Tuesday, 22 April 2014

Re: [wanabidii] NANI ANADANGANYA WATU ATI TANGANYIKA NI HARAMU NA HAIPO NA HAITAKIWI?

Wanaoibeza tanganyika na kusema hawaijui wanahitaji kuwauliza swali moja Jina lako la Ubin unaitwa nani? jina hilo mwenye nalo unamfahamu? Mimi naitwa Muhingo kama jina la Ubini. jina hilo ni la babu yangu. alikufa miaka hamsini kabla sijazaliwa. najisikia fahari kulitumia na sioni aibu. Wala sikusudii kulibadili. Huyo muacha asili asiyetaka kuijua Tanganinyika ana matatizo.

On Tuesday, April 22, 2014 10:34 AM, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
Napata tabu sana ninaposikia mtu anatoa hoja kwamba eti yeye kazaliwa Tanzania na wala haijui Tanganyika. Najiuliza swali, ina maana kuna wajumbe wa bunge maalumu la katiba ambao hawajasoma angalau kufikia darasa la saba?Na hata ingekuwa hajamaliza darasa la saba basi anaishi na watu na kwa vyovyote vile amewahi kusikia habari ya Tanganyika.

Kama anajua kusoma na pengine kasahau angepitia kwenye vitabu au kuuliza watu Tanganyika ni kitu gani. Watu wa namna hii wanajifanya wanamuenzi baba wa taifa wakati ni matapeli. Kama mtu anajifanya hajui historia ya nchi yake basi hata huyo baba wa taifa hamjui na anaviambia vizazi vijavyo kwamba yote yaliyofanyika kipindi hawajazaliwa ikiwemo mambo aliyoyafanya baba wa taifa hayana sababu ya kuyajua wala kuyathamini. Such people are contradicting themselves na dawa pekee ni kuwapuuza kwa sababu ni wapuuzi na wanafiki. Mara sijui Tanganyika imetokana na nini, kwani walitaka itokane na nini ili waitambue? Kama hawataki kuitambua Tanganyika basi wajitambue kutoka kwenye mikoa, wilaya, kata au makabila yao. Tanganyika is just a geographical location as it is for Zanzibar. Je hiyo Zanzibar wanayoitambua kama nchi  wanaijua maana yake? Siyo vyema kutufanya wajinga kiasi hicho, watambue tuna akili kama walivyo wao. Waje na sababu zenye mashiko siyo hizi za kitoto

Kama si unafiki basi nilitegemea mtu anayetwambia serikali tatu ni gharama apendekeze muundo wa serikali moja ambao utatufanya tuwe kitu kimoja kuliko ilivyo sasa. Lakini kwa kuwa ni wanafiki na waroho wa madaraka basi utasikia muundo wa serikali tatu utatugawa, utavunja muungano na maneno mengine yasiyokuwa na mashiko kama hayo. Binafsi ni muumini wa serikali moja kama alivyopendekeza Zitto. Kwa kiasi fulani naweza kuwaunga mkono wanaopropose muundo wa serikali tatu kwa vile si wanafiki kama hao wanaosema mbili.

Wanaosema mbili ningependa watueleze sababu zenye mashiko kwa nini wanairuka moja na kukimbila mbili? Rasimu inayotoka kwa wananchi inasema tatu na hivyo tulitegemea wachambue vyanzo vya mapato, gharama na mengineyo ili tupime wenyewe. Siyo kusimama na kutuimbia wimbo uleule aliotuimbia mwenye kaya siku alipoamua kutoa maoni yake baada ya muda wa kukusanya maoni kupita.

Ebu watueleze sababu za kutopendekeza muundo wa serikali moja na badala yake wanakimbilia mbili. Kama kuna woga wa kushindwa kuwaambia Wazanzibari kwamba tunataka tuungane tuwe kitu kimoja ina maana wanatambua ugumu wa kuwa na muundo wa serikali moja ila kwa unafiki wanajifanya sisi ni wamoja wakati wakijua sisi si wamoja (all animals are equal but others are more equal). Sisi na wazanzibari ni wamoja lakini si wamoja kabisa na ndiyo sababu ya woga huo. Kama si wamoja kabisa na kwamba muundo wa serikali moja haukubaliki kwa wazanzibari ya nini kulazimisha muundo wa serikali mbili badala ya tatu? Namalizia kwa kusema muundo wa serikali moja ndo muundo sahihi kwangu ila kama wengi wanasema muundo uwe wa serikali tatu nitalazimika kuwaunga mkono. Wanaosema mbili naamini kuna jambo wanalificha na si watu wa kuunga mkono ni POWER MONGERS.


On Tue, Apr 22, 2014 at 6:56 AM, Fred Hans Kipamila <fhkipamila@yahoo.com> wrote:
Hilo la serikali 1 limeshindikana toka enzi za Nyerere tufanyeje sasa? Lete hoja mbadala
--------------------------------------------
On Mon, 4/21/14, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:

 Subject: Re: [wanabidii] NANI ANADANGANYA WATU ATI TANGANYIKA NI HARAMU NA HAIPO NA HAITAKIWI?
 To: wanabidii@googlegroups.com
 Date: Monday, April 21, 2014, 2:25 AM

 Thamani, umoja, utu, upendo na
 amani yetu watanzania haitaletwa na idadi ya serikali. Ziwe
 2, 3 hata 4, kama kweli tunapendana na kutakiana mazuri
 hapana budi kuwa na serikali 1 tu baada ya kurekebisha
 kasoro za mfumo wa muungano wa sasa.


 Hakuna dawa nyingine ya kuimarisha muungano isipokuwa
 kuungana. Kuongeza serikali ya 3 ni kuzidi kuumegua na
 kuuvunja zaidi!!!
 "...by citizenship am a Tanzanian,
 nationality African..."



 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment