Fakhi-Ninachangia kwa kupenda historia ya wapare na kusema-Msome Prof Kimambo pia. Ameandika sana sana kuhusu Upare na Wapare, East Africana UDSM kuna archival information mpaka maktaba ya mambo ya kale pia. Soma kitabu cha mzungu mmoja-Lute Lwedi Lute Luvivi kimeandikwa na wamisionary. Ama katika kabila ambalo linatakiwa kuheshimiwa katika utunzaji mazingira tanzania ni hili na Baba wa taifa alipofika huko na kujifunza mambo yao mfumo wa Ujamaa ni 'PARE' system mfumo wa Uongozi wa kimila wa 'Ufumwa-wafumwa wa Upare -kuanzia juu ckwa Rais au chifu hazi ten-cell level na alituambia yeye na Mzee Mwinyi kuwa-Nendeni Upare mkajifunze. waliingia toka taita kupitia sambaa na Mkomazi kutokana na ukame (climate Change) ambao ndio ulioleta makabila mengine TZ mfano wasukuma kutuka mbali sana wakisaka makazi kukimbia ukame (West Africa-Chad to Bongoland)'. wakaona maji yanatililika kuingia mbuga ta Mkomazi-wakayafuatilia na kufika milima ya S.Pare wakaanzisha irrigation system ambapo chief anatawala mfumo huo toka juu hadi chini unapoingia kwenda kwingine na kamati za mazingira, canal caretakers wa main and tributaries na mpaka leo mfumo upo ila unaingiliwa na siasa na utawala wa sasa lakini kamati ya mila bado powerful. national service-Mshitu e-nyumbae (makambi ya mafunzo baada ya jando) ni full mafunzo ya kila aina sio tu mambo ya kifamilia bali mazingira, kilimo, mapigano, kutengeneza silaha, mizinga ya nyuki, ufugaji-full degree multi-sectoral. Vicoba na saccos na kusaidiana kivikundi mama akizaa mtaa hadi mtaa/sub-area kupeleka zawadi; ulinzi wa milima kwa kilimo cha terracing; barabara well constructed milimani; ulinzi wa mabwawa ya maji (Ndiwa/Ndiva) na kutenganisha ya kunywa binadamu, wanyama na njia ya kwenda mashambani, timing ya maji na sharing system kutoka juu hadi kuyarudisha mtoni yaende baharini ni utaalamu na ufuatiliaji masaa 24. Kuingiza wageni katika kamati za mila na kuwahoji kupata kujua kwao wanatatuaje suala hili na lile na unakuta kabila hizo zinapewa muda maalum wa kukaa kikao cha mila kisha kusepa na sheria ndogo ndogo na adhabu kutolewa-kama kulimi sustainably na kuingiza mfugo hata shambani kwako-inakula kwako watakupanguza mfugo mnene na utaitwa kikao cha mila kuonywa. Management ya common property resource ni kiboko na individual property budi uzingatie sheria za mila.Sharing poverty-huruhusiwi kuvuna na kuuza mazao pori haya ni ya kuvuna na kuuza watoto, haya akina mama, haya vijana na haya wazee na inaheshimiwa. maeneo ya mizinga ya nyuki na mashamba -no mifugo na kuchunga mifugo kwa vikundi (ndisha) ili kupeana nafasi za mtu kufanya kazi nyingine sio achunge daily. si kabila langu lakini katika makabila nilikowahi kula mihanjo vijijini-ninaliheshimu sana. Tusikae tukasifu baadhi ya makabila na kuyafanya-The best kabila mfano wakati ni kutaka kujilikana ili kupata donor funds tu na kusahau mengine ambayo tuna mengi ya kujifunza kwao (kama walivyofanya wakoloni ili kugeuza kibao na kututawala). Charle Lane aliwatetea na kufuta umbea uliotaka na kudai Mkomazi ni wa Maa groups. Wao Wapare waliwakuta watu waitwao Wagalla (from West Africa) hunters and gatherers na mapicha yao kwenye mapango ya Tussa Hills wamo humo na waliishia in early 1950s lakini familia moja ilikuwepo ambapo baba alikuwa na uwezo wa kuita tembo na wanyama wengine wawatakao wawindaji wa kizungu kwa nyama au pembe zao kisha wakampiga risasi wakamuua na kujifaidia. Ukoo upo Njiro sub-village ya kijiji cha Kisiwani. Akina Thomson na explorers wengine wameandika vema kulikohao ambao wanajifanya kutetea Ilparakuyo Maasai against the Pare kwa manufaa yao binafsi. Ila-wasambaa waliwavamia wapare wakatawala baadhi ya maeneo wakawakamata na kuwauza utumwa. Baadae South pare ikaunganishwa na Mkoa wa Tanga kabla haijarudishwa tena Mkoa wa Kilimanjaro.
Wapo wafugaji wa Ki-pare ambao hawalimi kabisa na wapo agro-pastoralists. wasiolima kwa sasa ni wachache sana wanaishi ukielekea mbuga za Hedaru. Sasa South pare ni Kiama. Mkomazi imekuwa national park, vijiji vinafanywa kuwa Small towns-Township. wakazi wanatakiwa wasiwe na mifugo-miji midogo. Hii inaathiri lishe ya watoto na elimu kwa watoto kwani wafugaji hukaa mbali na mji lakini kila kaya ina 2-5 cows na mbuzi wachache wa mama kukamua maziwa kwa kunywa familia, mtindi kula na ugali na kuuza maziwa hayo kupata senti za matumizi. irrigation farms zitaathirika, lishe itakuwa duni kwa mashamba kuwa housing plots. Ardhi ni ndogo in mid 1920s waliwahamishia Mbeya baadhi yao kupunguza tatizoi la overpopulation milimani kama wachaga walivyohamishiwa pamoja maeneo mengine na Morogoro. Wapare hawato sahau kipigo na vifungo vya Mjerumani kwa wao kukataa kuchukua mawe waliyokuwa wakifanyia terracing ktk mitelemko ktk kilimo ili yakajengewe reli ya Moshi Tanga. Waliona ni destructive bora wafe. Kupunguza uhaba wa ardhi hawakuwa na makabury bali kuweka mafuvu ktk protected clan forest yenye mapango na mafuvu kuwekwa ktk chungu na ukubwa/urembo kuonyesha position yako ktk familia. See attached. Pia, demographic control, iliwafanya kuua watoto waliozaliwa eti katanguliza mguu, kaota meno ya juu etc kumuachilia juu ya mwamba wa mlima akaaungukia chini ya pango (malameni-mafuvu ya vichanga yapo). ukipata mimba kambla ya kuchezwa unafungwa nyama iloyooza na kupitishwa kwenye tundu la ukuta wa nyumba uwende porini harufu itawavuta fisi wakutafune. ukipona kuliwa huko watoto wako ni Vihiria. waarabu wavuna meno ya tembo waliwaokota wakawaoa na kuwazalisha vihiria hao.
Ninawaabudu na kuwapenda Wapare!! Tuombe wenye uwezo kufufua Historical Society-vichapishwe upya vitabu vya zamani vinavyopotea, kutafiti upya makabila ambaye wazee wapo wasimulie na makanisa hayajachoma moto makala za wamisionari. Makusanyo mengi ya maandiko na file za ukoloni ya kuchukuliwa na TNA (Tanzania National Archives) wameyaacha wilayani yanaliwa na mchwa au majumba yameezuka vigae vya mkoloni maandiko yanaoza wilayani.Au maktaba za taifa wanafungulia mabomba ya maji yakikatika keshi wakija chumba kimejaa maji files zinaelea. Swedish people, Reance na Unesco wana interest na kukuza historia-tuwatumie na Idara ya Archeology ya UDSM.
On Saturday, 9 August 2014, 17:03, Fakhi Karume <fkarume@gmail.com> wrote:
Wapare wanaishi katika miteremko ya milima ya Upare Kaskazini, iliyopo Mashariki ya Milima ya Usambaa; na Kusini Mashariki mwa mlima Kilimanjaro. Kwa mujibu wa historia kutoka katika machapisho mbalimbali, lugha inayozungumzwa na watu wa eneo hili, inajulikana kama Chasu. Wenyeji wakaitwa Vaasu, hivyo kabila hilo lilijulikana k ama kabila la Waasu. Historia inaeleza kuwa katika Karne ya 18, Waasu walikuwa wenyeji wa Kenya eneo la Taita na Taveta. Lakini, baada ya kusikia habari za maajabu ya Kilimanjaro, walifanya mikakati ya kuhama ili waishi katika mteremko wa mlima huo. Waasu walipofika karibu na maeneo ya mlima wa ajabu, yaani Kilimanjaro, walielekea sehemu za Kaskazini ili waishi karibu na Kilimanjaro, wakiwa na matumaini makubwa ya kuishi huko. Tofauti na matarajio yao, walikutana na wenyeji wa eneo hilo, Wachaga. Hata hivyo, hawakukata tamaa, waliendelea kuweka mazingira ya kujenga himaya hayo. Wachaga walipoona wanaingiliwa, waliitana na kuanza kuwafukuza huku wakipiga makelele wakisema "wapare… wapare", ikiwa na maana wapige… wapige! Ili kuokoa maisha yao, Waasu walikimbia kuelekea sehemu za mteremko hadi eneo la Mwanga na Same, Kusini mwa mlima Kilimanjaro; ITAENDELEA.....
-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment