Yanayotokea katika bunge letu huko Dodoma ni kama mchezo wa kuigiza, lakini wenye hatari. Ni wazi kuwa hoja ya aina ya serikali katika muungano wetu imeleta mtafaruku na tofauti ya mawazo miongoni mwa wajumbe wa bunge la katiba. Hiki ni kitu cha kawaida kwani hatutarajii watu wote wakubaliane katika mitazamo na hasa katika jambo lenye umuhimu kama hili. Ikumbukwe kuwa hata huku nje ya bunge, kuna mawazo yenye mgawanyiko wa aina hiyo hiyo.
Tofauti za mawazo hujadiliwa kwa busara na uvumilivu na hatimaye makubaliano kufikiwa kwa hoja na siyo jaziba, matusi, vijembe na ushabiki kama inavyotokea Dodoma sasa. Tulioko nje tunashindwa kujua nani mwenye busara na ni kwa hoja gani makini. Ninavyofahamu mimi, demokrasia makini ni kusikilizana, kujadiliana, kuvumiliana na kukubali kushindwa kwa hoja. Hata kama kuna wingi wa kundi moja kutetea hoja fulani, ni muhimu kuyasikiliza maoni ya wachache kwani katika utekelezaji kuna mazuri yanayoweza kutumika kuongeza ufanisi.
Inasikitisha sana kuona wajmeb wengi wa Bunge letu wanakiuka kanuni walizoweka wenyewe na kuanza kuongea kwa jazba bila hata ya kuwa na hoja ya vifungu vinavyojadiliwa. Aidha, inasiktisha kuona viongozi waandamizi na wenye heshima kubwa serikalini wanajiunga katika kutoa matamshi yenye kuleta ukinzani. Wakumbuke kuwa sauti zao zina mvuto na ushawishi kwa watu.....kwa heri au hata shari.
Naomba wajumbe waliotoka watafakari njia itakayosaidia kufikisha mawazo yao ndani ya bunge kwani kutoshiriki ni kubariki mawazo ya upande mmoja. Kwa waliobaki ndani ya Bunge watumie busara ya kujadiliana jinsi ya kufikisha hoja zao bila matusi na kebehi hususan kwa tume iliyofanya kazi nzuri. Kama wameipuuza kwa vijembe kiasi hiki, je, wataweza kuisifu katika vifungu vilivyobakia? Katiba ni mambo mengi ns siyo muundo wa serikali tu.
Makongo
----------------------------------------------------------------
Japhet Maingu Makongo
Director, Ubunifu Associates Ltd
P.O. Box 32971, Dar es Salaam, TANZANIA
Website: www.ubunifu.co.tz, info@ubunifu.co.tz,
Tel: +255 22 2762027, Mobile:+255 754 571 256
Director, Ubunifu Associates Ltd
P.O. Box 32971, Dar es Salaam, TANZANIA
Website: www.ubunifu.co.tz, info@ubunifu.co.tz,
Tel: +255 22 2762027, Mobile:+255 754 571 256
0 comments:
Post a Comment