2012/7/25 Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
na Zitto Kabwe
Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari
yenye kusomeka 'Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015'. Habari
hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa
zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari
kukanusha maneno waliyonukuliwa kusema. Napenda kusema masuala
yafuatayo.
Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola,
Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David
Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa
kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi.
Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph
Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba.
Wabunge hawa hawakualikwa na mimi na wala sikufanya mazungumzo nao
yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au
hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa.
Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza.
Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee,
Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.
Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na
video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya
documentary ya tamasha lile la kihistoria.
Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii
iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana
katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe
tukio la Kigoma tu.
Kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi
itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi
zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema
Kigoma. Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyote ile na matamshi yao,
habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli
ndio utasimama.
Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya
kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya
urais yanapotajwa zinashangaza sana.
Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea
Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato
utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha
bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii
na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa
hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.
Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema
'weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba
ya maneno. Tusimalize yote.
Zitto Kabwe
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
Sent from Samsung Galaxy Ace GT-S 5830 --The future of Android Technology
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment