Karume, hii hadith kakufundisha nani?
----------
Sent from my Nokia phone
------Original message------
From: Fakhi Karume <fkarume@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, January 4, 2014 2:31:27 AM GMT-0800
Subject: [wanabidii] Jamani mapenzi ya kweli yapo mpaka sasa
Kijana asiye na kazi aitwaye Nolesy aliamua kumwoa rafiki yake wa muda
mrefu aliyekuwa akifanya kazi katika benki moja mashuhuri.
Nolesy alijitosa katika ndoa licha ya hofu na ushauri mwingi aliopewa na
ndugu kuwa ni vibaya kuoa ukiwa huna kazi.
Kila mwezi yule binti alimpa mmewe mshahara wake wote wa 800,000 baada ya
kutoa fungu la kumi kwa ajili ya kanisani.
Nolesy yeye alitoa 200,000 na kumpa mkewe kwa ajili ya matumizi binafsi na
zilizobaki kijana aliamua atumie kwa matumizi gani. Na hali hiyo ilidumu
kwa miaka mitatu mfululizo.
Furaha na amani viliitawala nyumba ile na kwa wanandoa wale pia kwa miaka
mitatu pamoja na kuwa marafiki wengi wa yule dada walimfuata na kumwambia
huwezi ukawa unalipa bill zote za nyumba na kufanya kazi zote wewe tuu na
mmeo kakaa tuu kwa nini msiachane?
Kuna mwezi mmoja kijana yule alitumia zaidi ya 500,000 akizunguka mikoa
mbalimbali kwa ajili ya intavyuu za kazi.
Hatimaye kijana alifanikiwa kupata kazi Mbeya katika kampuni ya Green
Entertainments na kuwa meneja mkuu huku akipokea mshahara wa milioni tatu
na nusu kama kianzio.
Akanunua gari yake ya kwanza mpyaa kwa bei ya shilingi 18M na akampa funguo
mkewe na kuendelea kutumia usafiri wa daladala kwa zaidi ya miaka miwili.
Baada ya hapo akanunua gari la pili jipya lenye thamani ya 30M na kumpa
mkewe na kulichukua gari la zamani na kulitumia yeye na mpya kumpa
mkewe.Miaka michache baadae wakahamia kwenye nyumba yao.
Siku moja mke alikuwa akitafuta dokyumenti zake katika makabrasha
mbalimbali pale chumbani kwao, alishangazwa kuona kuna bahasha ndogo
imefichwa na ndani kuna picha yake wakati wa harusi na akaona kuna
dokyumenti nyingine za manunuzi kiwanja na magari na vyote vikiwa
vimeandikwa kwa jina lake kabla ya kuona maandishi yaliyoandikwa:
''MKE WANGU NI KILA KITU KWANGU. ALIKUBALI KUOLEWA NA MIMI NIKIWA SINA
KITU, NA SASA NAAMINI HATA NIKIWA NA VITU VYOTE NI VYAKE KWANI MOYO WAKE NI
ZAIDI YA KILA KITU KWANGU NA FAMILIA YETU.AISHI MILELE"
Machozi yalimtoka dada yule na alifurahia sana ujumbe ule kabla ya
kukumbuka kuwa wiki chache baadae ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka yao ya
ndoa.
Hivi sasa MUNGU amewabariki na wana watoto wawili wakike na wakiume na
wanapendana mara mia zaidi ya mwanzo.
Jamani mapenzi ya kweli yapo mpaka sasa.
Je una uhakika kuwa mapenzi uliyonayo kwa mwenza wako ni sawa au yanaweza
kulinganishwa na haya?
Pamoja na vyote lakini kumbuka mnachaguana ili kuishi kwa shida na raha na
haijalishi nani ananunua mahitaji ya nyumbani au kulipa bili kwa
sasa.........
HAKUNA HALI YA UMASKINI INAYODUMU MILELE
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:
Post a Comment