Tuesday, 17 July 2012

Re: [wanabidii] MWANAHARAKATI MBEYA AFUNGWA MWAKA MMOJA NA NUSU

Wanaharakati wa kweli wamezungukwa na mambo mengi yenye muonjo wa visasi. Katika hili la huko Mbeya kufuatana na maelezo ya mleta habari linaweza kuwa na harufu ya hayo niliyoyasema hapo juu.

Cha kufanya, Ndg. Temba wasiliana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dar es Salaam, kitengo cha Humanrights Defenders. Watakachofanya, watakwenda mahakamani huko kesi ilikosikilizwa na kuamuliwa ili kupata mwenendo mzima wa kesi. Wakijiridhisha kwamba kulikuwa na mapungufu yoyote katika mwenendo wa kesi, basi wataishughurikia kwa gharama zao.



Asante sana kwa taarifa hii.



Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom

From: deogratius temba <deojkt@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 17 Jul 2012 03:16:30 -0700 (PDT)
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com<mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>; Wanazuoni@yahoogroups.com<Wanazuoni@yahoogroups.com>; wanakenya@googlegroups.com<wanakenya@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] MWANAHARAKATI MBEYA AFUNGWA MWAKA MMOJA NA NUSU

 
Mwanaharakati Mbeya afungwa mwaka  mmoja na nusu
 
Mwanaharakati mwenzetu  ngazi ya jamii aitwaye Frora Mathias, ambaye ni mtetezi wa  haki  za wanawake na makundi mengine yaliyoko pembezoni, yuko Gereza la Luanda Mkoani Mbeya tangu Ijumaa tarehe 13 Julai 2012 kwa kesi ya kupotea kwa fedha za SACCOS.
 
 Flora Mathias ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ifiga kata ya Ijombe,  wilaya ya Mbeya Vijijini ni Mhasibu wa kikundi cha  JUHUDI SACCOS  kata ya Ijombe, na amefanya kazi kama muhasibu wa SACCOS hiyo kwa miaka 7. Kwa mujibu wa Flora, siku ya Alhamisi tarehe 29 Juni 2012 alipokuwa anapeleka fedha za SACCOS benki kiasi cha shilingi milioni tano (Sh. 5,000,000/=) tu, muda wa saa nne asubuhi, aliposhuka kutoka kwenye basi alilosafiria alikutana na mtu ambaye alimsalimia. Baada ya hapo hakumbuki chochote kilichotokea ila alijikuta yuko katika kichaka eneo la makaburini saa kumi jioni akiwa hana fedha zote alizokuwa nazo awali. Alipoona hivyo Flora alirudi kijijini kwake na kutoa taarifa kwa wanakikundi wenzake.
 
Baada ya hapo Flora aliitwa ofisini  kwa Mtendaji wa Kata ya Ijombe, Bwana Mpoki Kajange ambaye aliamuru Flora akamatwe na mgambo na kupelekwa moja kwa moja mahakamani (mahakama ya mwanzo ya Uyole). Hakimu wa mahakama hiyo aliandika maelezo ya Flora na kuamuru apelekwe rumande gereza la Luanda na hakuruhusu dhamana. Mtendaji wa kata ya Ijombe alikataa kutoa barua ya dhamana akidai yeye ndiye aliyemshtaki Flora, hivyo alishauri wakatafute barua ya dhamana kutoka kata nyingine.  Flora alikaa rumande kuanzia tarehe 29 Juni  hadi alipopelekwa mahakamani tarehe 3 Julai 2012 na kupata dhamana kwa masharti ya kupeleka sh. milioni mbili na laki tano (2,500,000)=/ ifikapo siku ambayo alipangiwa kurudi tena mahakamani yaani tarehe 12 Julai 2012.
 
Baada ya Flora kutoka nje kwa dhamana alidai kuwa akiwa mahakamani siku alipokamatwa alishuhudia Mtendaji wa Kata ya Ijombe akimpa HAKIMU fedha. Wanakikundi wa SACCOS walimweleza Flora kuwa Mtendaji aliwadai wampe shilingi laki mbili (sh. 200,000/=) kwa ajili ya kufungua kesi mahakama ya mwanzo Uyole.  Hata hivyo Flora, waliamua kupeleka suala hili TAKUKURU Mbeya.
 
Siku ya Alhamisi tarehe 12/07/2012 Flora akiwa na msaidizi wa sheria toka ofisi ya Haki za Binadamu na wanakikundi wa Juhudi SACCOS, walifika mahakamani saa mbili asubuhi na kusubiri mpaka saa nane mchana, ndipo karani wa mahakama alipowajulisha kuwa hakimu hakuwepo hivyo warudi tena siku ya Jumatano tarehe 18 Julai 2012. Waliondoka na walipofika kituo cha basi yule karani aliwakimbilia na kuwajulisha kuwa hakimu alikuwa amefika hivyo warudi mahakamani. Baada ya kushauriana waliamua kutorudi kwani hata mshtaki (Mtendaji wa Kata) alikuwa ameshaondoka.
 
Ilipofika saa moja usiku siku hiyohiyo Flora alipigiwa simu na karani wa mahakama na kujulishwa kwamba kesho yake tarehe 13/07/2012 alitakiwa afike mahakamani. Walipofika mahakamani asubuhi walisubiri na ilipofika saa  saba mchana  hakimu  alisoma  mashtaka na kumhukumu Flora kwenda jela mwaka mmoja na nusu na kumtaka akitoka  alipe fedha za kikundi zilizopotea.
 
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

"By faithfulness we are collected and wound up into unity within ourselves, whereas we had been scattered abroad in multiplicity"
Saint Augustine (354-430) Theologian

0 comments:

Post a Comment