Friday, 4 July 2014

Re: [wanabidii] MASANJA NI VIZURI UKACHAGUA MOJA!

Kwa muda mrefu wanaume na wanawake wengi wamelitumia jina la Yesu kitapeli na kinafiki na ndiyo wanavyopenda iwe hivyo. Wametafuta kuwatumikia mabwana wawili na ni waongo na wadanganyifu mbele za Mungu. Wakati walitakiwa kuchukua majukumu ya uinjilishaji duniani, hawafanyi hivyo kabisa bali  ni wenye tamaa ya mali,  watafutao kipato chao wenyewe. Katika kufanya hivyo wamechukuliwa katika njia za tamaa na uasi. Ni kwa sababu wamekataa njia ya unyenyekevu iliyo katika Kristo.
Bado wanadhani kuwa katika matendo yao ya kipagani, usanii wao wote, mapato yao ya dhambi, kwamba kwa namna fulani ni Mungu anawabariki. Mungu anawalaani, kwa maana amewageuza watawaliwe na sanamu, watawaliwe na miungu mingine na watawaliwe na wapenzi waliowachagua zaidi ya Mungu.
Wanamtia Mungu kichefuchefu. Wametoa kafara uaminifu wao kwa miungu yao na wanapangusa midomo yao kana kwamba hawajafanya kosa lolote. Hawampendi Mungu bali wanajipenda wenyewe na mapepo yanayowatawala. Wamemwacha  Mungu, hawajashika upendo wao wa kwanza, wala kutembea katika ukamilifu. Hawajauzika ule utu wao wa kale, utu wao wa zamani, njia zao za zamani bali wameuacha kushamiri. Wakati wote wanajigamba, wanajivuna jinsi walivyofanikiwa, lakini mbele za Mungu ni maskini wakubwa na wahitaji.
Wakati Yesu alipokuja katika dunia hii na kutembea kama mwanadamu, watu wa dini walikuwa shabaha yake ya kwanza  kuwakemea. Ni kwa sababu kutokana na udini wao, kiburi chao, walikataa kuipokea kweli. Walimezwa na kule kujiona bora katika njia zao wenyewe na walikuwa mbali kabisa na Yeye. Wakachukuliwa katika kile kilichokuwa uchungu kwake, kwa sababu walikataa kutubu.
Watu wamelitumia bure jina la Yesu, wamejigamba kana kwamba ni Yeye wanamtumilia kumbe sio. Waneleta kiwango cha uharibifu, cha dunia, cha uchafu, cha uovu kiasi kwamba wenye dhambi hawahukumiwi tena. Wanaonekana ni wenzi wao katika dhambi, wenzi wao katika genge moja. Wakati watumishi wa Mungu wafanyapo manbo ya aibu, hata mbele za wapagani, wanakuwa chukizo kwa Mungu.
Mungu hakutarajia watu wake wamwaibishishe kiasi hicho. Wengi wa wanaojiita watumishi wa Mungu wameshaanguka. Ni kwamba hawatakiwi kutafuta siku kubwa ambayo wataanguka, kwa maana wamekwisha timiza kusudi. Hilo ni kusudi la yule mwongo, mdanganyifu, awachukuaye watu katika shimo la matapishi yao wenyewe.
Kama mtu atatubu kisawasawa, ikimaanisha kwamba kubadili njia zake ovu, na kuja katika njia ya Mungu, mtu huyo atampendeza Mungu. Mtu anapotubu ki kweli, kwa maana kwamba anaziacha njia zake mbaya, na kufanya kile Mungu atakacho  na aagizacho ataona nini? Atamwona Mungu ampaye rehema kila siku.

On Friday, July 4, 2014 10:51 AM, 'ezekiel kunyaranyara' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Mimi nafikiri maombi mazuri ya kumwokoa mtu ni pamoja na kukemea na kuonesha njia kama inavyofanyika hapa katika mjadala huu.

K.E.M.S.

On Friday, 4 July 2014, 9:39, Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com> wrote:

Uchungaji ama Ushemasi au hata Uaskofu hausomewi....mwongozo kamili upo kwenye Biblia. Haya masomo ya teolojia na nduguye Divinity...yamekuja kibinaadamu ili kumsoma Mungu. Nafikiri tusijadili sana haya kwasababu hao wasomi wetu walioko mimbarani na madhabahuni pamoja na kusoma na kutafakari kwa muda pamoja na kulelewa bado wakipata upenyo wanaasi vibaya hakuna cha Lutherani au Moravian, Anglican, Baptist au Roman Catholic....jambo la msingi kama mtu kaamua kumtumikia Mungu basi tuendelee kumwombea asismame kwenye hilo kusudi la Mungu....

2014-07-04 9:00 GMT+03:00 Joseph Ludovick <josephludovick@gmail.com>:
Marcus,
Nafikiri unaongelea malezi ya mapadre wa kanisa katoliki.
Masanja siyo mwinjilisti au padre wa kanisa katoliki. Kwa hiyo umuongelee kwa context ya huko aliko not on comparative basis.
Pili hata mapadre kanisa katoliki wapo wanaofuga rasta kabisa achilia mbali mabutu.
Ufalme wa Mungu siyo hayo
On 4 Jul 2014 08:52, "'marcuskabwella@yahoo.com' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Kwako Mr. Ekuranya!
Kwanza nakupongeza kwa ushauri wako kwa kijana wetu, Tatizo linalojitokeza kwa waliowengi hasa watu maarufu wamechukulia wokovu na uchungaji kama kitu cha mchezo sana.
Masanja namfahamu sana na kabla ya kujiita mlokole tulikuwa tunasali kanisa moja, kwa kanisa ninaloabudu mchungaji ni lazima amalize kidato cha sita na afaulu vizuri na anapewa muda wa kujitafakari mwaka mzima baada ya hapo akasome masomo ya falsafa na taaluma mungu na huko afaulu vizuri sambamba na hayo jamii inakuwa na jukumu la kumlea kwa sala na maombi.
Baada ya hapo atapelekwa kwenye mazingira atakayoishi na jamii husika ikiendelea Ku Lea mpaka siku ya kuwekwa wakfu si chini ya miaka tisa sasa najiuliza eti mtu maarufu,tajiri akiokoka siku mbili eti in Askofu najiuliza huu uaskofu wa kujibambika wanaona sifa? Mtu hajajua watu wanaomuelekea Mungu wanahitaji nini hujui matokeo yake kila usimamapo madhabahuni ni kukashifu dining za watu na vifungu viingi vya kuhamasisha sadaka.
Katika hili kuna upotoshaji wa hali ya juu.
Namkumbuka mtu mmoja baada ya kumaliza first degree ya electrical engineering akaamua kumtumikia Mungu kwa kuwa kuhani alijifunza muda wa kutosha na leo ni mfano wa kuigwa. Sasa masanja kutoka kwenye kazi ya kukusanya magazeti pale IPP media uchekeshaji akajiona ameiva na kuvamia uchungaji hana falsafa wa taaluma Mungu kwa asisuke mabutu na kusimama mimbarini? Nani atamshauri wakati aliemkaribisha alifanya hivyo kwa lengo la kupiga noti.
Uchungaji sio mchezo jamani zaidi ya kutumikiwa mchungaji ni mtumishi, makanisa yanayoibuka kama uyoga watapata muda kweli kuandaa watumishi?
Masanja huu ni ushauri kwa watu wanaokupenda tungekuwa na no yako ya simu tungekutafuta private ila jitafakari maana muonekano wa nje huwakilisha kilichomo ndani!
Nawasilisha.

From: 'ekunyaranyara' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] MASANJA NI VIZURI UKACHAGUA MOJA!
Sent: Fri, Jul 4, 2014 2:45:22 AM

Ni ushauri mujarabu. Nafikiri hata kwa sisi wengine hapa jukwaani umetukumbusha kurejea mienendo yetu. Barikiwa.

Sent from Samsung Mobile

-------- Original message --------
From: Fakhi Karume
Date:03/07/2014 19:09 (GMT+03:00)
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] MASANJA NI VIZURI UKACHAGUA MOJA!

KWAKO, Emmanuel Mgaya 'Masanja'. Naamini u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Kwa upande wangu nipo sawa, nakimbizana na maisha.
Nina machache ya kukushauri kuhusiana na maisha yako kama staa ambaye kwa sasa umetangaza kuokoka. Kwa maneno mengine ni kwamba, umeondoka kwenye utaifa, upo mikononi mwa Muumba wako.Nimekufahamu kwa kitambo kidogo. Kwangu mimi, wewe ni mmoja wa mastaa wa ukweli katika uchekeshaji Bongo. Mwenye kipaji cha hali ya juu na unayejua unachokifanya.
Tatizo ni kwamba, nashangazwa na aina ya maisha yako baada ya kutangaza kuokoka. Ninavyojua mimi, kuokoka ni kuachana na maisha ya awali ambayo (pengine) yalikuwa hayampendezi Mola na kugeukia katika maisha safi.Niliposikia umeokoka nilifurahi kuona kuwa umeelekea sehemu sahihi zaidi kiimani. Lakini moyoni nilikuwa na shaka kidogo maana wapo wasanii wengi kwenye uigizaji ambao walitangaza kuokoka lakini baadaye wakaonekana kwenye njia zao za awali.
Ukiachana na waigizaji, pia kuna wasanii wa Bongo Fleva ambao nao waliingia kwenye ulokole na mara wakaamua kurudia maisha yao ya awali.Baadaye nikasikia kuwa unasomea Uchungaji (ingawa inaelezwa kuwa ni Uinjilisti), hapo sikuwa na shaka tena na wokovu wako. Niliamini kwa mtu ambaye ameamua kuingia kwenye kufundisha wengine njia iliyo sahihi hawezi kudanganya kuwa ameokoka.
Siyo kama naingilia maisha yako au nakukosoa kwenye suala la imani yako. Uzuri ni kwamba, nami ninaamini katika imani yako, hivyo sioni tatizo kukushauri.Tatizo lipo kwenye staili yako ya maisha. Ni kweli kwamba umeokoka, lakini itawezekana vipi usuke mabutu kichwani? Maandiko yanaeleza wazi kuwa, wanaoamini ni barua inayosomeka kwa watu wote.
Je, watu watasoma nini kupitia mabutu? Unaweza kusema kuwa, imani ya mtu iko moyoni, hapo sitakubaliana na wewe, maana kinachoonekana nje, kinawakilisha kilichomo ndani.Vipi kama kanisa zima, wanaume wataingia wamesuka? Nafikiri si jambo sahihi. Watu watapata shaka na wokovu wako, tena mchunga kondoo. Wengine wanaweza kuona wokovu si jambo 'serious'. Kwamba mtu anaweza kuingia na akaendelea na mambo yake yaleyale, jambo ambalo si la kweli.
Wokovu ni pamoja na mwonekano wa nje. Mavazi, mitindo ya nywele n.k.Jambo jingine ambalo limenishangaza ni namna unavyoingiza komedi kwenye mambo yanayohusu dini.Usahihi wa kufanya utani kwenye vichekesho huku ukitaja jina la Mungu unatokea wapi? Masanja tumezuiwa kufanya mzaha au kulitaja bure Jina la Mungu wetu.
Nakushauri kama ni kweli umeamua kuokoka, badilika lakini kama unahisi bado unatamani maisha ya kawaida na kujichanganya, chagua moja ili jamii isikutafsiri tofauti.Ni uamuzi wako kufuata au kuacha hapahapa, lakini la muhimu ni kwamba, nitakuwa nimeshakushauri. Ubarikiwe sana mpendwa!
Yuleyule,
Mkweli daima,
.........................
Joseph Shaluwa.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Bariki G. Mwasaga,
P.O. Box 3021,
Dar es Salaam, Tanzania
+255 754 812 387

0 comments:

Post a Comment