Wednesday, 2 July 2014

RE: [wanabidii] Safu ya uongozi chama cha CUF 2014

Chadema wanakabiliwa na tatizo la ukanda,lakin si kweli kama chadema ni wakanda...lakini kisiasa chadema wanatakiwa kufanya jambo katika hili kwa mustakabali mwema wa chama. CUF hakuna atayewalazimisha kufanya jambo katika hili,lakin licha ya sababu za justification kuwepo,CUF watapendeza wakifanya jamba katika hili haswa katika nafasi za juu tatu za uongoz. Ngupula

'Julius' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Mrema,
Haya unayoyasema yana walakini mkubwa.
Sekretariati ya CUF inaundwa na wajumbe kutoka Bara na Znz.

Kwa upande wa Zanzibar asilimia zaidi ya 99 ya wananchi ni waislamu kwa hiyo karibu viongozi wote wa kila chama cha siasa wanaotoka Znz watakuwa waislamu.

Kwa upande wa Bara waislamu na wakristo wana uwiano ambao unaweza kukaribiana(sielewi dini ipi ina wafuasi wengi), na katika sekretariati ya Bara yenye wajumbe takribani watano wawili ni wakristo na watatu ni waislamu.

Kwa hali hiyo mimi sioni tatizo ni nini. Mnapokaa hapa na kudhani kuwa CUF ina dormination kwa waislamu mnahitaji utafiti.

Naweza kukupa mfano mdogo tu, karibu madiwani wote 12 wa CUF walioko Tanga, wote ni waislamu.
Madiwani wote wa CUF walioko Serengeti, Musoma Mjini, Musoma Vijijini na Tarime wote ni wakristo.
Madiwani zaidi ya 9 wa CUF walioko wilaya ya Kwimba karibu wote ni wakristo n.k n.k n.k....
Nani amewakataza wakristo kujiunga CUF??? Mbona wengine wengi tu wako CUF na wanaongoza kwenye halmashauri zao?

Jambo ambalp nakubalina nalo ni mfumo dume, hilo bado linatuathiri, nashukuru kuwa hv ss walau kwa upande wa Bara, hata Naibu Katibu Mkuu ni mwanamke na hata Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu ni mwanamke, hiyo haitoshi - tunapaswa kuongeza juhudi zaidi na kuongeza wanawake wenye uwezo zaidi katika uongozi.

Juzi siku chache kabla ya Mkutano Mkuu wa CUF, mimi na Katibu Mkuu wetu tulipokea wanachama wapya 54 wasomi wa vyuo vikuu katika ukumbi wa Lamada, karibia asilimia 70 walikuwa ni wakristo.

Hii propaganda ya CCM na udini wa kutupia vyama vingine itakwisha tu, tuipe muda, enzi hizi si enzi zile.

Julius Mtatiro,
DSM.

From: 'Ngupula GW' via Wanabidii
Sent: ‎7/‎2/‎2014 18:26
To: Herment Mrema; wanabidii@googlegroups.com
Subject: RE: [wanabidii] Safu ya uongozi chama cha CUF 2014

Bwana Mrema,CUF,ushauri wako hawatautendea kazi na wala chama hicho hakiwezi acha kuwa na mwegemeo wa kidini kisera na kwa jinsi hiyo kamwe haiwezi tokea kikaminika na wananchi na kushika dola ya nchi..ngupula

Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com> wrote:

Safu Mpya ya Kamati ya Utendaji ya Taifa (Sekretarieti) ya CUF ina walakini kwa kiasi fulani.  Ningependa CUF ipanuke zaidi sehemu za Bara lakini ukiona majina ya viongozi ambayo 88% ni wa majina kutoka dini moja ya Kiislamu inatia shaka kidogo. Nilitizamia uongozi uwe ni mchanganyiko wa Kikristo, Dini nyingine na Kiislamu.  Vile vile kina mama ni wachache mno.  Ningeshauri Chama kiangalieo hili kwa siku za usoni.

Ahsante

Herment A. Mrema


Date: Tue, 1 Jul 2014 23:49:50 -0700
From: hamisznz@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Safu ya uongozi chama cha CUF 2014

  • Prof. Ibrahim Lipumba - Mwenyekiti
  • Juma Duni Haji - Makamu Mwenyekiti
  • wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
    For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment