Sunday, 25 November 2012

Re: [wanabidii] RE: KINANA ANAJIDANGANYA KUWAKOMBOA WATANZANIA

Ushahidi, ushahidi, ushahidi,
Kamwe hatutaupata. Hatutaupata kwa sababu katika nchi yetu tuko chini viwango vya Kiafrika.

Jirani zetu Kenya wanaweza kusikia jambo kuhusu rushwa wakachukua hatua kesho yake, wakachunguza hata kama ni Waziri na wakatoa taarifa kwa umma.

Hapa kwetu ukiandika kuhusu tuhuma jamaa wanasimama kwamba eti kama una ushahidi tuletee. Hata ile level ya taasisi kuwajibisha watuhumiwa kwa sababu za kimaadili haipo.

Ndo maana Mukama, Chiligati na Msekwa wamevuliwa gamba kwa sababu tu walijaribu kuwagusa watuhumiwa wasiogusika. Ukisema rushwa waziwazi ndani ya CCM unageuka kuwa adui wa wengi.

Jana nilisema kwamba kwamba sijui akina Mangula wataanzia wapi, maana utulivu unaodaiwa kuwa upo ndani ya CCM ni kutokana na watuhumiwa wa ufisadi kuachiwa watambe katika uchaguzi wa ndani ya chama.

Siku wakiguswa tu, mtaniambia. Katika mazingira kama hayo, hatuwezi kusonga mbele. Rushwa na ufisadi ndani ya CCM vimetaasisiwa (instituted corruption) na ndiyo maana maadui wa chama ni wale wanaopinga rushwa.

Wachapa kazi ndani ya CCM hawatakiwi, ndo maana watu kama Dk Magufuli, Dk Mwakyembe na wengine wenye kasi kama yao, hawapendwi na wengine utendaji wao umewagharimu afya zao. Tony Diallo akiwa Maliasili na Utalii alimgusa Severe akang'olewa.

Kumbe CS Luhanjo aliyekuwa akimlinda Jairo na madudu yake, aliacha mizizi maliasili wakati akiwa KM chini ya Zakia Meghji. Katika mazingira haya, tunawaaminije hawa wapya katika sekretarieti ya CCM?

Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 25 Nov 2012 09:58:52 +0000
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] RE: KINANA ANAJIDANGANYA KUWAKOMBOA WATANZANIA

Ernest,


Unadandia treni jamani! Ngoja tuone mwelekeo. Kwani trafiki hao wataacha chadema wakitawala? Mwenye kosa ni chama ama serikali chini ya JK? Je, akija mtu kama Slaa lakini upande wa ccm utaacha ubishi au wewe kosa ni rangi tu?

Kimbuka serikali za kiafrica institutional governance hakuna, ipo individual head of state effort na jinsi atakavyo washughulikia wakosaji chini ya serikali yake. Kwahiyo, vyama ni vyombo vya kupitia tu, inategemea ujasiri wa mkuu wa kaya, period!
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

From: Ernest Mmbaga <emmbaga@hotmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 25 Nov 2012 09:47:00 +0000
To: wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: RE: [wanabidii] RE: KINANA ANAJIDANGANYA KUWAKOMBOA WATANZANIA

Ndugu  yangu  Tony
Hicho  kigezo  cha  kusema "lete  ushahidi"  ndicho  kilichoifikisha  CCM  hapo  ilipo  na  kuitwa  kichaka  cha  wanyang`anyi.  ikimanisha  kwamba  , ujambazi  wote  unaosemwa  juu  ya kiongozi  wa CCM  anaeusema  ataulizwa  lete  ushahidi.  sasa  ingekua  kuna  uzalendo  kwamab  ukiletwa  ushahidi   utafanyiwa  kazi ,  labada  ungeletwa .  lakini  tofauti  ni  kwamba  atakaeleta  ushahidi  ,  atasakamwa  gizani  (  tumeshuhudia  hayo). Mfano  mdogo  ni  ushahidi  uliotolewa  katika  sakata  la  Richmond.  lakini  hao  takukuru  unaodai  wapelekewe  walisafisha  wakasema  hakukua  na  kosa.
 
hivi  ndugu  tony  sema  tu  kama  mtanzania  halisi  unaepita  mtaani  au  hat  unaendesha  gari,  hujawahi  ona  rushwa  ya  wazi  kabisa  inayofaanywa  na  baadhi  ya  askari  wa  usalam  Traffic??
 
hivi  TAKUKURU  hawaoni  kabisa  hayo  tunayoona  sisi??  kweli  kabisa  toka  moyoni  mwako??
 
Au  wataka  kutuambiwa  hayaa  yote  yasemwayo  kuhusu  Ufisadi   wa  Baadhi  ya  viongozi   ni  uongoo??   tuache  unafiki  na  sio  eti  kwakua  amechaguliwa  kinana  kua  Katibu  Mkuu.  basii  kabala  hata  hajafanya  chochote  CCM  imeshakua  Safi  ??  du  kwe;li  mmeona  watanzania  ni  wajinga  na  hawatfakari.....  endeleeni
 
Ernest  
 
Hiv
 

Subject: Re: [wanabidii] RE: KINANA ANAJIDANGANYA KUWAKOMBOA WATANZANIA
To: wanabidii@googlegroups.com
From: tony_uk45@yahoo.co.uk
Date: Sun, 25 Nov 2012 07:02:20 +0000

Langai Mlima wa moto!

Hilo nalo neno, na kweli wananchi wanaudhika sana. Lakini pia kwanini msiwe mnawasema hapa: mfano badala ya kuhisia tu ana magari 600, kwanini usilete orodha ya hayo malori (Reg number) na jina la usajiri na kujua jina hilo ni la mtoto au ndugu yake?

Pia mafisadi, vizuri mfano hapo arusha majengo plot nr na hati kama unaifahamu itasaidia. Takukuru nayo sasa inajipanga kupokea taarifa kama hizi maana hisia tu hazitasaidia. Kuna watu siku moja watasema Mbowe ana dola milioni 50 kaweka Uswiss bila kuwa na details haisaidii sana.

Watanzania ni woga wa kutoa taarifa sahihi lakini wepesi kudakia maneno. Sasa kwanini hata ushupavu huu wa udaku tusiutumie kutaja mali za mafisadi hapa ukiwa na ushahidi? Mitandao inaweza kutumika productively ikasaidia kuongeza uwajibikaji na kupunguza ufisadi nchini; iwe kwa ccm au chadema au Cuf.

Umbeya na malalamiko tu yasiyo na takwimu sahihi haitasaidia hata tone na tatizo litaendelea hata kwa serikali zisizo za ccm. Watu ni walewale; watakuwa wamebadili rangi, matendo hayohayo.
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

From: LENGAI OLDOINYO <lengai2000@yahoo.co.uk>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 25 Nov 2012 05:50:02 +0000 (GMT)
To: <hlib@muhas.ac.tz>; <mum@mum.ac.tz>; <info@mzumbe.ac.tz>; <info@out.ac.tz>; <info@ruco.ac.tz>; <mfumbusa@yahoo.com>; <vcsaut@saut.ac.tz>; <admission@saut.ac.tz>; <stmarksadmin@sjut.ac.tz>; <gchelelo@sjut.ac.tz>; <admin@sjut.ac.tz>; <sua@suanet.ac.tz>; <vc@suanet.ac.tz>; <dvc@suanet.ac.tz>; <dvcadminfin@suanet.ac.tz>; <fos@suanet.ac.tz>; <ice@suanet.ac.tz>; <sua-tu@suanet.ac.tz>; <scsrd@suanet.ac.tz>; <pestman@suanet.ac.tz>; <plan@suanet.ac.tz>; <pro@suanet.ac.tz>; <support@suza.ac.tz>; <info@teku.ac.tz>; <dpacademic@duce.ac.tz>; <elctsmmuco@smmuco.ac.tz>; <info@butmaninternational.com>; <sematangotours@cybernet.co.tz>; <serenacarhire@habari.co.tz>; <sgresort@yahoo.com>; <sss@habari.co.tz>; <tours@albatros.co.tz>; <mia@albatros.co.tz>; <info@chadema.or.tz>; <rassingida@pmoralg.go.tz>; <mhariri@habarileo.co.tz>; <advertising@dailynews.co.tz>; <jennie@albatros.co.tz>; <shidolya@yako.habari.co.tz>; <sssafaris@cybernet.co.tz>; <s-s.kolowa@web.de>; <wanabidii@googlegroups.com>; <unasemaje@radiofreeafricatz.com>; <mwananchipapers@mwananchi.co.tz>; <globalpublishers@dar.bol.co.tz>; <educate@intafrica.com>; <costech@costech.opc.org>; <info@satif.or.tz>; <info@satf.org>; <eotf@raha.com>; <eotf@cats-net.com>; <zitto@chadema.or.tz>; <worldtourstanzania@hotmail.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] RE: KINANA ANAJIDANGANYA KUWAKOMBOA WATANZANIA

Katika mambo ambayo Katibu Mkuu wa chama tawala CCM ndugu Abdulrahaman Kinana anajidanganya nayo ni kutegemea kuwa ataweza kuleta mabadiliko Tanzania bila kuwatoa mhanga Mafisadi na watu waliojilimbikizia mali wakiwa madarakani. Kinachofanya watu waichukie CCM sio kitu kingine zaidi ya Viongozi walioko madarakani kuibia Watanbzania na kujilimbikizia mali.

 

Serekali ya CCM haitaweza kabisa kuleta imani kwa Watanzania bila kurudisha mali walizoiba na kufuta mikataba mibovu yote ya wawekezaji inayolifilisi Taifa. CHADEMA itaendelea kupeta na wakizubaa watajikuta wako nje ya utawala na mali zao zote kutaifishwa. CCM wakati ni huu wa kurudisha kila mlichokwapua. Sasa hivi tusiwadanganye Watanzania kwa kuwa kila linalofanyika Watanzania wanaliona. Mtoto wa Rais anamiliki biashara za kuchimba madini, kusafirisha mafuta, kusafirisha mizigo huku akiwa na malori zaidi ya 600 fedha hizo amezipata wapi?.

 

Mawaziri mbali mbali na viongozi wa ngazi za juu wa CCM na Serekali yake wanajihusisha na biashara. Chama kinaua viwanda kikidai hakitaki kujihusisha na biashara lakini viongozi wake wote ni Wafanya biashara. Kama Serekali imeviua viwanda vyote na kunyima Watanzania ajira kwa kisingizio cha kutokutaka kufanya biashara wao kama viongozi wanafanya biashara za kazi gani?.

 

CHADEMA tunaomba muikomboe Tanzania kabla ya kufilisika, na pingeni majeshi ya Tanzania kupelekwa Congo. Wale waasi wanapinga matumizi mabaya ya rasilimali hivyo hawana tofauti na nyie CHADEMA. Hakuna kumsaidia kabila anachezea mali za Wakongo kama CCM. Tanzania tuna matatizo makubwa ya rushwa, umasikini, uongozi mbobu, kupanda kwa maisha kwa nini tumsaidie mtu anayechezea rasilimali za nchi kama Kabila. CCM inataka kutoletee mambomu Tanzania.

 

 CHEDEMA piteni kila mahali kuhakikisha mnashinda uchaguzi Mwaka 2015. CCM ni usanii tu hakuna jipya. Mwisho kila Mtanzania anayeitakia mema Tanzania ajiulize ni kwa nini Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hajawahi katika maisha yake kuvaa mavazi ya CCM. Mwalimu Julius Nyerere alikuwa anaona mbali. Alijua CCM itamsaliti kwa kuzika juhudi zake zote za kumkomboa Mtanzania. CHADEMA kazi kwenu kuikomboa nchi, Kinana akitaka Watanzania tumuamini kuwa sio Kondoo aliyevaa ngozi ya chui awafunge kwanza wezi wa mali za umma.

Mkereketwa

Lengai Ole Letipipi


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk
CORE 2 DUO
2.0 GHZ CPU
2 GB RAM
DVD/CD - RW
WINDOWS 7 /WINDOWS XP
WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0718 637905
0786 806028
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk
CORE 2 DUO
2.0 GHZ CPU
2 GB RAM
DVD/CD - RW
WINDOWS 7 /WINDOWS XP
WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0718 637905
0786 806028
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment