NIMEKUWA NIKIFUATILIA KWA KARIBU SANA SAKATA LA MH. MBUNGE KIJANA MACHACHARI DAVID KAFULIRA NA MH. AG, F. WEREMA. KIMSINGI MIMI NAWALAUMU WOTE KATIKA FIKIRA TOFAUTI. NIANZE KUSEMA NAMLAUMU AG, WEREMA KWA KUMWITA KAFURILA TUMBILI. AWALI AKIWA BUNGENI ALIKUWA AKITOA TU MFANO KUPITIA TUMBILI LAKINI HAKUMTAJA KAFULIRA KUWA NDIYE TUMBILI JAPO INNUENDO ALIMAANISHA HIVYO INGAWA INNUENDO PIA INAHITAJI USHAHIDI KUTHIBITISHA HILO. LAKINI KITENDO CHA MZEE MZIMA KUSHINDWA KUCONTROO HASIRA ZAKE ALIPOITWA NA KAFULIRA KUWA WEWE NI MWIZI TU NAYE AKAMWAMBIA NYAMAZA WEWE TUMBILI ILIKUWA NI USHAHIDI TOSHA ULE MFANO WAKE WA KUMHUSISHA TUMBILI ULIMLENGA MBUNGE HUYO KIJANA. KWAA HILO NAMLAUMU SANA BABA YANGU HUYU NGULI WA SHERIA AMBAYE SI TU NI MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI BALI PIA NI JAJI WA MAHAKAMA KUU, HIVYO ANA WAJIBU WA JUU KABISA WA KUISHAURI SERIKALI KATIKA MAMBO YOTE YA SHERIA NA NDIYE WAKILI NAMBA MOJA KATI YA MAWAKILI WOTE WA TANZANIA AMBAO SASA IDADI YAKE INAKARIBIA ELFU TANO. HIVYO KAMA WAKILI NAMBA MOJA ANAPASHWA KUFUATA MAADILI YA MAWAKILI POPOTE PALE ALIPO BILA KUJALI YUKO BUNGENI, MAHAKAMANI AU KWENYE PUBLIC. KWA HIYO ALIVUNJA MAADILI YA UWAKILI KWA KUMTUKANA MWENZAKE TUMBILI HATA KAMA ALIKUWA AMEKAISIRIKA VIPI NDIYO MAANA AMEKUBALI KUINGIA KWENYE GENGE LA WANASIASA HIVYO ANAPASWA KUWA MVUMILIVU PALE ANAPOSHTUMIWA KWA VYOVYOTE VILE MAANA MKUU NI JALALA. KWA HIYO NI KWELI ALITUMIA LUGHA YA KUUDHI NA NDIYE ALYEANZA KUMWITA MWENZAKE TUMBILI KWA NJIA YA INNUENDO, KWA HIYO KUHUSU MWONGOZO WA SPIKA MAKINDA KWAMBA JAJI WEREMA ALIKUWA SAHIHI KUMWITA KAFULIRA TUMBILI ALIKUWA SAHIHI ETI ALIKUWA PROVOKED SI KWELI NA INAONEKANA DHAHIRI KABISA SPIKA MAKINDA HAJUI MATUMIZI SAHIHI YA PROVOCATION HIVYO ATAFUTE MSAADA ZAIDI KWA LEARNED BROTHERS AND SISTERS NA WASOMI WA KADA NYINGINE WALIO MAKINI WANAOJUA MAANA YA PROVOCATION WAMPE SHULE ILI NEXT TIME AKIOMBWA MWONGOZO KWENYE MASUALA YA KITAALAMU KAMA HAYA AJIBU VIZURI NA KUTOA MWONGOZO WENYE MASHIKO NA SI KAMA MWONGOZO ALIOTOA KATIKA SUALA HILI. LAKINI PAMOJA NA YOTE THE HON. WEREMA,J, NI JUJI AMBAYE NI MTAFSRI WA SHERIA ZILIZOTUNGWA NA BUNGE MAANA HATA AKIACHA UANASHERIA WAKE MKUU ANARUDI KWENYE BENCH, HIVYO TUNATEGEMEA AWE MAKINI SANA MAANA KILA NENO LITOKALO KINYWANI MWA JAJI LINATAKIWA KUWA NA MANTIKI KUBWA SANA KUTOKANA NA FURSA/NAFASI YAKE. MANENO YA MAJAJI NI MANENO YA MAHAKAMA NA MAHAKAMA NDICHO CHOMBO CHA JUU KABISA KATIKA KUTENDA HAKI HAPA NCHINI. SASA KWA MANENO KAMA YA JAJI WEREMA YA KUMWITA MWENZAKE TUMBILI, IKIWA YUKO KWENYE BENCH AKAFIKISHIWA KESI KAMA HIYO ATAIAMUA VIPI WAKATI YEYE MWENYEWE ANAONA NI RAHISI TU KUMWAMBIA MWENZIE TUMBILI NA KWAMBA ATAONDOKA NA KICHWA CHAKE? HILO LA KICHWA CHAKE NITALIJADILI SIKU NYINGINE MAANA NALO LINA TAFSRI KUBWA KISHERIA.
KWA UPANDE WA KAFURILA YEYE ANA MAKOSA MAWILI. LA KWANZA AMEKIUKA KATIBA YA NCHI NA SHERIA YA KANUNI ZA ADHABU SURA YA 16 KAMA ILIVYOFANYIWA MASAHIHISHO MWAKA 2002 (CAP 16 R.E. 2002). HAPA NITAZUNGUMZIA KWA UJUMLA KWAMBA SHERIA HIZO ZOTE ZINASEMA KWA NO PERSON SHALL BE CONDEMNED UNHEARD, AU KWA LUGHA NYINGINE NINASISITIZA KUWA EVERY PERSON IS INNOCENT UNTIL THE CONTRARY IS PROVED. YAANI HAKUNA MTU ATAKAYETIWA HATIANI BILA KUSIKILIZWA AU KILA MTU ANACHUKULIWA NI NI MWEMA MPAKA HAPO ITAKAPOTHIBITSHWA VINGINE. SASA MH. KAFULIRA ALIKOSEA KUMTIA HATIANI ,MH. AG, WEREMA KWA KUMWITA MWIZI BILA KUMPA FURSA YA KUJITETEA NA PILI ALIMHUKUMU BILA KUMCHUKULIA KUWA NI MWEMA MPAKA HAPO ITAKAPOTHIBITISHWA KWAMA SI MWEMA. NA KAZI YA KUSEMA NI MWEMA AU SI MWEMA PIA YA KUMSILIKILIZA ILI IJULIKANE KAMA NI MWEMA AU SI MWEMA NI YA MAHAKAMA KAMA AMBAVYO KATIBA AMBAYO WABUNGE WOTE WAMEAPA KUILINDA INATAMKA KUWA CHOMBO CHA JUU KABISA CHA UTOWAJI HAKI NCHINI NI MAHAKAMA. KWA HIYO BASI HAPA MH. KAFULIRA ALIKOSEA KABISA KUMWITA WEREMA,J, KUWA NI MWIZI PAMOJA NA WENGINE WOTE ALIOWAITA HIVYO. ALIPASWA KUWAITA KUWA NI WATUHUMIWA. LAKINI HATA MTUHUMIWA ANA HAKI YAKE NA MOJA YA HAKI YAKE MUHIMU KABISA NI YA KUPATA FURSA YA KUJIBU TUHUMA ZAKE. KWA HIYO JAJI WEREMA HAKUWA AMEFUNGWA MDOMO KISHERIA ASIZUNGUMZE JAMBO LOLOTE KUHUSU HIYO SHUTUMA YA ESCROW, MAANA NDO NAFASI PEKEE ALIYOKUWA NAYO KWA MUDA HUO. HIYO HAIKUWA NA TAFSRI KWAMBA MTUHUMIWA HAWAZI KUAMUA KESI YAKE MWENYEWE YAANI THAT THE JUDGE CANNOT JUDGE HIS OWN CASE. WHAT THE HON. JUDGE WAS DOING WAS TO RESPOND TO WHAT WAS SAID BY THE HON. PARLIAMENTARIAN AND THAT HE WAS DELIVERING THE JUDGMENT AS THIS MATTER HAD BEEN ALREADY LEFT TO OTHER RELEVANT OUTHORITIES WITH A MANDATE TO INVESTIGATE AND COME UP WITH THEIR FINDINGS. KWA HIYO KAFULILA PIA ALIKOSEA AMA KWA KUJUA AU KUTOKUJUA NA NDO MAANA NIMEVUNJA UKIMYA HUU KUMWELIMISHA YEYE NA WENGINE WATAKAOTAKA ELIMU HII YA BURE AMBAYO MARA ZOTE HUWA NAITOA KWA MALIPO EITHER MAHAKAMANI AU KWA CONSULTANCY.
JAMBO JINGINE KWA KAFULIRA NAONA KAMA ANALIFANYA LA KISIASA ZAIDI AU ANATAKA COVERAGE YA VYOMBO VYA HABARI. KWA NINI NASEMA HIVO? NI KWA SABABU ANASEMA KATISHIWA KUUAWA NA AG. SHERIA IKO WAZI KWAMBA MAKOSA YOTE YA JINAI YANASHUGHULIKIWA NA JESHI LA POLISI. HIVYO ALIPASWA KUTOA TAARIFA KITUO CHA POLISI KILICHO KARIBU NAYE KUHUSU KUTISHIWA KWAKE KUUAWA NA SIYO KUMWANDIKIA SPIKA BARUA NA KUTOA NAKALA YA BARUA HIYO KWA MKUU WA JESHI LA POLISI. HIZO NI POLITICS NYEPESINYEPESI TU AMBAZO ZINA LENGO LA KUOMBA HURUMA YA UMMA. IKIWA KILA RAIA WA NCHI ATATENDEWA MAKOSA YA JINAI NA KURIPOTI KWA MKUU WAKE WA KAZI NA KUTOA NAKALA KWA MKUUI WA JESHI LA POLISI AU RPC, AU OCD AU OC CID TUTAFIKA WAPI NA HUU NI UTARATIBU GANI WA KISHERIA? NILITEGEMEA WATUNGA SHERIA PIA ANGALAU WANAJUA UTARATIBU WA SHERIA KUMBE HAWJUI, NGOJA BASI SISI WASAIDIZI WA WAFAFANUA SHERIA TUWASIDIE TARATIBU ZILIVYO ILI WACHUKUE FURSA HII KUWASAIDIA HATA WAPIGA KURA WAO. MH. KAFULIRA UTARITIBU WOTE ULIOFANYA MPAKA HAPO NI NULLY AND VOID UNTIL YOU OBSERVE THE PROPER PROCEDURE ILA SPIKA NAYE ALIKOSEA KUTOKUKUPATIA MAJIBU SAHIHI ULIPOOMBA MWONGOZO WA SPIKA KUHUSU SAKATA LENU HILO LA KISIASA. NINGEKUWA NI MIMI SPIKA NINGEKUSHAURI IPASAVYO KUHUSU KUTISHIWA MAISHA KAMA NILIVYOSEMA HAPO JUU LAKINI KUHUSU KUITWA TUMBILI NINGEMWAMURU AG KUFUTA KAULI YAKE MARA MOJA. ASANTE NA KWA HERI ILA BUNGE LA KATIBA LIKIANZA KAMA MKIELEWANA UKAWA MKAINGIA BUNGENI UNGANENI NA WENGINE MLETE TASWIRA YA UTANZANIA NA SI VINGINEVYO. ALUTA CONTINUA.
ADVOCATE LEONARD ELIAS MAGWAYEGA (BOB LEO).
On Friday, June 27, 2014 3:25 PM, 'tumaini bakobi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Hili la Werema ni ulevi wa madaraka tu!
On Friday, 27 June 2014, 14:56, Magiri paul <kiganyi@gmail.com> wrote:
Sasa CHADEMA inaingiaje hapa, kwahiyo unaona ni sawa kwake kuitwa TUMBILI na AG?
Ukiwa mjinga na unajificha nyuma ya majina feki unakuwa kituko kabisa.Tarehe 27 Juni 2014 12:53 PM, MABADILIKO CHADEMA <mabadilikochadema@gmail.com> aliandika:
Kafulila ameshasahau kuwa hakufukuzwa CHADEMA, kweli binadamu tu wasahaulifu.--
On Friday, June 27, 2014 2:39:22 PM UTC+3, kiganyi wrote:Mwanasheria mkuu wa serikali jaji Fredrick Werema ametuhumiwa kumtishia kifo mbunge wa Kigoma Kusini mh David Kafulila,Imedaiwa kuwa jaji Werema alimtolea maneno hayo ya vitisho mh Kafulila jana asubuhi kwenye viunga vya bunge mjini Dodoma baada ya bunge kuahirishwa.Culled from JamiiForums
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii,mh Werema alimtolea maneno hayo ya kitisho mbele ya mwenyekiti wa Bunge Mussa Hassan Zungu,mwandishi wa habari mmoja alietajwa kwa jina moja la Butare,akiwa na waandishi wa habari wenzake ambao hawakutajwa majina yao ,wakiambatana na mpiga picha ambaye pia ametajwa kwa jina la moja la Edwin na baadhi ya wabunge kadhaa waliokuwa wanapita,mh Werema amanukuliwa akimwambia mh kafulila kwamba "I will take your head,unless you apologize"ikimaanisha atamkata kichwa iwapo hatamwomba msamaha,
Kufuatia sakata hilo mh Kafulila amemthibitishia ukweli wa madai hayo mwandishi wa Bloghii ya " http://nicholauskilunga.blogspot.com/" na kwamba tayari ameshachukua hatua kwa kuiandikia barua ya madai ya kutishiwa maisha ofisi ya spika wa bunge,huku nakala ya barua hiyo akiipeleka kwa mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Mangu na nakala nyingine ameipeleka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma(RPC Dodoma)mh Kafulila aliendelea kuongea na mwandishi wa habari hii akisema"ni kweli nimetishiwa maisha na mwanasheria mkuu wa serikali leo asubuhi kwenye viunga vya bunge,na nimekwisha chukua hatua tayari,lakini watanzania wakumbuke kwamba nilipokuwa nikichangia hoja ya ufisadi huu wa Escrow wakati wa bajeti ya wizara ya nishati,nilisema,hata kifo cha Mgimwa kilipaswa kuchunguzwa, kwasababu aliugua na kufariki kipindi ambacho kulikuwa na pressure kubwa ya kuzitoa pesa hizi za Escrow na hivyo kuna mashaka sana kuhusu kifo cha waziri huyo hasa ikizingatiwa makosa yaliyofanywa na Hazina na BOT kwa kushirikiana na wizara ya nishati na madini na jaji Werema alihakikisha hizo Bilioni 200 zinatolewa"alimaliza kuongea mh Kafulila.
Mbunge Kafulila ambaye pia ni mbunge Kigoma kusini kupitia chama cha NCCR na waziri kivuli wa wizara ya Viwanda na Biashara,aliendelea kumweleza mwandishi wa habari hii kwamba jaji Werema anajua kila kitu kilichotokea kwenye mchakato huo,anasema jaji Werema ndiye aliyetoa ushauri wa kisheria na kuelekeza bank kuu kuruhusu utolewaji wa fedha hiyo na aliruhusu hayo akiwa kama mwansheria wa mkuu wa serikali,na hatua yake yake hiyo ya kuruhusu utolewaji wa fedha hiyo kufuatia wizara ya nishati na madini kuwa tayari ilikwisha saini makubaliano na kampuni aliyoiita ya kitapeli inayomilikiwa na mtu alieitwa na mh Kafulila kuwa Singasinga ijulikanayo kama PAP iliyopewa fedha hizo kama mmiliki halali wa wa fedha hizo wakti haikuwa na sifa hiyo.
Nae mh Werema alipopigiwa simu na mwandishi wetu na kutakiwa kuthibitisha ukweli wa taarifa hizi za madai ya kutishia kumwua mh Kafulila alijibu"Hilo jambo si jambo la kitaifa,tafadharini sana msilifanye kuwa la kitaifa,mimi nilifikiri umenipigia kwa ajili ya kuzungumzia mambo ya kitaifa,kwa hili sina majibu naomba uniache nipumzike"alimaliza kuongea mh Werema huku akikwepa swali la msingi alilokuwa ameulizwa na mwandishi hii,
Sakata hili liliibuka jana bungeni mjini Dodoma,kufuatia mwongozo uliokuwa umeomba na mh Kafulila kuhusiana na majibu ya waziri wa nishati na madini aliedai kwamba alilidanganya Bunge na kusema uwongo ndani ya bunge tena mbele ya waziri mkuu,pale alipokuwa akijibu hoja juu ya madai ya ufisadi kwenye akaunti ya Escrow na kusema kwamba fedha hizo zilitolewa baada ya kesi kuamuliwa,ndipo alipotaka muongozo katika suala hilo hali iliyomlazimisha mwanasheria wa serikali jaji Werema kuingilia kati na kujibu swala hilo kwa kusema taratibu zote zilifuatwa wakati wa utolewaji wa fedha hizo, na ni kweli kesi ilikuwa imekwisha amuliwa,wakati akiendela kuongea mh Werema alienda mbali zaidi kwa kulitolea mfano wa kabila lake kwamba wanamsemo mmoja kwamba Tumbili hana maamuzi ndani ya msitu hali iliyotafsiriwa kumlenga Kafulila ambaye nae alimjibu kwamba ni mwizi hali iliyompandisha hasira zaidi jaji Werema huku akivuka mstari na kutaka kwenda kumpiga mh Kafulila kabla wabunge kumzuia jaji Werema na baadae kutolewa nje na askari wa bunge.
Mheshimiwa Kafulila alisema kinachofanywa na serikali ni sawa na kile kilichotokea mwanzoni mwa miaka ya 2006 na 2007 pale katibu mkuu wa CHADEMA na aliekuwa mbunge wa jimbo la Karatu Dr Wilbroad Slaa pale alipoibua ufisadi mkubwa kwenye akaunti ya madeni ya nje yaani EPA,alisema mwanzoni mwa sakata lile serikali na chama cha mapinduzi walilipinga sana na kusema madai yale yalikuwa ya uzushi mtupu na kwamba hayana ukweli wowote,lakini baadae yalibainika kuwa madai ya kweli,
Tulijaribui kuwasiliana na ofisi ya spika kuthibitisha madai ya kupokea barua hiyo,lakini ilishindikana mpaka tunakwenda mtamboni,lakini tunawaahidi wasomaji wetu wapendwa kwamba kesho tutaweka hapa nakala ya barua hiyo,hivyo endelea kutusoma na kutufuatilia.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment