2012/7/24 Boniface Magessa <magessabm@gmail.com>
nilishangaa sana kwa habari ile, nafarijika kuona hili la leo.--2012/7/24 Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com>
Kwenye barua yake kwenda kwa uongozi wa juu wa gazeti la mwananchi,
hii ni sehemu ya barua yake.
Nasikitika kutumia nafasi hii kukuandikia kukutaarifu kuwa gazeti lako
la Mwananchi la Julai 23, 2012, katika habari yake iliyoongoza ukurasa
wa kwanza (lead story) limenilisha maneno na kunikuu isivyo sahihi.
Katika habari hiyo yenye kichwa cha habari kisemacho "Wabunge
wamsafishia Zitto njia ya urais 2015," gazeti lako limeandika hivi
"Mdee aliyepewa nafasi ya kuwasalimia wananchi alisema amekuwa na
Zitto tangu Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kwamba kutokana na ujasiri
na umahiri wake katika kutetea masilahi ya wanyonge na taifa, anafaa
kuwa mmoja wa viongozi wa juu katika Taifa."
Gazeti lako pia katika aya iliyofuata limenukuu kuwa mimi nimesema;
*"Ndugu zangu watu wa Kigoma, kwa kweli mna bahati sana, achilia mbali
kuwa na vipaji katika sanaa ya muziki na michezo hasa mpira wa miguu,
lakini mna wanasiasa wakali ambao ni tishio hapa nchini. Mimi
namkubali sana Zitto Kabwe na ninaamini kuna siku atakuwa kiongozi wa
juu katika nchi yetu," alisema Mdee"
Nasikitika kusema kuwa gazeti lako limeandika habari zisizo za kweli
kwa kunilisha *maneno na kudai kuwa mimi ndiye nimesema maneno hayo,
kisha kuyaweka kwenye nukuu, likisema kuwa ni nukuu yangu. Sijajua nia
au kusudio la gazeti lako kuamua kupotosha ukweli na kushindwa kabisa
kuninukuu kwa usahihi, kama inavyotakiwa katika misingi ya taaluma ya
habari.
Nasikitika pia kusema kuwa gazeti lako ambalo limeonekana kujijengea
heshima miongoni mwa wasomaji wa kada mbalimbali nchini na hivyo
linapaswa kuwa mfano wa kuigwa, linaweza kusigina misingi ya uandishi
wa habari na hususan katika kufuata maadili ya taaluma hii muhimu, kwa
kiwango cha kufanya moja ya dhambi kubwa ya kukilisha maneno chanzo
cha habari.
Kwa ajili ya kutunza heshima ya gazeti lako, lakini pia kwa ajili ya
maslahi mapana ya taaluma ya habari na jamii ya Watanzania,
nakuandikia kulitaka gazeti lako likanushe maneno liliyoninukuu katika
toleo hilo la Julai 23, 2012. Ni vyema sana hilo likafanyika kwa uzito
unaostahili kama ilivyoandikwa katika toleo hilo.
Habari hiyo imeniletea usumbufu mkubwa hasa kwa wanachama wa chama
changu, CHADEMA, ambao wanajua kuwa chama chao makini ni mahiri katika
kufuata katiba, kanuni na taratibu katika kuendesha mambo yake kwa
manufaa ya watu wote. Napenda kuwa mmoja wa Watanzania makini na
viongozi wanaojua wajibu, ikiwemo kufanya nini na kusema nini, mahali
gani na wakati gani.
Nakutakia utekelezaji mwema katika hilo.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
Sent from Samsung Galaxy Ace GT-S 5830 --The future of Android Technology
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
..Blaming fate instead of oneself is always the way cowards sleep better at night!
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment