Friday, 20 July 2012

[wanabidii] cuf imemtosa waziri wake, ajali ya meli

KUFUATIA kuzama kwa meli ya MV SKAGIT ,Mwenyekiti wa chama cha wananchi cuf, Prof.Ibrahim Lipumba amesema kuwa anaamini Waziri wa miundombinu na mawasiliano,Hamad Masoud atapima uzito na kulazimika kuwajibika kisiasa ili kumchia nafasi rais kufanya maamzi mengine.

Profesa Lipumba ametamka hayo kwenye mkutano na wandhishi wa habari baada ya kuulizwa swali na mwanahabari kuwa CUF inatuhumiwa kumlinda Masoud ambaye ni mwanachama wao asijiuzulu katika ajali kama hiyo iliyotokea Mwaka jana na kusababisha watu takribani 300 kupoteza maisha.

"Kwa hili staki kumsemea waziri lakini naamini ,waziri wetu ni mtu mwenye busara atachukua maamzi ya busara hata kama itabainika kuwa haukuwa uzembe wake , hiyo ni kawaida kwa wanasiasa kuwajibika pale inapotokea waliopo chini yake wakafanya kosa au uzembe kama tunavyooona hata kwenye bajeti wanaoandaa bajeti ni wengine lakini linapotkea tatizo waziri ndio anajiuzulu"alisema Prof.Lipumba

kauli hiyo imeweka wazi stofahamu iliyokuwa imetanda zanzibar kuwa kabla ya chama cha wananchi cuf kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ilikuwa ya kwanza kushinikiza viongozi wa CCM kujiuzulu linapotokea tatizo zanzbar lakini sasa tangu walipoingia madarakani wamekuwa wakishindwa kuonyesha mfano huo.

0 comments:

Post a Comment