Tuesday, 22 April 2014

Re: [wanabidii] BUNGE LA KATIBA NI " KOMEDI" ?

Ni;ianza kwa kushangaa, watawala walipoanza kutukana viongozi wa tume badala hoja zilizomo. Nimeona siasa za kizanzibar zikianza kuchomoza na kudakwa na wabara.
Namshukuru dr Migiro nilimwona akikwepa kujadili kwa mtindo huwo.
Kwakuwa picha zinachukuliwa watoto na wajukuu zetu watahukumu kwa hilo.
--------------------------------------------
On Tue, 4/22/14, 'ananilea nkya <ananilea_nkya@yahoo.com>' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] BUNGE LA KATIBA NI " KOMEDI" ?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, April 22, 2014, 10:48 PM

Historia 
itahukumu  watawala  wetu -wanawake na
wanaume  kwa kusambaza sumu ya maneno ya kulipasua
taifa letu vipande vipande.
Tusubiri.   Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
On Saturday, April
19, 2014 1:42 PM, Happiness Katabazi
<katabazihappy@yahoo.com> wrote:
BUNGE LA KATIBA NI
" KOMEDI" ?

Na Happiness Katabazi
HAKUNA Ubishi kuwa siku hizi ukitaka kucheka, kukereka na
kupunguza msongo wa mawazo uliyonayo, ukitaka kujifunza
maneno machafu mapya, huna budi kufungulia Televisheni ya
Taifa (TBC1), na kuanza kuangalia mijadala ya Bunge la
Katiba la Tanzania linavyoendeshwa na jinsi wajumbe wa bunge
hilo wanavyochangia kwa kutumia lugha za matusi,
zisizonastaa na zinazopolomosha heshima ya bunge hilo na
jamii yetu ya Tanzania.

Na Baadhi wananchi wengine wamekuwa wakisema uenda kabla ya
bunge hilo
kuanza , baadhi ya wajumbe wanakunywa kwanza 'viroba'
ndiyo wanaingia ndani ya bunge na kuanza kuchangia mjadala
kwa kutoa lugha za kejeli, uzushi, kuzomea na kugonga meza
ovyo.

Nimeyasema hayo kwasababu tayari baadhi ya wananchi wameisha
lipachika bunge la Katiba kuwa ni 'Komedi'. Kwa wajumbe
wa bunge hilo ambao ni watu wazima wenye umri wa zaidi ya
miaka 18 , baadhi yao wameshindwa kujiheshimu na kuchunga
kauli zao wakati wakichangia mjadala wa mchakato wa kupata
Katiba Mpya

Kila kukicha tumesikia wabunge hao wengine wakiwa na umri
mdogo wamekuwa wakiwatolea maneno ya 'shombo' wajumbe
wenzao ambao wamewazidi umri kwa kisingizio kuwa wajumbe hao
wenye umri unaowazidi na kuwapita hata wazazi hao wamekuwa
wakilidanganya bunge, na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo
ambao wanaumri mkubwa nao wamekuwa wakiwatolea maneno
yasiyofahaa wajumbe wenzao wenye umri mdogo wachangiapo
mjadala huo.

Mila na tamaduni zetu ni mkubwa
anamheshimu mdogo na mdogo anamheshimu mkubwa lakini
kupitia bunge letu la Katib a'Komedi', niwazi wajumbe wa
bunge hilo wanauzika utamaduni huo na kufanya sasa jamii ya
watanzania waanze kuishi kwa kutumia utawawa Kambare kwani
baba,mama ,mtoto wa kambare wote wanandevu hakuna wa
kumbabaisha mwenzie.

Nia ya Rais Jakaya Kikwete ya kutaka Tanzania iandike Katiba
mpya ni njema, ila sasa tunashuhudia baadhi ya wajumbe wa
bunge hilo hawataki nia hiyo ikamilike kwa kila siku kuibua
mapingamizi na hoja zisizokuwa na kichwa wa miguu hali
inayosababisha hivi sasa  heshima ya bunge hilo
kuporomoka na kuona ni kheri tubakie na Katiba ya zamani ya
mwaka 1977 licha ina mapungufu yake kuliko kuletewa Katiba
mpya ambayo inaendelea kuandikwa na baadhi ya wajumbe
waliokosa adabu, wanatumia lugha za matusi, uzushi kwa
kisingizio kuwa eti wanataka serikali mbili wengine wanataka
serikali tatu.

Kwa wale tuliopata kuisoma rasimu ya pili ya Katiba,
mtakubaliana na mimi rasimu hiyo imeandikwa vitu vingi sana
siyo Muungo wa Serikali mbili, Serikali tatu, wala hati ya
Muungano pekee.Imeandikwa vitu vingi lakini hatuoni kama
baadhi ya wajumbe wanajipa muda wa kuisoma rasmi hiyo yote
na kufahamu kilichoandikwa.

Leo hii baadhi ya wajumbe wanaibuka wanasema hati za
Muungano mara zimegushiwa, mara hazipo kwa sababu hiyo
hakuna muungano.Na mbaya zaidi wanaongea uzushi ndani ya
bunge hilo hawatoi vielelezo.Tuwaulize wajumbe wa aina hii
hivi siku hati za Muungano zilivyokuwa zinatengenezwa na
waliozitengeneza na zikasainiwa na Marehemu Baba wa Taifa
Julias Nyerere na Rais wa Zanzibar, Abeid Aman Karume
walikuwepo?

Mapema wiki hii  Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue
alifanya mkutano wake na waandishi wa habari na kuwaonyesha
hati za Muungano na kusema hati hiyo ni halisi na kwamba
Rais Jakaya Kikwete amesikitishwa na uzushi huo kwamba hati
hazipo, na lugha za kejeli na
matusi.

Minashangaa sana huyo Balozi Sefue anavyosema Rais Kikwete
eti amesikitishwa na vitendo hivyo.

Naye Rais Kikwete amenukuliwa juzi akisema kuwa anakerwa na
lugha za kejeli , matusi nakuwakejeri waasisi wa taifa
hili.

Ni najiuliza Kwa hiyo rais Kikwete akishasikitika ndiyo hao
wajumbe wazushi, wanaotoa lugha za kejeli ndiyo wataacha
tabia hiyo ambalo linaporomosha heshima ya bunge hilo mbele
ya jamii?

Kwa hiyo Rais Kikwete akisikitishwa na lugha hiyo za kejeli
zinazotolewa na Hao  baadhi ya wabunge la Katiba, ambao
watu tunaofikiri sawa sawa HIvi sasa kutokana na vitendo Vya
kishenzi na kijani  vinavyofanywa  ndani ya Bunge
na Hao wajumbe  HIvi huo mchakato wa kuwapata wajumbe
wale ulifanywa na watu wenye akili timamu  au wahuni
tu?

Maana aingii akilini kabisa kuna baadhi ya wajumbe ambao
tangu serikali hii iingie madarakani Desemba 21 mwaka 2005 ,
wamekuwa wakipinga kila kinachofanywa na
serikali hii kiwe kizuri au kibaya na wazushi wakubwa,
lakini cha ajabu Rais Kikwete akawateua baadhi ya wanasiasa
hao sijui akidhani kwa kuwateua ndio atawafurahisha na
wataacha kuzua uongo?

Matokeo yake wajumbe hao wenye tabia hiyo baada ya kufika
ndani ya bunge hilo ndiyo kwanza wameendelea na tabia zao ya
uzushi, kulazimisha mambo wanayoyataka wao tu na wanataka
watu wote waamini yale wanayoyaamini wao na kuzua taftari ma
maneno ya shombo ndani ya bunge jambo linalosababisha hivi
sasa heshima ya bunge hilo kuanza kuporomoka kwasababu ya
vitendo vya kiuni kufanywa na baadhi ya wajumbe ambao
wengine ni wateuli wa rais Kikwete.

Wahenga waliwahi Kusema " Mtoto umleavyo ndivyo
akuwavyo". Msemo huu umethibitika kwamba Katika Utawala
wa serikali awamu ya nne imekuwa ikiwa lea na wakiwa
kukumbatia baadhi ya wanasiasa na wanaharakati ambao
wamekuwa wakitoa maoni Yao kupitia vyombo Vya Habari,
mikutano ya adharani kuzulia uongo na kuwachafua
mahasimu wao kisiasa, vyama Vya siasa na wakati mwingine
serikali.

Sasa tabia hiyo chafu ya kuzua maneno ya uongo ndiyo
Imefikia mahali sasa wajumbe wa Bunge la Katiba kufikia
Hatua ya Kusema Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Mara imegushiwa Mara haipo wakati ipo.

Kwa hiyo tabia hii Chafu iliyoota mizizi sasa Kwenye vinywa
na Fikra Kwa baadhi ya wanasiasa wetu uchwara ya uzishi,
upotoshaji kwa kiasi kubwa nadiriki Kusema imelelewa na
kukumbatia sana na Utawala wa serikali awamu ya NNE ambayo
Katika Utawala awamu ya NNE ndiyo wanasiasa Wengi uchwara
hapa nchini ndiyo wamekuwa walitumia mbinu hiyo ya uzishi na
uongo Katika hotuba zao kuwadanganya wananchi Katika Mashaka
mbalimbali.

Na uthibitisho wa hili ni kitendo Cha baadhi ya wajumbe wa
Bunge Hilo kusimama ndani ya Bunge Kusema eti hati ya
Muungano haipo , wengine imegushiwa Kumbe hati hiyo ipo.

Mbona serikali hii imeishawahi kuyafungia baadhi ya magazeti
kwa kile
ilichodai kuwa magazeti hayo yamekuwa yakiandika habari
ambazo zinaleta uchochezi na uhasama katika jamii?.

Kwanini baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kwa ushabiki wao wa
kijinga tu wa kundi moja linataka serikali mbili jingine
linataka serikali tatu lifikie sehemu ya kufanya vitendo vya
kulidhalilisha bunge letu mbele ya walipa kodi?

Hata kama hati zilizotolewa na Balozi Sefue ni halisi au
zimegushiwa hao walisema hati za muungano hazipo na
zimeghushiwa  wanaweza kuzitambua? .Tukubaliane
kimsingi si kila nyaraka ya serikali inatakiwa kuwekwa
wazi.Nyaraka zingine hazistahili kuwekwa adharani.

Siku zote wananchi wataendelea kuzieheshimu na kuziogopa
mahakama licha mahakama zetu nyingi hazina mazingira mazuri
ya ofisi kwasababu mahakimu na majaji wanaoendesha kesi
wanajiheshimu wawapo mahakamani wakiendesha kesi.Wakati kesi
zikiendeshwa hutakuta mtu akipokea simu, wala kuchati wala
kupigana picha na kisha picha kuweka kwenye simu
wakati kesi zikiendelea.

Lakini hivi sasa tunashuhudia baadhi ya wajumbe wa bunge la
Katiba wakati bunge hilo likiendelea wakitumia Ipad na simu
zao kuchati na kupigana picha.Hivi tujiulize muda wa
kufuatilia kwa makini hoja zinazotolewa na wajumbe wenzao
wanaupata wapi?Maana muda wote wapo bize na simu?

Na nina mshangaa sana huyu Mwenyekiti wa Bunge la
Katiba,Samuel Sitta ambaye ni msomi wa sheria anashindwa
kupiga marufuku ufedhuli huu ambao nao  unaporomosha
heshima ya bunge hilo ambalo hivi sasa huku mitaani limepewa
jina la utani la 'Komedi'.

Kwa uhuni huu unaofanywa na baadhi ya wajumbe wa bunge la
Katiba wa kuibua hoja za uzushi, kejeli,matusi ambazo
zimesababisha baadhi ya wajumbe hao wamekosa adabu wanaacha
bila kuchukuliwa hatua, kunanifanya sasa nione ni kheri
tuendelee kutumia Katiba ya zamani ya mwaka 1977 ambayo ni
kweli ina mapungufu ambayo yanaweza kurekebishwa kuliko kuja
kutumia hiyo Katiba mpya
ambayo  inaendelea kutengenezwa na hawa baadhi wajumbe
ambao wakati wanaitengeneza walikuwa wakitumia lugha chafu
na uzushi.

Katiba Mpya sio itaji muhimu sana kama lilivyoitaji la
serikali kutoa hela kununua madawa mengi kuweka
mahospitalini, kujenga miundombinu,kutengeneza wodi za
kuzaliwa wa kinamama, kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa UTI
ambao hivi sasa umeanza kuwa tishio kubwa hapa nchini.

Kama kweli tunataka kutengeneza hiyo Katiba mpya, wale
wajumbe wa bunge hilo ambao kisheria sisi tunasema wao siyo
wa mwisho wa kutengeneza Katiba mpya ,wajiheshimu na
watimize jukumu lao hilo kwa nidhamu bila kuvunja heshima ya
bunge hilo na kupotosha jamii.

Ni ajabu sana wajumbe wa bunge la Katiba kutaka kuparurana
kuhusu mchakato wa kupata Katiba mpya, wakati sisi tuliosoma
somo la Katiba tumefundishwa kuna hatua kadhaa za kufikia
kutengeneza Katiba mpya. Hatua ya kwanza ni Tume kukusanya
maoni ya wananchi, tume kuyaweka kwenye maandishi
maoni hayo(rasimu), Bunge la Katiba kuijadili rasimu husika
kama bunge linavyofanya sasa, kisha yaliyojadiliwa na Bunge
yapelekwe kwa  kwa wananchi wayapigie kura za ndio au
hapana.

Sasa nyie wajumbe mnaotaka kuparulana kwa kisingizio cha
kutaka serikali mbili, mara tatu make mkijua bunge siyo
chombo cha mwisho ya kutengeneza Katiba mpya.

0716 774494
www.katabazihappy.blogspot.com
Aprili 19 Mwaka 2014.


Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence statements and facts must be presented responsibly.
Your continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment