Wednesday, 23 April 2014

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] USHAHIDI KWAMBA SERIKALI 3 NI RAHISI KULIKO SERIKALI 2

Gikaro;
Umefikiria kuhusu gharama hizo kwa Mawaziri wote; Wabunge wote na makatibu wakuu wote (Serikali ya Muungano + hizo za washirika) kwa idadi yao na hasa ukitegemea ni kodi za wananchi haohao? Unadhani itakuwa nafuu? Hii ukiacha na hizo figure zisizo sahihi ulizoweka!





"I work in the shade to bring out the LIGHT to my Country. Shade means Patriotism, Loyalty and Integrity."

Sent from my iPhone

On Apr 24, 2014, at 2:33, Augustine Rukoma <rukomapekee@gmail.com> wrote:

Wakiingia msituni mbona ndio itakuwa nafuu yetu

On 4/23/14, 'Gikaro Ryoba <gikaroryoba@yahoo.com>' via Mabadiliko
Forum <mabadilikotanzania@googlegroups.com> wrote:
Ushahidi
mdogo tu unaoonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuziendesha kuliko serikali
2
unapatikana katika rasimu ya katiba inayojadiliwa sasa hivi Dodoma, ambayo
inapigwa vita na kundi la wengi kwa nguvu zao zote (na hata ikibidi wako
tayari
kuingia msituni kutetea serikali 2). Sura zifuatazo zinadhihirisha gharama
hizi:

USHAHIDI
WA KWANZA
Sura
ya saba, ibara ya 98(2). Kifungu hiki kinasomeka ifuatavyo:

"Kwa
madhumuni ya ibara ndogo ya 98(1), idadi ya mawaziri na manaibu waziri wa
serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitazidi 15". Mwisho wa kunukuu.

Idadi
ya mawaziri na manaibu waziri katika serikali ya sasa ni zaidi ya 60! Kila
waziri
analipwa mshahara (excluding gharama za nyumba, gari, mafuta, safari na
anasa
zingine) wa Tsh 20,000,000. Jumla ya mshahara kwa mawaziri 60 wa serikali 2
ni
Tsh 20,000,000×60= 1,200,000,000. Hizi ni Tsh 1.2 billion (sawa na Tsh 14.4
bilion kwa mwaka).

Mshahara
wa mawaziri 15 wanaopendekezwa katika serikali 3 ni Tsh
20,000,000×15=300,000,000.
Hizi ni Tsh million 300 (sawa na Tsh 3.6 billion).

Kwa
hivyo mtaona kwamba gharama ya kuendesha mawaziri 15 wa serikali 3 ni
rahisi
kwa Tsh billion 10.8 sawa na 75%. Haya, sasa wale mnaodai kwamba serikali 3
ni
ghali huwa mnatumia kigezo gani? Msidhani kila mtanzania ni zuzu. Mnaposema
ughali
au urahsi sharti muoneshe mnakokotoaje hizo gharama, sio watu
wanakaririshwa
majibu kwenye vikao halafu wanakuja kupayuka hadharani bila takwimu. Huo ni
ujuha!

USHAHIDI
WA PILI
Kwa
mujibu wa rasimu ya katiba ibara ya 113(1) na (2) idadi ya wabunge
inayopendekezwa kwenye rasimu ni wabunge 70 wa kuchaguliwa (50 kutoka
Tanganyika
na 20 kutoka Zanzibar) na 5 walemavu watakaoteuliwa na rais. Hawa ni sawa na
jumla
ya wabunge 75. Bunge la sasa lina jumla ya wabunge 389 wa kuchaguliwa na 10
wa
kuteuliwa, sawa na wabunge 399. Kila mbunge hulipwa Tsh 11,000,000
(+5,000,000
za jimbo)=16,000,000. Wabunge wote 399 wanalipwa jumla ya Tsh
399×16,000,000=6,384,000,000
(sawa na billion 6.4). Gharama ya wabunge hawa kwa mwaka ni Tsh 76.4
bilion.

Gharama
kwa wabunge 75 wa serikali 3 ni Tsh 16,000,000×75=1,200,000,000(sawa na Tsh
14.4 bilion kwa mwaka).
Tofauti
ya gharama za kuendesha bunge la serikali 2 ukilinganisha na bunge la
seriakli
3 ni Tsh 62 bilion. Sasa hawa waongo wanaosema kwamba kuendesha serikali 3
ni
ghali wanatumia kigezo kipi hawa vilaza?

KUMBUKA:
Ukokotozi
wa gharama uliofanywa hapo juu haujumuishi gharama za mishahara,
marupurupu,
mafuta, safari, anasa, nk za makatibu wakuu, makamishina, wakurugenzi na
wakuu
wa idara katika wizara husika. Ukijumlisha na gharama za kuwalipa viongozi
hawa
pesa zitakuwa nyingi zaidi ya mara mbili ya hizo zilizokotolewa hapo juu.
Huu ushahidi
unatosha kabisa kuonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuliko serikali 2. Kwa
hiyo,
ule uongo mnaoambiwa na wanasiasa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2
mnapaswa
kuupuuzilia mbali. Wanakudanganyeni kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa ili
waendelee kukukandamizeni, kukumasikinisha na kukuchukulieni kama mazuzu wa
kupandia ngazi za madaraka na kujichumia mali kwa ajili ya matumbo yao
binafsi.


TAHADHARI
Kwa
upande mwingine, ifungu hivyo nilivyonukuu hapo juu ni mwiba mkali kwa CCM
kwani vinawanyima uhuru wa kujitungia wizara na kuwapa uwaziri makada wao
kama
zawadi kwa kazi nzuri ya kukitumikia chama. Wanapenda tuendelee na mfumo
ghali
wa serikali 2 ili wananchi waendelee kubebeshwa gharama za kuendesha
serikali
kwa manufaa yao binafsi. Mwenye macho haambiwa tazama. Kila mtanzania
anapaswa
kufunguka macho na kuhoji hizo gharama wanazodai wanazikokotoa kwa kutumia
kigezo kipi. Sio mtu unakaririshwa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2
unakubali tu kama zuzu. Unatakiwa kuhoji. Ujinga wa watanzania kutohoji
mambo ndio
unaosababisha wanasiasa waendelee kutudanganya na kutufanya ngazi za
kupandia
na kuning'inia madarakani kwa manufaa yao binafsi.


N.B
Uchambuzi
zaidi kuhusu gharama kubwa za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na serikali
3
utafuata baadaye. Nataka wale waongo wanaowadanganya raia kwamba serikali 3
ni
ghali kuliko 2 waumbuke mchana kweupe.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com


For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups
"Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit
https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/1398266789.47389.YahooMailNeo%40web163103.mail.bf1.yahoo.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--
mission without implementation is hallucination

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment