Thursday, 17 April 2014

Re: [wanabidii] SABABU ZA UKAWA KUSUSIA BUNGE LA KATIBA

Bunge Maalum la Katiba linaendelea mjini Dodoma likiwa na wajumbe kutoka vyama vya upinzani visivyokuwa na wabunge vikiwemo vya APPT-Maendeleo, Demokrasia Makini,ADC, Jahazi Asilia, Chama cha Wakulima AFP, TADEA, UPDP, CCK, Chausta, Sauti ya Umma, UMD,DP, NLD,NRA na UDP.

Akizungumza bungeni leo asubuhi mmoja wa wajumbe mh. Issac Cheyo amesema wapo wan a ukawa wanaoamini kufanya majadiliano badala ya kukimbia Kama yeye na baadhi ya wenzake waliorudi bungeni.

On Wednesday, April 16, 2014 12:57:39 PM UTC-7, ELISA MUHINGO wrote:
Wana UKAWA tulioko nje tunaona sababu zaidi za UKAWA kuondoka bungeni. Kama wanaopendekeza mfumo wa serikali mbili wangekuwa wanakuja na majibu ya sababu zilizopelekea kupendekeza serikali tatu wanaUKAWA wasingetoka bungeni. nchi haiwezi kuwa bila kiongozi watu wenyeakili mkakaa kuandaa katiba ambayo kesho nchi itaendelea kuongozwa na marais wawili.

Marehemu Nyerere akiwa rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar aliweza kushika vibuyu viwili vya mchanga kutoka Zanzibar na Tanganyika na kuuchanganya na ikawa alama ya kuunganisha nchi. Lakini Kikwete ameshindwa kupokea rasimu ya katiba na ikawa imepokelewa na Tanzania mpaka na rais wa Zanzibar apokee. Maana yake Kikwete kwa niaba ya Bara na shein kwa niaba ya Zanzibar. Kusudi ya pendekezo la serikali tatu ni kuondoa upuuzi huo. Watu wakikataa hilo bila majibu utakaa kujadiliana nini nao???

On Wednesday, April 16, 2014 10:38 PM, Vincent Mhangwa <vmha...@gmail.com> wrote:
Asante Fhaki. UKAWA wamesusa bunge baada ya kuchoka kusikiliza hoja za wanaotaka muundo wa serikali 2 kinyume na mapendekezo ya Tume ya Warioba yaliyomo ktk rasimu ya pili? Basi? Hakuna sababu nyingine?
Lakini pia sina hakika kama Katiba ya sasa ilirekebishwa kwa mara mwisho mwaka 1977.
On 16 Apr 2014 14:58, "Fakhi Karume" <fkarume@gmail.com> wrote:
Wajumbe wa bunge la kutoka vyama vya upinzani vya CUF. Chadema, NCCR , Dp, NRA, NLD na Udp ambao wanaunda umoja wao unaojulikana Kama Ukawa wamesusia bunge na kuondoka bungeni kwa kushindwa kuvumilia hoja zinazotolewa na wapinzani wao wakuu kutoka chama tawala.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba ameliambia bunge la katiba takriban saa 10.30 leo jioni kuwa wamechoka kusikiliza hoja za wajumbe wanaotaka muundo wa serikali mbili kinyume na mapendekezo yaliyotolewa na rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Jaji Warioba.
Mara baada ya kumaliza kuzungumza na kuwaaga wajumbe wa bunge Hilo kwa niaba ya wajumbe wa Ukawa prof. Lipumba aliwaongoza wajumbe wenzake wa Ukawa kutoka nje ya bunge.
Hata hivyo Wajumbe hao walioaga bunge kupitia prof Lipumba walitoka bungeni kuelekea katika ukumbi wa msekwa kufanya kikao cha ukawa huku Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba mh. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuliongoza bunge Hilo kwa wajumbe kuendelea kuchangia.
Wengi wa wajumbe kutoka kundi la 201 wapo bungeni wakiwemo wale wa kundi la viongozi wa dini.
Bunge maalum la Katiba Jumatatu saa Saba mchana lilimaliza kupokea taarifa kutoka kamati 12 zilizokuwa zinajadili sura ya kwanza na Sita zinazohusu muundo wa muungano kazi iliyofanywa kwa Siku Tatu.
Wakati wa uwasilishaji wa taarifa hizo za kamati kundi la wajumbe wachache likiongozwa na wana ukawa lilipewa masala 6 kufafanua hoja zao zilizosomwa na wenyeviti wa kamati hizo kwa niaba yao fursa ambayo waliitumia kueleza Maoni yao ya kukubaliana na muundo wa serikali 3 uliopendekezwa na Tume ya Jaji Warioba.
Hoja walizotoa ni pamoja na muungano uliopo haukuhalalishwa hususan na serikali ya mapinduzi zanzibar, kutokuwepo kwa hati ya muungano, Mwalimu Nyerere alitumia ujanja ujanja kutekeleza shughuli za muungano, waliozoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi kwani wameishi kwa uongo kwa zaidi ya miaka 50 yaani nusu karne na sasa wamefikia mwisho wake na mengine mengi.
Jumatatu mchana wajumbe wa bunge la Katiba walianza kuchangia kwa hoja zilizoonyesha kuwa muungano uliodumu kwa miaka zaidi ya miaka 50 ni halali na jana Jumanne Serikali ilitoa hati ya muungano na wajumbe hao wa kundi la waliowengi kueleza hoja zilizotolewa na wana Ukawa za kuwadhalilisha waasisi hazitendi haki kwa waasisi hao.
Bunge Maalum la katiba linaloendelea hivi sasa mjini Dodoma likishindwa kupitisha rasimu ya katiba jamhuri ya muungano wa Tanzania itaendelea kutumia KATIBA ya zamani iliyorekebishwa Mara ya mwisho 1977
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
0 comments:

Post a Comment