Thursday, 10 April 2014

Re: [wanabidii] Katiba Mpya: Nimeitafakari Sana Njia Ya Kikwete...

sawa kabisa
On Thursday, April 10, 2014 11:16 AM, flano mambo <flein47@yahoo.com> wrote:
Mjengwa Kaka yangu sisi ndo tunaumia kwa hisia nyingi. Jambo hili nakumbuka niliwahi kuwaandikia Mh Tundu Lisu na Mh. John Mnyika mapema kabisa suala la katiba mpya lilipoanza kusikika. Niliona bila shaka mwaka 2015 hatutotumia katiba mpya kwa sababu  nilihisi kama wenzetu watataka mahakama ya kadhi iinginzwe kwenye katiba itahitaji muda kuliweka jambo hilo vizuri ili kuwe na maridhiano lakini ZITO kuliko ilikua ni suala la muungano.

Niwajuavyo mimi Wazanzibari hawatarudi nyuma baada ya kurekebisha katiba yao isivyo halali kutengeneza nchi ndani ya nchi. Na nijuavyo mimi naomba nirekebishwe kama nakosea. Marekebisho ya 10 ya katiba ya zanzibar ya mwaka 2010 yaliyoipa zanzibar hadhi ya nchi yalisimamiwa si na UAMSHO hapana ni viongozi halali wa zanzibar akiwemo Mheshimiwa Aman Abeid Karume. Na wakati mambo hayo yanafanyika wote tulikua mashahidi viongozi wetu wakuu akiwemo Mheshimiwa raisi wetu alikaa kimya. Labda mwenzenu kumbukumbu zangu ndogo mie sikumbuki kama kuna siku JK alilitolea tamko sakata la mabadiliko ya katiba ya zanzibar. Kwa hiyo kwa ukimya ule its like naye alikubaliana na mchezo ule na akaubariki JAPO ALIAPA KUILINDA NA KUITETEA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAMANI.

Sasa ni haki kweli leo hii tuanze kuwaona wazanzibari ati wahaini wakati wanafanya mchezo viongozi wakuu wa jamuhuri walikaa kimya? kwani ilikua siri?

Tume ya warioba iliweka wazi mambo yaliyokuwa hayaeleweki kwa wengi tunajua kabisa kuwa 
1. Wenzetu wanakerwa na muundo uliopo
2. Hawako tayari kurudi nyuma. Ikiwa serikali 2 kwao imekua kero je wako tayari kukubali serikali1 ambayo wasomi wanaitaka? je wako tayari kushawishiwa kuwa tuwe na serikali 2 zilizoboreshwa wakatuelewa? hapo kuna kazi.

3. Hata hawa wazee wa zanzibar wanaopinga serikali 3 nisameheni mwenzenu nawaona wanafiki kwasababu mbona hawakupinga marekebisho ya katiba ya zanzibar kwani hawakujua athari zake?
Ona baadhi ya viongozi wa zanzibar wanapinga serikali3 kwa nguvu lakini walikua kimya kwenye marekebisho ya katiba yao ilhali walijua walichokua wanataka. HAPA JAMANI wenzetu wanafanya kaunafiki fulani. mi napenda wawe wawazi maana siku zote wametulalamikia sana wabara, imefika hatua hata wabara walioko unguja wamekua wanapata changamoto kweli mara maduka yamechomwa moto mara tindikali mara risasi. Baadhi wenzetu wamefika hatua wametujengea chuki kana kwamba sisi ni kikwazo kwa maendeleo yao.

JE MJENGWA UNADHANI KUNA MARIDHIANO YA DHATI KUWA NA SERIKALI2?? HAPO UTAFANYIKA USANII TU
On Thursday, April 10, 2014 10:25 AM, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:


Ndugu zangu,

Naziona ishara za kuendelea kwa mvumo mbaya wa upepo wa kisiasa na hususan inapohusu hoja ya Muungano na muundo wa Serikali.

Mjadala unaoendelea sasa ni kama vile umefunikwa kwa chandarua kisicho na kinga ya wadudu wenye madhara kama mbu.

Tunakoelekea si kuzuri. Msimamo wangu uko wazi, kuwa tunahitaji muundo wa Serikali Tatu ili tuimarishe Muungano wetu. Kwamba tunahitaji uwepo wa Tanganyika kama nchi.

Lakini, nahofia katika tofauti hizi za mitazamo, kuna wenye kuamini katika Serikali Tatu lakini bila kuwa na nia njema kwa nchi. Na kuna wenye kuamini hivyo wakiwa na dhamira njema pia. Hivyo hivyo kwa wenye kuamini katika Serikali Mbili.

Hivyo, nimeipitia mara kadhaa hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa alipokuwa akifungua Bunge Maalum la Katiba. Nimejitahidi kuitafuta mantiki kwa alichokizungumza Rais wa Nchi. Naamini Jakaya Kikwete aliongea kile alichokiamini moyoni mwake. Kikwete alionyesha hofu juu ya Serikali Tatu ingawa aliweka wazi kuwa maamuzi ya mwisho ni ya Wabunge wenyewe. Ni haki ya Kikwete kama mwanadamu kuelezea hisia zake.

Lakini , Jakaya Kikwete si kama Watanzania wengine. Ni Rais wa Nchi. Nikifikiri leo, naamini ilikuwa sahihi kwa Kikwete kukisema alichokisema, hata kama hakifanani na misimamo kama ya kwangu.

Maana, nikiwasikiliza ndugu zetu wa Zanzibar , hasa wenye kuupinga Muungano katika hali iliyopo, na jinsi wanavyojadili, kwa kweli natishikia pia. Na hakika, kwa kuufuatilia mvumo wa upepo wa kisiasa unaoendelea sasa, Jakaya Kikwete alitusaidia kuyaweka wazi mawazo yake binafsi. Maana, ingawa Serikali Tatu na Tanganyika inahitajika, lakini, huu si wakati wake. Ni jambo la kusubiri lije tutakapokuwa tayari kama watu tulioungana; Visiwani na Bara. Na tuanze sasa kufanya jitihada za kuyatafuta maridhiano juu ya kwa nini haya ya kubadilli mfumo wa Serikali kwenda Serikali Tatu wakati wake haujafika.

Maana, kuendelea kujadili Serikali Tatu sasa ni kuzidi kuipeleka nchi yetu tunayoipenda kwenye mgawanyiko na mpasuko mkubwa. Ni busara nionavyo, kuwa Wabunge wetu kule Dodoma watambue kuwa rasimu ya Jaji Warioba, ukiacha muundo wa Muungano na mfumo wa Serikali , ina mengi sana ya muhimu ili kututoa hapa tulipo na kuwasaidia wananchi.

Waitafute busara ya kulisubirisha hili la Muuundo wa Muungano unaopendekezwa na Rasimu ya Warioba na hata muundo wa Serikali. Tubaki na Serikali Mbili na tuboreshe kinachoweza kuboreshwa.

Maana, si kila unachokigawa maana yake kuna kinachobaki. Kugawa pia kuna maana ya kumaliza pia.

Na mengine tuyafanyao katika wakati usio sahihi huzaa kutokuaminiana.
Na kwa mwanadamu pale mtaji wa imani unapomalizika, kinachobakia ni kumaliziana.

Usimwone nyani ana makovu ukadhani ni simba aliyemjeruhi. Nyani huishi kwa kumwogopa zaidi nyani mwenziwe.

Kugawanyika kwa shari ni kutawanya mitaji ya kuaminiana.
Na kitachobaki ni kuumizana, kwa kugombani kiduchu chunguni kilichogandiana…

Ni wakati sasa wa kutanguliza busara na hekima zitakazotunusuru na mpasuko mkubwa zaidi wa kijamii.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

Maggid,
Iringa.
http://mjengwablog.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.




0 comments:

Post a Comment