'Chris' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Na lowassa mbona ni kama anajitetea kuwa ni ng'ombe mia nane tu kana kwamba kuwa tajiri ni dhambi?tufike mahali tusione kuwa maskini ni sifa ya uongozi mara nyingine umaskini ni simply lack of larger vision of oneself and poor imagination.Kuna fursa nyingi tu zimejitokeza Tanzania ambapo mtu anaweza kuwa tajiri.Tusione utajiri ni dhambi.Utajiri ni jambo hema wore tunafanya kazi kwa bidii ili tutajirike.
Sent from my iPhone
Bwana Mrema,Mwandishi wa habari hapaswi kulaumiwa kwani yeye ametimiza kazi yake ya kufikisha ujumbe kwa wasomaji wake na hicho alichoripoti ndicho alichoelezwa na Lowasa. Wewe ulitaka aandike nini zaidi ya hicho alichopata kutoka kwa mhusika mwenyewe? Sasa ni juu ya wasomaji kujudge kama mhojiwa kasema ukweli au la, sio kumlaumu mwandishi---humtendei haki hata kidogo.On Wednesday, July 2, 2014 12:29 PM, Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com> wrote:
Jamani imefika mahali tuseme kuwa hii inatosha. Sikutegemea gazeti la hadhi ya mwananchi nalo kujishusha kufikia hadhi ya gazeti la mitaani ambalo nia yake ni kujiuza hata kwa kutumia mbinu za porini. Huyu mwandishi wetu aliyeaandika taarifa kuhusu kuwa "Lowassa aweka wazi utajiri wake" ni mbabaishaji na hana hadhi ya kuitwa mwandishi. Kilichopo kwenye andiko hilo sio kabisa kinachofanana na kichwa cha habari. Tunamwomba atuombe radhi wasomi wa gazeti hili kwani ametudhalilisha.
Ina maana huyu mwandishi anakubaliana na maneno ya Lowassa kuwa mali zake ni ngombe 800 tu na hana mali nyingine? Je alifanya utafiti kidogo kujua kama alichosema Lowassa kina ukweli?. Mimi binafsi siamini hivyo kwani wewe na mimi tunajua kuwa Lowassa ni tajiri na ana mali nyingi zaidi ya ngombe 800.
Ukweli binafsi nikisoma tena taarifa za namna hiyo nitaacha kabisa kununua gazeti la Mwananchi ijapokuwa mimi ni mnunuaji na msomi mzuri wa gazeti hili.
Ahsante
Herment A. Mrema
Date: Wed, 2 Jul 2014 11:55:50 +0300
Subject: Re: [wanabidii] Lowassa aweka wazi utajiri wake
From: mngonge@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.comNilidhani kataja mali zake kumbe ni projo za mhandishi wa makala hii tu. Ina maana anamiliki ng'ombe 800 tu hakuna vitu vingine anavyomiliki? Kitendo cha kutaja ng'ombe tu huku akiziacha mali nyingine kinatia shaka na hata yeye mwenyewe kama alitaja ng'ombe tu ina maana anapata shida kuzitaja mali zake za ukweli. Lakini hata mtu kumiliki ng'ombe 800 si mchezo ni utajiri mkubwa tu
Subscribe to: Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment