Thursday, 14 August 2014

Re: [wanabidii] Taarifa ya UKAWA kuhusu Katiba Mpya na yanayoendelea BMK

wATANZANIA TUWE MAKINI. Tutawaongoza ni UKAWA kuwaongoza watanzania. Kila anayefuatilia mambo ataona kuwa MUSA kapotelea winguni. Hatujui kilichompata. Nchi haionekani kuwa na kiongozi katika hili. hatuhitaji kuuliza maswali kana kwamba huu ni ushabiki wa mpira au tunagombea udiwani (kwa maana kuwa tume imechagua wagombea atakayepita yeyote anatosha)
Tunajadili katiba kama ambavyo 1977 tulijadili kivyake iliyokuwepo.
Tunahitaji kufanya maamuzi sasa la sivyo tunaiandaa Spmalia ya myaka ijayo.
Huenda wenye kuona tukiungana na UKAWA na majukwaa mengine tunaweza kupata ufumbuzi wa amani. Tupipuuza hatua hii tujue kuwa Muungano umekwenda na Tanganyika inaingia tena bila kupitia Katiba maana haitakuwepo.
Huwezi kuendelea kuandaa katiba ya serikali mbili bila kujadili Katiba ya Zanzibar. Huwezi kuijaadili katiba ya Zanzibar maana wazanzibari walitunga katiba inazuia hilo. Huwezi kuendelea kuwabufruza watanganyika kama majuha kwa muda mrefu. Tunafikiri Rais kikwete atachukua maamuzi magumu. Tunafikiri viongozi wa CCM watasema 'AHAA'. Bila hilo hali ngiumu huko tuendako.

nawakilisha
--------------------------------------------
On Thu, 8/14/14, mngonge franco <mngonge@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Taarifa ya UKAWA kuhusu Katiba Mpya na yanayoendelea BMK
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, August 14, 2014, 4:01 AM

No research, no right
to speak. Wasemaji wa vyombo hivyo ndo wananchi? Ni viongozi
vya vyombo hivyo walioamua kutoa maoni yao, na wala siyo
wanachama au waumini kwa ujumla wao



2014-08-14 11:19
GMT+03:00 Joseph Ludovick <josephludovick@gmail.com>:

..."IWAPO
ATASHINDWA.......TUTAWAONGOZA.." inachukua muda gani
kujua kuwa ameshindwa? na je hii tutawaongoza akina nani?
maana tujuavyo, baraza la maaskofu katoliki TEC, CCT na
Wapentekoste, pamoja na BAKWATA wamewataka UKAWA warudi
bungeni. WASOMI pale chuo kikuu waliwataka warudi bungeni.
na wana CCM wanaunga mkono warudi bungeni. hawa wote kwa
macho ya UKAWA siyo WANANCHI?




2014-08-14 1:08
GMT-07:00 mngonge franco <mngonge@gmail.com>:


Nimependa maneno
"UKAWA
tutawaongoza Watanzania kupaza sauti zaidi kupinga najisi
inayotiwa kwenye maoni yao" Ni kweli hawa jamaa
wasioambilika wanajaribu kuyatia najisi maoni ya
wananchi





2014-08-14 10:50
GMT+03:00 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>:



MCHAKATO WA
KATIBA MPYA NA YANAYOENDELEA BUNGE MAALUM LA KATIBA



Ndugu wanahabari,



Sote tunaelewa kuwa kwa matakwa ya CCM, Bunge Maalum la
Katiba (BMK) limeendelea kufanya vikao vyake mjini Dodoma
kuanzia Agosti 5 mwaka huu, kinyume kabisa na matarajio ya
Watanzania, ambao kupitia fursa mbalimbali wamepaza sauti
zao wakisisitiza maridhiano na mwafaka wa kitaifa
kutangulizwa mbele badala ya maslahi ya
watawala.



Tukiwa viongozi wa kisiasa ambao ni sehemu ya uongozi ndani
ya jamii, wenye wajibu wa kuwa na maono chanya na muhimu kwa
taifa letu, tumeendelea kufuatilia kwa karibu namna mchakato
wa Katiba Mpya unavyoendelea kunajisiwa kupitia vikao hivyo
vya BMK linaloendelea mjini Dodoma, likitumia rasilimali za
taifa, zikiwemo kodi za Watanzania wanyonge, kujadili vitu
visivyotokana na wananchi.




Mtu yeyote makini ataweza kubaini kuwa kwa namna mchakato wa
Katiba Mpya unavyopelekwa auunavyokwenda
kwa sasa ni matokeo ya kukosekana kwa uongozi wa kisiasa kwa
Chama kinachoongoza Serikali, CCM.




Kuna ombwe kubwa la uongozi wa kisiasa katika jambo hili. Ni
kama vile mchakato unajiendea tu wenyewe bila mwongozo
wowote kutoka kwa watu walioko madarakani ambao wananchi
walitarajia wangetumia mamlaka yao ya dhamana ya uongozi ili
taifa lipite salama katika wakati huu mgumu na tupate Katiba
Mpya na bora.




Vipo viashiria vingi tu vinavyoweka wazi hali hiyo ya ombwe
la uongozi wa kisiasa katika mchakato huu wa kisiasa, ikiwa
ni pamoja na kauli kinzani za viongozi wa Serikali na CCM
yenyewe. 
Wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza kama vile
kunahitajika mazungumzo zaidi na kwamba suala la muundo wa
serikali lilipaswa kupigiwa kura kabla, Mwenyekiti wa BMK
anaendelea kuongoza bunge kama vile mchakato ni mali binafsi
ya CCM na walioko madarakani.




Wakati baadhi ya viongozi wa Serikali ya CCM wakitoa kauli
za kuhitaji kuwa makini na taratibu za kuendesha mchakato
huu chama chao kinatoa kauli za kuzidi kuharamisha na kutia
najisi mchakato mzima. Mchakato unakwama, nchi inayumba,
Watanzania wako katika sintofahamu kwa sababu tu tumekosa
uongozi wa kisiasa katika jambo hili.




Kiashiria kingine cha pengo hilo la uongozi wa kisiasa
ambacho kwa kweli kwetu sisi kimetusikitisha zaidi kitendo
cha Rais Jakaya Kikwete kuendelea na 'hamsini zake' kama
vile nchi haina tatizo lolote. 

Yaani wakati nchi na wananchi wako katika sintofahamu ya
hatma ya Katiba Mpya itakayoweka misingi ya wao kujitawala
na kuongozwa watakavyo, makundi mbalimbali yakipaza sauti
zao, mataifa mengine yakituangalia kwa makini na wawekezaji
wa ndani na nje ya nchi wakifuatilia mchakato, Rais Kikwete
anapata muda wa kutembelea ranch ya Rais Mstaafu wa Marekani
George Bush! 




Wakati Rais Kikwete akiendelea kutalii dunia, wenzake wako
mjini Dodoma wakichukua posho kwa kazi ambayo wananchi
hawajui wanaifanya kwa maslahi ya nani!

Kwa ujumla mambo yote yanayoendelea sasa katika mchakato huu
ni matokeo ya ombwe hilo kama tulivyosema. 




Inaonesha kuwa CCM wamelewa madaraka na viongozi wanaona
dhamana ya uongozi iko juu ya wananchi hivyo hawajali
umuhimu na nafasi ya mamlaka ya wananchi katika kuamua
mstakabali wa taifa lao kwa ajili ya kizazi cha sasa na
kuweka msingi wa vizazi vingi vijavyo.



Hivyo leo tungependa kuzungumza tena kuhusu Rasimu ya Katiba
na mchakato wenyewe hapa ulipokwama;

Tunapenda kusema wazi kuwa tumeshangazwa sana na kitendo cha
CCM na Serikali yake kulazimisha kuendelea kwa Bunge Maalum
la Katiba Mpya, tena kwa mtindo ule ule wa kunajisi na
kupuuza maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Pili ya
Katiba Mpya kama yalivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba.




Wamefanya hivyo pasi na kujali kilio cha wananchi
kinachopazwa kutoka kila kona ya nchi, ambapo Watanzania
mmoja mmoja na katika makundi mbalimbali wametaka maoni yao
yazingatiwe kwa kujadiliwa, kuboreshwa na kisha kupitishwa
na Bunge Maalum la Katiba kabla wao hawajayapigia kura ya
maoni kwa ajili ya kuipitisha au kuikataa Rasimu ya Katiba
Mpya.




Wajumbe wanaotokana na CCM pamoja na makada wengine wapatao
166 wa chama hicho ambao waliteuliwa kuingia kwenye bunge
hilo kusimamia maslahi ya CCM kupitia kundi la wajumbe 201,
wameamua bila haya mbele ya umma si tu kupuuza rasimu
iliyotokana na maoni ya wananchi bali sasa wameamua kuingiza
mambo yao waliyodhamiria tangu mwanzo kwa kadri ya maamuzi
na maelekezo ya vikao vya chama hicho vikiongozwa na
Mwenyekiti wao Jakaya Kikwete.




Bila kujali wala kuguswa na miito ya Watanzania mbalimbali
wanaotaka jambo hili liongozwe na maridhiano kwa ajili ya
mwafaka wa kitaifa badala ya kuweka matamanio ya watawala
mbele, CCM na mawakala wao katika mchakato huu wameendelea
pia kufuja na kutumia vibaya fedha za wananchi kupitia Bunge
Maalum la Katiba kwa kujadili na kuingiza vitu visivyokuwemo
au visiyotakiwa kuwa sehemu ya rasimu hii iliyopo sasa.




Hali hiyo imefanyika kwa namna kadhaa ikiwa ni pamoja na
kutofuata sheria inayosimamia mchakato mzima, kubadili
kanuni za uendeshaji wa BMK hasa katika taratibu za kujadili
na kupitisha ibara na kubwa zaidi kuingiza masuala ya
Tanganyika kwenye Rasimu ya Katiba ya Muungano.




Kimsingi masuala wanayoyajadili na kuyachomeka kinyemela
kwenye Rasimu ya Pili ya Warioba, mathalan masuala ya Ardhi,
Elimu, Maji, Kilimo, Uvuvi, Mifugo, Serikali za Mitaa nk ni
masuala yanayopaswa kuandikwa kwa kina ndani ya Katiba ya
Tanganyika na siyo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.




Ni vyema kukumbuka kuwa Zanzibar walijadili wenyewe mambo
Yao ya Ndani na kutengeneza Katiba yao na hatuoni mantiki ya
kuruhusu Wajumbe toka Zanzibar kujadili na kuamua mambo ya
Tanganyika. BMK haina Sifa ya kujadili yasiyo ya Muungano.




Hivyo tofauti na wanavyotaka kujionesha katika jamii, CCM
kupitia BMK wameamua kupindua kabisa rasimu nzima na kuweka
maazimio ya vikao vyao kuwa ndiyo Katiba ya Tanzania. Jambo
hili haliwezi kukubalika.

Kutokana na uchakachuaji huo wa Katiba Mpya unaoendelea
kufanywa na CCM kupitia BMK, UKAWA tumefikia maamuzi
yafuatayo;



Tunamtaka Rais
Jakaya Kikwete asitishe shughuli za BMK mara moja
lisiendelee kuvuruga na kuharibu mchakato wa Katiba Mpya na
kuiweka nchi katika sintofahamu juu ya jambo hili
nyeti;


Tunamtaka Rais
Kikwete asitishe BMK ili lisiendelee kufuja fedha za
Watanzania maskini wanaopigania Katiba Mpya iwapatie
matumaini ya kuongozwa na kujitawala
wanavyotaka.


Tunamtaka
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya
ukaguzi maalum kwenye matumizi ya fedha za BMK ambayo
kuanzia Bunge la Bajeti lililopita tumebainisha wazi kuwa
yana uvundo mkubwa wa ufisadi na hayana maelezo
sahihi.


Iwapo Rais
Kikwete atashindwa kutumia mamlaka yake kusitisha BMK na
hivyo likaendelea kinyume cha matakwa na maslahi ya wananchi
kama lilivyofanya awali na linavyofanya sasa,


UKAWA
tutawaongoza Watanzania kupaza sauti zaidi kupinga najisi
inayotiwa kwenye maoni yao, kupitia maandamano na mikutano
ya hadhara nchi nzima.



Asanteni kwa kutusikiliza.

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti CUF

Freeman Aikaeli Mbowe
Mwenyekiti CHADEMA

James Francis Mbatia



Mwenyekiti NCCR Mageuzi

Wilbrod Peter Slaa
Kny Makatibu Wakuu, UKAWA.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.




---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment