Unakataa matusi kwa kutukana wenzako kwa kuwa bwana wako unamuona bora zaidi kuliko wa wenzako. Nani kakupa jeuri hiyo ya kutukana wenzio kama si ulevi wa madaraka aliyokupa bwana wako? Sisi sote ni Watanzania wa Tanganyika na Zanzibar tueshimiane. Anapokosea mwenzetu tumwambie umekosea kwa staha na si kwa matusi. Najua unapata jeuri kwa kuwa mmetengeneza tabaka la watwana na waungwana ambamo mtoto wa muungwana ndiye atarithi madaraka ya baba yake. Kama wewe ni muungwana omba radhi ila kama ni mlevi nyamaza kwa jeuri
--------------------------------------------
On Mon, 4/21/14, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] NILICHOONGEA NA WAANDISHI WA HABARI LEO JUMATATU 21/4/2014
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, April 21, 2014, 4:51 AM
NILICHOONGEA
NA WAANDISHI WA HABARI LEO JUMATATU 21/4/2014Leo
Nitatumia maneno makali kidogo ili tuelewane kiurahisi.
Wapinzani wa Nchi hii ni "BAPHOON". Maana ya
BAPHOON ni Watu au Kundi la Watu linalotumika Kwa Maslahi ya
Mataifa Mengine Kuangamiza Taifa Lao. Wako Tayari Hata
Kuchukua Mabomu na kulipua Nchi yao Wenyewe. Hawa ndio
wanaojiita UKAWA (THE BAPHOON)Imani
namba Tano na namba nane za Chama Cha Mapinduzi kwa pamoja
zinasema:Cheo
ni Dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa
faida yangu na Nitasema Kweli Daima Fitna kwangu
Mwiko.Kwa
tafsiri ya Imani ya Chama tunakubaliana na maneno ya
Mwanahistoria wa zamani wa Uingereza Lord Acton aliyewahi
kusema;"Power
tends to Corrupt, and absolute power corrupts absolutely.
Great men are almost always bad men"Yakimaanisha
kuwa;"Madaraka
yana tabia ya kuwaharibu walio nayo, na wenye madaraka
makubwa Zaidi huharibika Zaidi kwa kuwa hata watu wema
hugeuka kuwa wabaya wakishakuwa na madaraka"Na
sisi Vijana Wazalendo tunasema;
"Watu wenye Madaraka Makubwa Wakiharibiwa na hayo madaraka
hulewa hayo madaraka na kuanza hata kutukana kudharau
waliowapa madaraka hayo. Lakini wenye madaraka makubwa
wanaojua kuwa madaraka yao ni dhamana, kwanza huwa wapore na
wanyenyekevu na hubeba dhamana kubwa ambayo wao huona
madaraka hayo ni Mzigo wala si zawadi."Wapo
wanaodhani kuwa Vyama vya Upinzani vipo kwa ajili ya Maslahi
ya Taifa. Wapo wanaodhani Vyama vya Upinzani ndio mkombozi
wao. Na wapo wanaodhani muarobaini wa matatizo ya taifa hili
ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ni vyama vya Upinzani.
Ukweli halisi wamepotoka sana. Vyama vya Upinzani vipo kwa
maslahi yao tu na vimekuwa ni dhaifu kiasi haviwezi
kuaminiwa kupewa dhamana ya Uongozi wa Taifa hili.Hatuna
haja ya kuwaambia BAVICHA waombe radhi kwa matamshi yao
yasiyo na adabu waliyoyatamka jana dhidi ya Rais wa Jamhuri
na Waziri Mkuu kwa sababu tunajua wanadhani wako sahihi.
Lakini tunajua wanajua hawako sahihi na wanafanya hivyo ili
kuwaridhisha mabwana zao ambao wanawatumia wao kutengeneza
mitaji yao kisiasa. Wao wanabaki tu kama kigenge fulani
ambacho kama kikiachwa kikue na uwongo wake mwishowe
kitaaminiwa na hapana shaka nchi hii ipo siku itaongozwa na
Vichaa.Tuelewe
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ndiyo Lulu pekee
iliyobaki Afrika ambayo imeundwa na sisi wenyewe , kwa hiari
yetu wenyewe baada ya kukomboa sehemu zake mbili kutoka
katika Ukoloni. Haiwezekani tuache Muungane uchezewe tu na
wachache wetu ambao kinachowasukuma ni Uroho tu wa
madaraka.Tulipoanzisha
Mfumo wa Vyama vingi, tulidhamiria kuwa na vyama vyenye
nguvu za dhati ambazo ama zingekuwa kubwa kuliko CCM ili
kuweza kuiwajibisha serikali sawasawa nayo iwajibike moja
kwa moja kwa ujenzi wa taifa. Miaka 21 baada ya kuwa na
mfumo wa vyama vingi, tumekuwa na vyama legelege ambavyo
havina dira wala mwelekeo badala yake vimejikita katika
uchochezi na ulaghai. Hali hii inatupa wasiwasi kama kweli
hivi ni vyama vya siasa ama ni vikundi tu vya harakati
vinavyofanya siasa. Watanzania wako tayari kuamini Upinzani
lakini si kwa miaka hii ya karibuni,ni mpaka tutakapopata
vyama vyenye nia thabiti ya kuleta maendeleo ya nchi hii
huku vikithibitisha kwamba vitadumisha muungano wa nchi
mbili serikali mbili na kuheshimu Katiba ya Nchi.Chama
Cha Mapinduzi kinabaki Imara na Msimamo thabiti wa Kuendelea
na Jamhuri Muungano wa nchi mbili na Serikali Mbili. Azimio
la kutaka serikali tatu si mara ya kwanza sasa. Azimio kama
hili lilikuwepo Mwaka 1993 kwa hoja Binafsi ya Wabunge 55
(G55) iliyopelekwa na Mh. Njelu Kasaka Mbunge wa Chunya. Kwa
kikao Cha Bunge cha August 24-27, Bunge liliridhia mchakato
wa kuanzisha serikali ya Tanganyika. Lakini kwa Uthabiti wa
CCM ambao ni imara sana sasa kuliko mwaka 1993, kilisimamia
mfumo wa kubaki na Muungano wa Nchi mbili na Serikali Mbili.
Msimamo wa CCM wa Mwaka 1993 ni thabiti sana sasa, hatuwezi
kufufua Tanganyika isipokuwa tutatumia mfumo uliopo kutatua
kero za Muungano zilizopo. Changamoto kubwa zinazotukabili
ni za kiuchumi kuliko zilivyo za kijamii na muungano wetu
sana una nia thabiti ya kijamii kuliko uchumi.Demokrasia
imechukua njia hadi sasa hata mifumo ya demokrasia imeanza
kupuuzwa. Nasema inapuuzwa kwa sababu hata Vichaa sasa
wanaweza kuamka tu na kutoa matamko yasiyo na kichwa wala
Miguu. BAVICHA ni Vijana wadogo sana ambao hawawezi kuamka
na kutoa matamko waliyoyatoa ila kwa kutumwa na Bwana zao.
Na hao Bwana zao wanafadhiliwa na Mataifa ya nje ambay
hayataki kuona siku moja AFrika inaungana na kuwa taifa moja
kubwa. Namna pekee ya kufanikisha uovu huo mkubwa dhidi ya
Afrika, ni kuibomoa Tanzania, na wenzetu hawa wapinzani
wamekubali kutumika kama vibaraka wa kudidimiza
Afrika.Hatuoni
Sababu ya Kukaa Kimya, Sitanyamaza kufumbia macho Ujinga
huu. Nani kawatuma BAVICHA kutoa Matamko dhidi ya Rais na
Waziri Mkuu? Nani kawadanganya kuwa eti Mchakato wanaoutaka
UKAWA ndio Mchakato wanaoutaka Wananchi?Unamsikiliza
Mh. Lipumba, amejawa maneno kinywani mwake ya uchochezi tu
wa kidini na ubaguzi wa wazi kabisa. Hizo zote ni hila
ambazo kama zisipodhibitiwa kwa kuelezwa ukweli wake kama
hivi, taifa litaangamia. Tumedhamiria kupambana na hili,
hatutakaa kimya Mpaka watanzania watuelewe na wawapuuze
wapinzani kwa lugha zao za uchochezi.Kwa
Nini wakatake kufanyia Mkutano Zanzibar kibanda Maiti na Si
Dodoma maana wote walikuwepo hapa? Hivi wapi ni Karibu,
Iramba kwa Tundu Lisu au Zanzibar (Unguja Kibanda Maiti)?
kuna Umbali gani Hai kwa Mbowe au Tabora kwa Lipumba au
Vunjo kwa Mbatia ukilinganisha na Zanzibar? Hawa waheshimiwa
wasitake kulaghai Umma, kuna ajenda wameibeba ambayo
hawataki kuisema. Warudi Bungeni waje wajenge hoja maana
Katiba haitapatikana Majukwaani bali kwa kukamilisha
Mchakato Bungeni na ndicho CCM tutakachofanya. Tunaendelea
na Bunge na tunakamilisha Mchakato hata wasiporudi.Ikiwa
wao ni vyama vya kidemokrasia na nia yao ni kujenga
demokrasia, kwa nini hawataki kukaa meza ya Mazungumzo? kwa
nini wakimbie mkutano halali wa kidemokrasia wasikae hapo
wajenge hoja hapo badala yake wanakimbilia eti kwenye
mikutano ya hadhara? Hapo kuna walakini na demokrasia
wanayohubiri. Anayehubiri demokrasia lazima awe wa kwanza
kukaa meza ya mazungumzo. Mumewasikia wakitoa matamko kwamba
hawako tayari kukaa meza ya mazungumzo na serikali wala CCM,
hawa ni washari na wanatangaza shari na kisha wanatafuta
huruma ya wananchi. Hiyo siyo demokrasia ni Vurugu. Uhuru
bila mipaka i vurugu na Demokrasia bila Utaratibu nayo ni
vurugu.Tunazo
tetesi kuwa hivi vyama vinafadhiliwa na wasiotaka kuiona
Afrika ikiungana na kuwa jumuiya moja kubwa yenye nguvu.
wanatafuta ucku na Mchana kuisambaratisha Afrika na namna
pekee ye kuisambaratisha Afrika ni kuisambarataisha Tanzania
kwa maana Tanzania ndiyo kinara wa Umoja wa Afrika. Kutumiwa
kwao na Ukibaraka wao uendelee lakini tuko imara sana
kulinda Muungano wetu. Hawa ni BAPHOON.Lugha
za kichochezi za wapinzani wananchi wamezisikia. Wamemsikia
Prof. Ibrahim Lipumba akiweka matabaka ya watu kwa sababu za
Kidini, wamemsikia Tundu Lisu akipandikiza chuki dhidi ya
Mwalimu Nyerere na waasisi wa Muungano, Mumewasikia viongozi
wa CUF, NCCR Mageuzi, wakifanya juhudi za kufitinisha
watanzania kwa kauli zao ovu. Ufitini wa aina yoyote, uwe wa
kidini, kikanda, kikabila au haiba ya watu hauna budi
kupigwa vita kubwa na kila Mtanzania mpenda amani.Wakumbuke,
Chuki wanazozijenga sasa, itafika mahali zitakomaa na
zikishakomaa zitaanza kuwa mwiba mkali kwao wao wenyewe. Kwa
maana wakifanikiwa kupanda mbegu ya chuki miongoni mwa
watanzania kwa namna yoyote ile, hakuna namna ambayo hao
waliowapandikiza chuki watawapenda wao. Chuki yao itawala
wao wenyewe na itaangamiza taifa. Hatuwezi kuacha hili
litokee tukiangalia kwa macho yetu.Taifa
halitajengwa na watu waoga wala waongo na wafitini.
Watanzania wenzangu tujikite katika kujenga uchumi na
kujiletea maendeleo kwani tukiendelea kuwasikiliza
"BAPHOON" hawa na kuacha shughuli zetu za
kiuchumi, ni kujipotezea fursa tulizo nazo kwa faida ya
wengine. Hawa wanawasumbua nyie mwasikilize, wao shughuli
zao za NIGHT CLUBS, GUEST HOUSE ZAO, BAR ZAO, CASINO ZAO,
DALADALA ZAO, MAHOTEL, na BIASHARA ZAO NYINGINE zinaendelea
kuwaingizia Pesa na wanachofanya ni kuwajaza matumaini ya
uwongo huku wao wanajaa MAPESA. Kwa kuwa wameamua kutumika
na mataifa ya nje kuhujumu nchi yao, bado wanalipwa kwa kazi
yao ya UFITINI. Mapato yao hayayumbi na wala
hayatayumba.Ewe
Mtanzania Mwenzangu, Shtuka, Achana na BAPHOON.Mungu
Ibariki TanzaniaPaul
C. Makonda
Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM
Mjumbe Bunge Maalum la Katiba
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment