Wednesday, 2 July 2014

Re: [wanabidii] Lowassa aweka wazi utajiri wake

Bwana Mrema,
Mwandishi wa habari hapaswi kulaumiwa kwani yeye ametimiza kazi yake ya kufikisha ujumbe kwa wasomaji wake na hicho alichoripoti ndicho alichoelezwa na Lowasa. Wewe ulitaka aandike nini zaidi ya hicho alichopata kutoka kwa mhusika mwenyewe? Sasa ni juu ya wasomaji kujudge kama mhojiwa kasema ukweli au la, sio kumlaumu mwandishi---humtendei haki hata kidogo.

On Wednesday, July 2, 2014 12:29 PM, Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com> wrote:

Jamani imefika mahali tuseme kuwa hii inatosha.  Sikutegemea gazeti la hadhi ya mwananchi nalo kujishusha kufikia hadhi ya gazeti la mitaani ambalo nia yake ni kujiuza hata kwa kutumia mbinu za porini.  Huyu mwandishi wetu aliyeaandika taarifa kuhusu kuwa "Lowassa aweka wazi utajiri wake" ni mbabaishaji na hana hadhi ya kuitwa mwandishi.  Kilichopo kwenye andiko hilo sio kabisa kinachofanana na kichwa cha habari.  Tunamwomba atuombe radhi wasomi wa gazeti hili kwani ametudhalilisha. 

Ina maana huyu mwandishi anakubaliana na maneno ya Lowassa kuwa mali zake ni ngombe 800 tu na hana mali nyingine? Je alifanya utafiti kidogo kujua kama alichosema Lowassa kina ukweli?.  Mimi binafsi siamini hivyo kwani wewe na mimi tunajua kuwa Lowassa ni tajiri na ana mali nyingi zaidi ya ngombe 800. 

Ukweli binafsi nikisoma tena taarifa za namna hiyo nitaacha kabisa kununua gazeti la Mwananchi ijapokuwa mimi ni mnunuaji na msomi mzuri wa gazeti hili.

Ahsante

Herment A. Mrema

Date: Wed, 2 Jul 2014 11:55:50 +0300
Subject: Re: [wanabidii] Lowassa aweka wazi utajiri wake
From: mngonge@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Nilidhani kataja mali zake kumbe ni projo za mhandishi wa makala hii  tu. Ina maana anamiliki ng'ombe 800 tu hakuna vitu vingine anavyomiliki? Kitendo cha kutaja ng'ombe tu huku akiziacha mali nyingine kinatia shaka na hata yeye mwenyewe kama alitaja ng'ombe tu ina maana anapata shida kuzitaja mali zake za ukweli. Lakini hata mtu kumiliki ng'ombe 800 si mchezo ni utajiri mkubwa tu

2014-07-02 9:47 GMT+03:00 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>:
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema madai kwamba yeye ni tajiri hayana ukweli wowote. Amesema yeye ni mfugaji na anamiliki ng'ombe zaidi ya 800 katika Jimbo la Monduli, mkoani Arusha.
Lowassa alisema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisini kwake wiki iliyopita mjini Dodoma.
 "Haya madai hayana hata chembe ya ukweli hata kidogo, isipokuwa mimi nadhani wananitakia mema kwa sababu ukiona jumba zuri wanasema la Lowassa, gari nzuri la Lowassa, kitu chochote kizuri wanasema cha Lowassa," alisema na kuongeza:
"Wamesema uongo mwingi sana, mimi nasema tu nilichopata nimepata na sina utajiri kiasi hicho, lakini si mbadhirifu wa haki zangu ninazopata kama mshahara na haki nyingine."
Alipotakiwa kutaja mali anazomiliki, Lowassa alisema: "Mimi ni mfugaji, nina ng'ombe zaidi ya 800 jimboni kwangu Monduli."
Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli, alisema madai kwamba anamiliki utajiri uliopindukia yalianza kabla hajajiuzulu uwaziri mkuu na ilielezwa kuwa "maduka fulani" ni yake.
Alibainisha kuwa hata kampuni ya Alphatel ambayo wanamiliki kwenye familia yake iliwahi kuhusishwa na jengo kubwa lililojengwa na mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia wilayani Kinondoni, Dar es Salaam likiitwa Alpha.
"Ikaonekana ni jengo langu, kule Mbezi kuna rafiki yangu mmoja walienda watu wakasema hii nyumba ya Lowassa. Yule bwana alitoka na bastola akawakimbiza. Mimi sina nyumba maeneo hayo," alisema Lowassa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment