Tuesday, 10 July 2012

Re: [wanabidii] Dr. Namala Mkopi apandishwa kizimbani

Tiks, usije kulia tu hapa bure! 

2012/7/10 <tikooza@yahoo.com>
Ahsante Mutabaazi kwa shule.

Kipofu kama mimi naendelea kuwaza hivi kushtakiwa kwa Rais wa MAT itasaidia kuondoa mgogoro au itaongeza?? Bado najiuliza jinsi ambavyo tunacheza na afya za watanzania walio maskini.

Naanza kuona madhara ya mgomo huu yatakuwa makubwa kuliko serikali inavyofikiria kama haitatafuta suluhu nje ya mahakama. Nimesema muda fulani hapa jukwaani kwamba mgomo wa madaktari utaathiri wanafunzi wanaopenda sayansi hasa PCB kuhamia masomo mengine. Nakumbuka mwaka 2002 pale mlimani wanafunzi waliomaliza PCM waligoma kuomba engineering courses badala yake wengi wakakimbilia kuomba Bcom. Hii ilitokana na kwamba na wakati huo wanafunzi wa engineering walikuwa wanafeli sana.

Sasa piga picha hali hii ya madaktari ambayo unasoma miaka saba kupata shahada ya kwanza. Huku fani zingine anasoma miaka mitatu na anaweza kusoma shahada ya pili wakati bado huyu daktari anahangaika na moja. Fikiria tabu anayopata kwa kuhaingaika na wagonjwa, mshahara mdogo, hurusiwe kudai haki yako kwa kuwa ni kazi ya wito na kiapo cha kazi hakiruhusu kugoma. Piga picha anapogundua kuwa hana ulinzi pale anapodai haki yake.

Sioni namna gani mwanafunzi anaweza kupenda kazi hii labda kama ana malengo ya kutumikia nje ya Tanzania.

Mungu atusamehe, huruma yake ndio tumaini letu maskini.
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

From: "mutabaazi lugaziya" <mjlugaziya@mail.com>
Date: Tue, 10 Jul 2012 13:44:13 -0400
Subject: [wanabidii] Dr. Namala Mkopi apandishwa kizimbani

Baada ya serikali kuitumia mahakama ya Kazi kujaribu kuwadhibiti madaktari, sasa imekimbilia mahakama ya Kisutu, ambako kuna vijana wanaoutaka Ujaji-wakiambiwa, wanafanya!

Ndugu zangu, kwa mujibu wa sheria, Penal Code, Sura ya 16, kifungu cha 114, kosa analotuhumiwa nalo Dr. Mpoki ni kudharau mahakama. Period!.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, anayedharau amri ya mahakama huwa anapelekwa mbele ya Jaji au Hakimu aliyetoa AMRI iliyokaidiwa. Kwa msingi huu, nathubutu kusema, na niko tayari kutetea kauli hii, kwamba kesi iliyo mahakama ya Kisutu, haiko sawa kisheria.

Hivi, wahusika wote katika system ya administration of justice, hawajui jambo hili ambalo "anybody with a browing acquaintance with law" analijua?.

Kwa lugha nyingine, inawezekana kwamba hawajui kuwa kwa hakika wao ndion wanafanya kosa la CONTEMPT OF COURT, kwa kuonyesha, kwa kujua ama kutokujua(which is never a defence), kwamba Mh. Jaji Sekela Moshi aliyetoa amri ile HANA UWEZO WA KUISIMAMIA AMRI YAKE?

Je Hakimu hajui kuwa anafanya kosa lile lile kwa kupokea kesi ambayo iko kwa mkubwa wake kikazi? Kosa linalodaiwa limefanywa "in limine litis" yaani katikati ya shauri linaloendelea Mahakama Kuu.

Mahakama inao uwezo wa kutokukubali mashauri yanayopelekwa kwake kinyume cha sheria. Ni vema mahakimu wetu wakaelewa mamlaka waliyonayo katika kupokea na kusikiliza mashauri.

Hivyo ndivyo sheria ilivyo,

MJL

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment