Thursday, 3 July 2014

Re: [wanabidii] Lowassa aweka wazi utajiri wake

hizo chuki zako binafsi mzee


On Thursday, 3 July 2014, 8:13, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Mimi nilifikiri unataka kujiuliza na kumuuliza kwa nini miaka yote toka ashutumiwe kuanzia Mwalimu Nyerere akiwa hai alisubiri nini ndiyo aseme leo? Nilifikiri utamuuliza pia kuwa labda alikuwa anaweka mambo sawa ili akisema basi waliosema ukweli enzi hizo iwe kwamba ulikuwa uwongo?
Maswali kama hayo  na mengine ambayo sioni sababu ya kumuulisa (maana haimsaidii wala kulisaidia taifa) ndiyo muhimu sana au labda angeamua kunyamaza tu


On Thursday, July 3, 2014 7:58 AM, 'Ngupula GW' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Nawaunga mkono wote wanaoanza kufunguka. Utajiri sio dhambi na nadhani hatupaswi kabisa kuwa na mifumo ya kunyanyasa matajiri wetu kwani watatukimbia na nchi itabakia na wapiga hadithi tu...

'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

 Niliposoma gazeti kuwa ana mifugo-ng'ombe 800+ niliona anastahili kukamatwa au kushitakiwa kwa kuchangia uharibifu wa mazingira. Hao amewafuga kisasa au ni wale wa kuzurura na kugawia wachungaji wanaohamahama nao nchi zima yeye akipata mafao. Hakutaja mifugo mingine-mbuzi, punda, kondoo, mbwa wa kusindikiza mifugo malishoni. Ikiwa ktk semi-arid area kama Monduli ng'ombe mmoja anatakiwa kutumia 5 square acres kama ndio sustainable level ya ufugaji, yeye ana ekari ngapi. Si ina maana anamiliki vijiji kadhaa pekee? amepanda nyasi za kulishia kwa zero grazing au ndio migratory pastoralism.Kamata huyu!! Amefufua visima vya mkoloni boreholes za mashamba ya ngano ya zamani, kajenga dip na nywesheo lake ananywesha mifugo yake na kuongesha? au ananyweshea mtoni? Ng'ata meno Mh Werema yupo wapi hii ya Mh Kafulila ihamie huku maana tumechoka sasa kuona viongozi sio role models katika kilimo, ufugaji na uhifadhi mazingira; umiliki ardhi-kujilimbikizia kujipa mashamba ya zamani ya serikali. huyu ni mwekezaji wa ndani-anafaidishaje vijiji vinavyomzunguka, anavipa mafao gani?
Mbona kabila lake linazidi kumomonyoa ardhi kwa kufuka beyond land's carrying capacity, makorongo, dryland na kutafuta maji kilometa kadhaa kutwa na wanawake na watoto kuteseka. kule kulikuwa na mashamba ya ngano ya wazungu wakati kabla ya uhuru na kila shamba lilikuwa na deep boreholes. Amefufua ngapi kuwapa mafao nduguze. Hadi wazungu wanakuja kufufua baadhi kuwapa wamasai maji, kuwajengea josho na nywesheo yeye amejenga mangapi? ngoja nigombee ubunge maana tumechoka kuchapwa bakora kwetu, siku hizi wanabaka na kubaka kama adhabu ya kufukuza mifugo isile mazao yako shambani.

Ningekuwa na chopa ningeiondoa mifugo Kilosa na Morogoro Rural Kwa Mh Nkya na Kologolesi na huko inakohamia Kilwa na Lindi na watu kupigwa mikuki  na ningeishusha shambani kwake huyu bosi alambe uchungu ile imalize nyasi, mazao ili naye aone umuhimu ya kuongea na nduguze masuala ya mabadiliko, ufugaji endelevu kwa maendeleo na kipato kuondoa uamsikini na kujiendeleza kifamilia sio kuzurura na kutesa wengine kwa sifa ya kimila ya utajiri wa mifugo bila kujali sustainability ya maisha na mifugo. sasa wamekausha Ruvu River, Mgeta, Mkulazi vyanzo vya maji Morogoro Milimani. DAWASA inahaha kkt kupatia maji DSM na miji mingine. Ruaha viboko na mamba wanaombea masika iendelee mwaka mzima; Mbeya Rukwa ndio kufukuzana wasikate misitu na kuhamia hao wasukuma wafugaji na wakulimwa (kwao wanamlima mcheke vibaya sana lakini hawalishii mifugo). Huyu anamiliki ekari ngapi, wapi na wapi?

 Mwandishi katembelea miliki zake zote Tanzania nzima. Alipataje ardhi ya kufanya uwekezaji huo wote? Alitumia nafasi ya cheo chake kujilimbikizia mali au alirithi toka kwa baba? Ninaomba KURA niingine bungeni nikamuhoji.



On Thursday, 3 July 2014, 0:16, "hosea.ndaki@gmail.com" <hosea.ndaki@gmail.com> wrote:


Chris, nakuunga mkono watz tubadilike tusione utajiri ni dhambi, tuachane na mawazo ya kimasikini kuwa watanzania uwezo wao kutengeneza maji ya chupa na sio visima vya gesi.

Hebu tizama yusufu manji anavyotia rupia yanga hadi maximo karudi ati. Ona chamazi pale ni nguvu ya mkwanja.

Hili la kudhani kuwa umasikini ni sifa inabidi ifike sehemu ukome, ikibidi kiongozi kabla ya kuchaguliwa aweke dhamana ya mali ili akituingiza mkenge tukamate dhamana yake.

Tuweke utaratibu waziri lazima awe na mali isiyohamishika ili akiingia mkataba wa kipumbavu tutaifishe.

Tunachagua kingozi asiyekuwa na majukumu kutwa nzima anazurura, angekuwa hata na ngombe wa maziwa angetumia muda wake wa weekend kutizama mifugo yake. Umasikini umeshatuchosha tunahitaji mtu wa kutusukuma mbele.
----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: 'Chris' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: "wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment