Wakiingia msituni mbona ndio itakuwa nafuu yetu
On 4/23/14, 'Gikaro Ryoba <gikaroryoba@yahoo.com>' via Mabadiliko
Forum <mabadilikotanzania@googlegroups.com> wrote:
> Ushahidi
> mdogo tu unaoonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuziendesha kuliko serikali
> 2
> unapatikana katika rasimu ya katiba inayojadiliwa sasa hivi Dodoma, ambayo
> inapigwa vita na kundi la wengi kwa nguvu zao zote (na hata ikibidi wako
> tayari
> kuingia msituni kutetea serikali 2). Sura zifuatazo zinadhihirisha gharama
> hizi:
>
> USHAHIDI
> WA KWANZA
> Sura
> ya saba, ibara ya 98(2). Kifungu hiki kinasomeka ifuatavyo:
>
> "Kwa
> madhumuni ya ibara ndogo ya 98(1), idadi ya mawaziri na manaibu waziri wa
> serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitazidi 15". Mwisho wa kunukuu.
>
> Idadi
> ya mawaziri na manaibu waziri katika serikali ya sasa ni zaidi ya 60! Kila
> waziri
> analipwa mshahara (excluding gharama za nyumba, gari, mafuta, safari na
> anasa
> zingine) wa Tsh 20,000,000. Jumla ya mshahara kwa mawaziri 60 wa serikali 2
> ni
> Tsh 20,000,000×60= 1,200,000,000. Hizi ni Tsh 1.2 billion (sawa na Tsh 14.4
> bilion kwa mwaka).
>
> Mshahara
> wa mawaziri 15 wanaopendekezwa katika serikali 3 ni Tsh
> 20,000,000×15=300,000,000.
> Hizi ni Tsh million 300 (sawa na Tsh 3.6 billion).
>
> Kwa
> hivyo mtaona kwamba gharama ya kuendesha mawaziri 15 wa serikali 3 ni
> rahisi
> kwa Tsh billion 10.8 sawa na 75%. Haya, sasa wale mnaodai kwamba serikali 3
> ni
> ghali huwa mnatumia kigezo gani? Msidhani kila mtanzania ni zuzu. Mnaposema
> ughali
> au urahsi sharti muoneshe mnakokotoaje hizo gharama, sio watu
> wanakaririshwa
> majibu kwenye vikao halafu wanakuja kupayuka hadharani bila takwimu. Huo ni
> ujuha!
>
> USHAHIDI
> WA PILI
> Kwa
> mujibu wa rasimu ya katiba ibara ya 113(1) na (2) idadi ya wabunge
> inayopendekezwa kwenye rasimu ni wabunge 70 wa kuchaguliwa (50 kutoka
> Tanganyika
> na 20 kutoka Zanzibar) na 5 walemavu watakaoteuliwa na rais. Hawa ni sawa na
> jumla
> ya wabunge 75. Bunge la sasa lina jumla ya wabunge 389 wa kuchaguliwa na 10
> wa
> kuteuliwa, sawa na wabunge 399. Kila mbunge hulipwa Tsh 11,000,000
> (+5,000,000
> za jimbo)=16,000,000. Wabunge wote 399 wanalipwa jumla ya Tsh
> 399×16,000,000=6,384,000,000
> (sawa na billion 6.4). Gharama ya wabunge hawa kwa mwaka ni Tsh 76.4
> bilion.
>
> Gharama
> kwa wabunge 75 wa serikali 3 ni Tsh 16,000,000×75=1,200,000,000(sawa na Tsh
> 14.4 bilion kwa mwaka).
> Tofauti
> ya gharama za kuendesha bunge la serikali 2 ukilinganisha na bunge la
> seriakli
> 3 ni Tsh 62 bilion. Sasa hawa waongo wanaosema kwamba kuendesha serikali 3
> ni
> ghali wanatumia kigezo kipi hawa vilaza?
>
> KUMBUKA:
> Ukokotozi
> wa gharama uliofanywa hapo juu haujumuishi gharama za mishahara,
> marupurupu,
> mafuta, safari, anasa, nk za makatibu wakuu, makamishina, wakurugenzi na
> wakuu
> wa idara katika wizara husika. Ukijumlisha na gharama za kuwalipa viongozi
> hawa
> pesa zitakuwa nyingi zaidi ya mara mbili ya hizo zilizokotolewa hapo juu.
> Huu ushahidi
> unatosha kabisa kuonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuliko serikali 2. Kwa
> hiyo,
> ule uongo mnaoambiwa na wanasiasa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2
> mnapaswa
> kuupuuzilia mbali. Wanakudanganyeni kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa ili
> waendelee kukukandamizeni, kukumasikinisha na kukuchukulieni kama mazuzu wa
> kupandia ngazi za madaraka na kujichumia mali kwa ajili ya matumbo yao
> binafsi.
>
>
> TAHADHARI
> Kwa
> upande mwingine, ifungu hivyo nilivyonukuu hapo juu ni mwiba mkali kwa CCM
> kwani vinawanyima uhuru wa kujitungia wizara na kuwapa uwaziri makada wao
> kama
> zawadi kwa kazi nzuri ya kukitumikia chama. Wanapenda tuendelee na mfumo
> ghali
> wa serikali 2 ili wananchi waendelee kubebeshwa gharama za kuendesha
> serikali
> kwa manufaa yao binafsi. Mwenye macho haambiwa tazama. Kila mtanzania
> anapaswa
> kufunguka macho na kuhoji hizo gharama wanazodai wanazikokotoa kwa kutumia
> kigezo kipi. Sio mtu unakaririshwa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2
> unakubali tu kama zuzu. Unatakiwa kuhoji. Ujinga wa watanzania kutohoji
> mambo ndio
> unaosababisha wanasiasa waendelee kutudanganya na kutufanya ngazi za
> kupandia
> na kuning'inia madarakani kwa manufaa yao binafsi.
>
>
> N.B
> Uchambuzi
> zaidi kuhusu gharama kubwa za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na serikali
> 3
> utafuata baadaye. Nataka wale waongo wanaowadanganya raia kwamba serikali 3
> ni
> ghali kuliko 2 waumbuke mchana kweupe.
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forum" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
> To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
> Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
> To view this discussion on the web visit
> https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/1398266789.47389.YahooMailNeo%40web163103.mail.bf1.yahoo.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
--
mission without implementation is hallucination
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment