Saturday, 11 January 2014

Re: [wanabidii] MATOKEO YA SENSA YA IDADI YA TEMBO WA SELOUS-MIKUMI NA RUAHA-RUNGWA

Hivi hamna namna ya kuvuna hizi pembe bila kuwauwa hawa tembo, huku kwetu tunawakata pembe ng'ombe wakorofi, sasa hawa tembo hatuwezi kuwakata pembe kwa ustaadi pasipo kuwauwa?

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, January 11, 2014 2:19:26 AM GMT-0800
Subject: Re: [wanabidii] MATOKEO YA SENSA YA IDADI YA TEMBO WA SELOUS-MIKUMI NA RUAHA-RUNGWA

TEMBO 2 WANAUAWA KILA SIKU SELOUS PEKE YAKE
TEMBO 96 WANAUAWA KILA SIKU DUNIANI,
TEMBO 35,000 WALIUAWA MWAKA 2012 PEKE YAKE,

Serikali isitishe mpango wake wa kuomba ruhusaa ya kuuza meno yote
yaliyokamatwa na badala yake yachomwe moto hadharani watanzania
wakishuhudia. Wahusika washughulikiwe vikali. Na hukumu zao zitangazwe
hadharani watanzania wote wajue. Kitendo cha kupata kibali na kuyauza
tutakuwa tumetumia njia nyingine ya kuwafikishia meno hayo watu ambao
wamechangia kufanya ushawishi wa kuua Tembo wetu. Marekani, Ufilipino na
China wameshaonesha mfano, Wameteketeza meno yaliyokamatwa

Aidha wakati huo huo Serikali ichukue hatua za haraka kuiwekea msimamo
mkali Serikali ya China kutokana na tatizo la wananchi wake kuhusika kwa
kiasi kikubwa kwa kushirikiana na wenyeji wasiolitakia mema taifa letu,
watu ambao hata hawastahili kuitwa Watanzania. China wako mahili sana
kukamta madawa ya kulevya lakini Meno ya tembo hatusikii watu kukamatwa,
kufungwa wala kunyongwa? Kwanini tusianze kuwa na wasiwasi na Serikali
yenyewe ya China?. Kwanini tusihisi hii choma choma waliyoifanya ni zuga tu?
Na kwa upande mwingine Serikali iendelee na opereshen tokomeza kwa nguvu
kubwa lakini wahusika wakizingatia sheria na haki za kibinadamu.

On Friday, January 10, 2014 8:40:02 PM UTC+3, vins wrote:
>
> Halafu baadaye tuanze kulia umaskini wakati tunafuja rasilimali zetu. Haya
> ni matokeo ya serikali legelege lakini inayotumia mabavu pasipo hitajika.
> On 10 Jan 2014 15:49, "Abdalah Hamis" <hami...@gmail.com <javascript:>>
> wrote:
>
>> *MATOKEO YA SENSA YA IDADI YA TEMBO KATIKA MFUMO WA IKOLOJIA WA
>> SELOUS-MIKUMI NA RUAHA-RUNGWA*
>>
>> Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuujulisha umma matokeo ya sensa
>> ya tembo iliyofanyika mwezi Oktoba na Novemba mwaka huu ili kuiwezesha
>> Serikali kutambua hali ya rasilimali ya wanyamapori ndani na nje ya maeneo
>> yaliyohifadhiwa.
>>
>> Wizara kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani na nje ya nchi imefanya
>> sensa katika Maeneo ya Mfumo ikolojia wa Selous – Mikumi na Ruaha – Rungwa
>> pekee kwa kuwa ni maeneo yenye tembo wengi nchini.
>>
>> Matokeo ya sensa hii yanaonyesha kwamba Mfumo wa ikolojia wa
>> Selous-Mikumi kwa sasa una tembo wapatao 13,084 na
>> Ruaha–Rungwa una tembo wapatao 20,090. Takwimu hizi zinaonesha kupungua
>> kwa idadi ya tembo na hasa katika mfumo ikolojia wa Selous-Mikumi
>> ikilinganishwa na Sensa za awali.
>>
>> Takwimu za muda mrefu zinaonesha kwamba mwaka 1976 katika mfumo ikolojia
>> wa Selous–Mikumi kulikuwa na tembo 109,419. Idadi hii ilipungua kufikia
>> 22,208 mwaka 1991 kutokana na wimbi la ujangili uliokuwepo katika kipindi
>> cha mwaka 1984 -1989. Hata hivyo, idadi hiyo iliongezeka na kufikia 70,406
>> mwaka 2006 baada ya Operesheni Uhai iliyofanyika mwaka 1989 na 1990 na
>> juhudi za kimataifa za uhifadhi ikiwemo kusitisha biashara ya meno ya tembo.
>>
>> Aidha, idadi ya tembo nchini ilipungua hadi kufikia jumla ya tembo 38,975
>> mwaka 2009 na kuendelea kupungua hadi kufikia tembo 13,084 hivi sasa.
>>
>> Hali kama hiyo inaonekana pia katika mfumo wa ikolojia wa Ruaha-Rungwa
>> ambapo sensa ya mwaka 1990 ilionesha kuwa na tembo 11,712 kutokana na wimbi
>> la ujangili. Idadi hii iliongezeka na kufikia 35,461 mwaka 2006. Hata
>> hivyo, idadi hiyo imepungua na kubakia tembo 20,090 hivi sasa.
>>
>> Kwa matokeo haya inaonesha kuwa katika mfumo ikolojia wa Selous-Mikumi
>> idadi ya tembo imepungua kwa asilimia 66 ikilinganishwa na idadi ya mwaka
>> 2009 ambapo kulikuwa na jumla ya tembo 38,975. na katika Mfumo ikolojia wa
>> Ruaha–Rungwa Tembo wamepungua kwa asilimia 36.5 ikilinganishwa na idadi ya
>> mwaka 2009 ambapo kulikuwa na jumla ya tembo wapatao 31,625.
>>
>> Kupungua huku kunathibitishwa na idadi ya mizoga ya tembo iliyohesabiwa
>> wakati wa zoezi la sensa. Jumla ya mizoga 6,516 na 3,496 ilihesabiwa katika
>> mifumo ikolojia ya Selous-Mikumi na Ruaha–Rungwa. Katika zoezi hili Wizara
>> ilitumia vigezo vya uwiano wa mizoga na tembo hai waliohesabiwa (carcass
>> ratio) kubaini vyanzo vya vifo hivyo. Katika hali ya kawaida, uwiano wa
>> asilimia 7 – 8 unaashiria vifo vya asili kama vile ugonjwa na uzee. Zaidi
>> ya asilimia hiyo inaashiria vifo visivyo vya asili.
>> Sensa iliyofanyika mwaka huu imeonesha uwiano wa asilimia 30 kwa mfumo
>> ikolojia wa Selous-Mikumi na asilimia 14.6 kwa Ruaha–Rungwa. Kwa mujibu wa
>> matokeo hayo, idadi kubwa ya vifo vya tembo vimetokana na vifo visivyo vya
>> asili.
>>
>> Uchambuzi wa kina umebainisha kuwa asilimia 95 na 85 ya mizoga
>> iliyoonekana katika mifumo ikolojia ya Selous-Mikumi na Ruaha–Rungwa ni ya
>> zaidi ya miezi 18 iliyopita.
>> Hii inaonesha kuwa juhudi za makusudi zilizofanywa na serikali ikiwa ni
>> pamoja na kuimarisha doria na operesheni maalum mbalimbali za hivi karibuni
>> zimesaidia kupunguza wimbi la ujangili kwa kiasi kikubwa.
>>
>> Aidha, kukamatwa kwa meno ya tembo yenye uzito wa kilogramu 32,987 ndani
>> na nje ya nchi katika kipindi cha 2008 hadi Septemba 2013 ni ishara tosha
>> kuwa ujangili ni mojawapo ya sababu kubwa za kupungua kwa idadi ya tembo
>> nchini.
>>
>> Sababu nyingine ni kuongezeka kwa mifugo katika maeneo yaliyohifadhiwa na
>> shoroba za wanyamapori. Mathalan, katika Pori Tengefu la Kilombero ambalo
>> ni sehemu ya ikolojia ya Selous – Mikumi, mwaka 2002 lilikuwa na tembo
>> 2,080, katika sensa ya mwaka huu, hukukuwa na tembo hata mmoja.
>>
>> Ongezeko la bei katika masoko ya biashara haramu ya meno ya tembo hususan
>> katika nchi za Mashariki ya mbali ni kichocheo na kisababishi kikubwa.
>> Kufuatia hali hii, Wizara inaimarisha ulinzi wa wanyamapori kwa
>> kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi nyingine za kanda
>> na kimataifa pamoja na kuelimisha na kushirikisha wananchi katika masuala
>> mbalimbali ya uhifadhi.
>>
>> Ili kuimarisha na kuboresha shughuli za uhifadhi, Wizara iko katika hatua
>> za mwisho za kuanzisha mamlaka mpya ya wanyamapori. Vilevile sheria za
>> uhifadhi zinapitiwa ili kuruhusu kuanzishwa kwa mfumo wa kijeshi kwa
>> watumishi wa sekta ya wanyamapori.
>> Wizara inapenda kuwatambua na kuwashukuru wafadhili wote waliofanikisha
>> sensa hii iliyogharimu kiasi cha dola za kimarekani 160,000ikiwa ni fedha
>> za serikali na wafadhili. Wafadhili hao ni Shirika la Misaada ya Kiufundi
>> la Ujerumani (GIZ) kupitia Frankfurt Zoological Society (FZS) na Shirika la
>> Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kupitia Mradi wa TANAPA wa SPANEST.
>>
>> *Imetolewa na*
>> Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
>> Mhe. Lazaro Nyalandu (MB)
>> 10/01/2014
>>
>> --
>> Send Emails to wana...@googlegroups.com <javascript:>
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+...@googlegroups.com <javascript:> Utapata Email ya
>> kudhibitisha ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts
>> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+...@googlegroups.com <javascript:>.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment