huu ni udictator wa wazi, SSRA wanataka kujiopanga kiuchumi, watumie fedha zetu kujinufaisha, ninasikitika kuwa hizo fedha zinzpotea ni haki zetu lakini zimeporwa. mfano kampuni zetu binafsi tunazofanyia kazi huwa zinakufa usipofuatilia mafao yako NSSF nao wanakuwa wasanii wakijua kampuni ilikufa wanakuambia katafute barua ya mwajiri au akujazie fomu wakati hayupo, utakwenda wapi? siku hizi imekuwa tatizo ukitaka fedha zako wanakusumbua miaka miwili, njoo ndenda rudi!!! mzee wa miaka 60 upo kijijini unapigwa changa mjini hata nauli huna, utajisikiaje?
Mimi ni m moja wapo wa walionufaika na mafo ya kujitoa, ni ukweli kuwa hizo fedha zimenisaidia sana na zimebadilisha hali ya masiaha yangu, nilivyokuwa mwaka jana na mwaka huu ni tofauti kabisa, niomeweza kufanya kainvestment kangu kadogo na kameeleweka wakati huu ambao nina nguvu na afya nzuri na ninaweza kuikimbizana, je kama ningeliepwa nikiwa mzee ningeweza kukimbizana na biashara? hivi sasa nimepata kibarua tena mahali nataka kurudi kwenye mfuko!
Kila la Heri wajameni ambao mtafikisha hiyo miaka 50, hayo ni majadiliwa ya Mungu. tunaambiwa kuwa umri wa kuishi ni 47 sasa 55 inatoka wapi?
From: John George <georgejn2000@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, July 23, 2012 8:14 AM
Subject: Re: [wanabidii] UFAFANUZI KUHUS FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII
Je kuna namna yeyote ya kudai sheria hii ibadilishwe? Inakuwaje wafanyakazi wenyewe hawajui. Je walishirikishwa kiasi gani katika hilo maana pesa ya ya kwao wameichangia. Hakuna riba baada ya miaka yoote mtu anapofanya kazi na kuchangia.Tunajua Social security kwa nchi kama hii ni tataizo na inatikona na kwamba ukichanga millioni 30 after 30 years utapata hizohizo nazo zitakuwa sawa na millioni mbili au elfu thelathini wakati huo
2012/7/22 RAMADHANI Selemani <ramson34@gmail.com>Mambo mengine ni ya ajabu sana...life span ya mtanzania ni kama miaka 47 hivi kwasasa, ukisema mtu aende akachukue mafao yake baada ya miaka 55-60, je utakwenda mzimu wake!!!???nchi hii sometimes ina maamuzi ya ki bogus sana.ktk hili hatuhitaji phd kujua kwamba huu ni ujinga..On Jul 21, 2012 1:20 PM, "Yona Maro" <oldmoshi@gmail.com> wrote:--Makamu wa Rais, Corporate AffairsBarrick GoldS.L.P 1081Dar-es-SalaamUFAFANUZI KUHUS FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia1
wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo. Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.Wenu.Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment