho na safari za nje kama wangeyafumua mapungufu yake hadharani! Hapo inaonesha kuwa wajumbe hao walipewa rushwa!!
- Kama JK anataka viongozi wa kisiasa na wa serikali watenganishe biashara na uongozi wa ku – 'sacrifice' kimojawapo, hilo litakuwa gumu kwa sababu Sitta alipokuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo cha cha Uwekezaji nchini (TIC) alitumia nafasi hiyo kuingia ubia na wafanyabiashara wengi wa Kigeni. Je, Wizara ya Maliasili na Utalii inatambua kuwa Spika ana hisa kwenye kampuni moja ya Kichina inayosafirisha nagogo licha ya marufuku yaliyowekwa?!
On Sunday, August 10, 2014 7:03:29 PM UTC+3, Abdalah Hamis wrote:
SITTA AMEPUNGUKIWA SIFA SITA ZA UONGOZIWatanzania tuna bahati kubwa maana kwa kupitia Bunge Maalum la Katiba angalao tumeweza kufahamu vema tabia ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samweli Sitta. Katika kutekeleza majukumu yake kwenye Bunge hilo Sitta amejibainisha wazi kuwa anapungukiwa sifa SITA alizotakiwa kuwa nazo kiongozi yeyote katika nchi yetu ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Sitta amepungukiwa sifa sita zifuatazo.(1) Uwezeshaji wa maridhianoSamweli Sitta ametudhihirishia kwamba hana ujuzi wala dhamira ya kujenga maridhiano pale watu wanapotofautiana. Tumeona wazi kuwa ameshindwa kujenga maridhiano miongoni wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kama alivyofanya Jaji Joseph Sinde Warioba kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Hii ni ishara kwamba Sitta akipewa uongozi wa nchi ataipasua nchi vipande vipande hata kama angeweza kuepuka kwa kujifunza kutoka kwa kiongozi aliyemtangulia. Kwa mfano angeweza kujifunza kutoka kwa kiongozi wetu mahiri na mzalendo wa ukweli, Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye aliweza kujenga maridhiano miongozi wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Hakuna ubishi kwamba wajumbe wa Tume ya Warioba waliingia kwenye tume hiyo wakiwa vipande vipande maana walikuwa na itikadi tofauti za kisiasa, imani tofauti za dini na hata viwango tofauti vya uelewa wa masuala yanayohusu nchi yetu. Lakini wote waliweza kufanya kazi kubwa tena kwa wakati na iliyopokelewa kwa kishindo cha furaha na umma wa Watanzania. Tume iliweza kufanya kazi hiyo kwa sababu bila shaka Mwenyekiti wake hakuwa mbabe. Akijinyenyekeza akamsikiliza kila mjumbe na kujifunza kutoka kwao na hivyo akafanikiwa kujenga muafaka na ndipo tume ikaweza kujinyenyekeza kwa wananchi ili kusikiliza wananchi wanataka nchi yao iendeshwe vipi. Baada ya kukusanya maoni tume iliweza kuyachakata na kuandika Rasimu kwa maridhiano tena bila kupiga kura. Hivyo, tume iliweza kutoa mfano wa kuigwa kwa umma kwamba MARIDHIANO yanawezekana na yanaweza kujengwa katika kila hatua ya mchakato wa kuandika Katiba Mpya.Lakini baada ya Rasimu kufikishwa katika Bunge Maalum la Katiba na Samweli Sitta kukabidhiwa kazi ya kuongoza Bunge hilo kuijadili na kuipitisha Rasimu hiyo, badala ya kuhakikisha kuna MARIDHIANO baina ya wajumbe yanakuwepo, tumeshuhudia akikumbatia ushabiki wa kivyama, ubabe na unafiki na mwishowe baadhi ya wajumbe wamesusia mchakato na wamekataa kurejea Bungeni. Tena anajinasibu kwamba Katiba itaandikwa hata kama baadhi ya wajumbe hawapo Bungeni. Lo! laiti angelijua kwamba kiongozi wa ukweli angeugua moyoni hata kama ni mjumbe mmoja tu ameudhika na kukataa kushiriki kazi hiyo muhimu maana Katiba ni MARIDHIANO au MUAFAKA wa Kitaifa. Laiti pengine hajui kuwa mbabe na mnafiki hawezi kuongoza timu ikafikia maridhiano. Anapaswa kujua kwamba hata mchunga kondoo wa ukweli ikitokea kondoo wake mmoja amebaki porini kitamuuma sana na atarudi porini kumtafuta hata kama kundi la kondoo wengine elfu moja litakuwa limerejea kwenye zizi.(2) Ujasiri wa kutetea nchi na wananchiKupitia kazi muhimu aliyopewa ya kuongoza Bunge Maalum la Katiba tumeshuhudia jinsi anavyoweka mbele maslahi yake binafsi na ya chama chake badala ya maslahi ya wananchi na nchi yetu, TANZANIA. Mfano alivunja kanuni za Bunge Maalum la Katiba na kumpotosha Rais wetu kutoa maoni yake Bungeni badala ya kufanya kazi yake kama mkuu wa nchi ya kufungua Bunge hilo. Hapa Sitta alipaswa kuonyesha ujasiri kwa kumshauri Rais kufanya alichotakiwa kwa wakati husika. Kwa kutokuwa na ujasiri wa kumshauri Rais kwa upendo na ukweli ameweka wazi kwamba hana chembe ya ujasiri wa kutetea wananchi na nchi yetu. Amedhihirisha kwamba yeye anaweka mbele zaidi maslahi yake binafsi na dirisha lake analopitia kutafuta uongozi (chama chake cha siasa) naanasahau kwamba Tanzania ni kiubwa kuliko sisi sote.(3) Kulinda maadili na utamaduni wa MtanzaniaKwa kipindi chote alichoongoza Bunge Maalum la Katiba tumeshuhudia jinsi alivyokaa kimya huku baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakirushiana matusi ya nguoni. Aidha alikaa kimya pia hata pale baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo walipomtukana, kumbeza na kumdhihaki Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba. Watu makini wanaamini kwamba waliomtukana na kumbeza Jaji Warioba waliwabeza na kuwatukana pia Watanzania wote, Tanzania na Rais wetu aliyeiteua tume hiyo kufanya kazi. Bunge Maalum la Katiba limeacha sifa mbaya sana kwa jamii kuwa viongozi wanawake na wanaume wanaweza kusimama hadharani na kuporomosha matusi ya nguoni. Lakini ni wazi kuwa kama Sitta angekuwa ni mtu anayejali na kuthamini maadili ya taifa letu, angalao angekemea wajumbe waliokuwa wanaporomosha matusi na hata ikibidi kuwachukulia hatua za kisheria.4) Kuheshimu uhuru wa kujielezaTumeshuhudia Samweli Sitta akivinyooshea kidole vyombo vya habari hasa televisheni na redio za kitaifa kwa kutangaza midahalo kuhusu Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya. Alijidhihirisha zaidi hasa pale Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipotokeza hadharani kusahihisha upotoshaji mkubwa uliokuwa unafanywa kimkakati na wahafidhina wa mabadiliko kuhusu Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya. Mtu huyu akipewa uongozi wa nchi siyo tu kwa kukosa uvumilivu katika kukuza demokrasia, ataweza kuvifungia vyombo vya habari ambavyo vitakuwa vinakosoa uwajibikaji wa serikali, bali pia hata kufuta usajili wa mashirika ya kijamii yatakayokosoa utendaji wa viongozi wa nchi na pengine hata vyama vya siasa vya upinzani. Kiongozi wa namna hii ni mtu hatari kwa amani na maendeleo ya nchi yetu.(5) Kukubali mabadiliko.Mtu yeyote ambaye anaogopa mabadiliko chanya ni mtu hatari maana bila mabadiliko ya kimfumo na kifikra nchi yetu haiwezi kupata maendeleo ya kweli kwa zama hizi mpya. Rasimu ya Pili ya Madadiliko ya Katiba kwa mujibu wa Jaji Warioba ikipitishwa italeta mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiuongozi na hivyo maendeleo makubwa nchini. Lakini kwa jinsi Sitta alivyokimbilia kubadilisha kanuni za Bunge Maalum la Katiba katika awamu hii ya pili inadhihirisha wazi kuwa amedhamiria kabisa kukwamisha kwa makusudi mabadiliko chanya katika nchi yetu ambayo yangeletwa na Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi. Hii inadhihirisha kwamba Sitta anakumbatia uafidhina na waafidhina wanaodhani kuwa wao ni wakubwa kuliko nchi yetu.(6) Hana huruma kwa wananchiSitta anajuwa wazi kwamba Katiba Mpya itakayokubalika na kuheshimiwa na umma mpana wa wananchi haiwezi kupatikana bila maridhiano ya kitaifa. Lakini tumemuona aking'ang'ania Bunge Maalum la Katiba liendelee hata pale wajumbe kadhaa wa Bunge hilo akiwepo Naibu Waziri wa Fedha Mwingulu Mchemba alipoinuka kwa ujasiri akamshauri kwamba tathmini ifanyike kwanza kuona kama theluthi mbili inayotakiwa kupitisha vifungu vya Katiba hiyo inafikiwa. Endapo haifikiwi Bunge lisitishwe maana ni likiendelea ni sawa na kubariki kupoteza mabilioni ya fedha za kodi za wananchi ambao wanakabiliwa na hali duni ya maisha. Yeye Sitta kwa ubabe alishupaa na kusema theluthi inayotakiwa ipo na walioko nje watakuja tu.! Je kama ikibainika theluthi hiyo haipo na wasiokuwepo wasipokuja atalipa fedha za umma ambazo kila mjumbe wa Bunge hilo Maalum la Katiba anayehudhuria kikao cha sasa atakuwa ameweka mfukoni mwake zaidi ya shilingi milioni 25 ili hali wananchi wengi wakiwa hawana hata uwezo wa kula milo miwili kwa siku?Hivyo, sisi wananchi tunapotafakari tunaona kwamba endapo nchi yetu itakuwa imekwama kupata Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba Samweli Sitta ndiye wa kubebeshwa lawama zote .
On Saturday, August 9, 2014 11:40:01 AM UTC+3, Method Francis Ngonge wrote:Du! kwa sifa hizo ina maana sitta ni Majanga?. Binafsi namuhurumia sana mzee huyu jinsi wenziye walivyomfanya mbuzi wa kafara kwa kumpendekeza kuwa mwenyekiti wa bunge maalumu la katiba lenye mazabezabe na mangumashi tupu.
Hivyo watu watakuwa na reference ya kushindwa kwake kusimamia mambo ya msingi hivi karibuni. Maskini Sitta kweli zigo zito mtwike mnyamwezi lakini hili ni zito kupindukia sijui kama safari yake ya kuelekea ikulu itafika mwisho
2014-08-08 16:43 GMT+03:00 Telesphor Magobe <tma...@gmail.com>:Pia kama ilivyo kwa mgema, aliposifiwa ametia maji!2014-08-08 14:40 GMT+03:00 'Eberi Manya' via Wanabidii <wana...@googlegroups.com>:
Huyo Sitta ni layman. Hana jipya..
'Godfrey Ngupula' via Wanabidii <wana...@googlegroups.com> wrote:
>Pia, anajali sana maslahi binasi..
>
>
>
>On Friday, 8 August 2014, 11:20, Jovias Mwesiga <ngo...@gmail.com> wrote:
>
>
>
>Weka kabisa kuwa alichapwa kwa kuendesha huo mgomo lol
>On Aug 8, 2014 3:08 AM, "Emma Kaaya" <emma...@gmail.com> wrote:
>
>
>>
>>- Mwanafunzi
>wa Kwanza kuongoza maandamano ya chuo kikuu cha dar es salaam mpaka ikulu mwaka
>1966.
>>- Amekua
>kiongozi kuanzia mwaka 1970, kwenye nafasi za waziri , mbunge na mkurugenzi .
>>- Akiwa
>spika wa bunge alijenga nyumba ya mil 500.
>>- Mkewe
>Mhe Magret sitta aliwahi kukamatwa na tukukuru kwa kutoa rushwa ili ashinde
>ubunge .
>>- Toka
>amekuwa waziri wa afrika mashariki nchi imetengwa kwenye miradi mingi ya
>kimaendeleo inayofanywa nan chi jirani .
>>- Hata
>mafanikio yoyote ya kujivunia kitaaluma ya sheria ambayo ndio aliyosomea chuoni
>.
>>- Hajawahi
>kuandika wala kuchapa kitabu chochote .
>>- Hashiriki
>michezo wala shuguli za kijamii zaidi ya dini yake ya kilutheri .
>>- Ana
>umri wa miaka zaidi ya 65 , umri wa kustaafu kazi za umma ni 60 .
>--
>>Send Emails to wana...@googlegroups.com
>>
>>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>>wanabidii+...@googlegroups. com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>>
>>Disclaimer:
>>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>---
>>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com .
>>For more options, visit https://groups.google.com/d/ optout.
>>
>--
>Send Emails to wana...@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+...@googlegroups. com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com .
>For more options, visit https://groups.google.com/d/ optout.
>
>--
>Send Emails to wana...@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+...@googlegroups. com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com .
>For more options, visit https://groups.google.com/d/ optout.
--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/ optout.
--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/ optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment