Monday, 1 April 2013

[wanabidii] Re: TANZANIANS AND FEAR TO SYSTEMATIC ANSWERS

Mnamo tarehe 7 Machi 2013, ikiwa ni takribani wiki mbili kabla ya kifo cha Mawalla, Manyerere aliandika maneno haya mtandaoni: "Tatu, Grumeti haipo Ngorongoro, bali ipo ndani ya Serengeti, wilaya ya Serengeti, mkoani Mara. Nabii wao wa kisheria ni Mawalla anayepatikana mjini Arusha. Hii ni mali ya kina Tudor Jones, Sir George Kahama na makaburu kadhaa. Kwa msaada zaidi kamwone Madanga Shaaban Madanga au yule veteran aliyeng'atuka Uhuru. Grumeti ni moja ya sehemu tamu kabisa za kwenda kupumzika. Kuna vyumba vya bei nafuu vya dola 1,800 za Marekani (siyo za Zimbabwe) kwa usiku mmoja! Wadau wengine watembelee huko wale maisha kama ulivyokula dada Leila"


From: Deo Kibambizi <kibambizi@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, April 1, 2013 2:49 AM
Subject: [wanabidii] TANZANIANS AND FEAR TO SYSTEMATIC ANSWERS

Mara nyingi kwenye blog zetu,nimekuwa nikiona wana jamvi wakichangia sana sana kwa mambo ambayo majibu yake hayako wazi.Mfano mambo ya dini ambayo kila mtu anakuwa na jibu lake yamekuwa yakiongoza kwenye post.Na pia mambo ya majungu nikimaanisaha mambo ambayo kiukweli hamna wa kuthibitisha yamekuwa yakipata wachangiaji,na cha kusikitisha mchangiaji anajiita MSOMI.Ila kuna mambo mengine ambayo,japo yana kasoro ila yakipata mtu wa kuyaelezea vema(SYSTEMATIC) basi hakuna wa kuchangia kwa sababu watu wengi hasa ndugu waandishi hawana uelewa wa mambo fulani fulani.Ila we....LETA JUNGU UONE jinsi kila mmoja atakuwa mstari wa mbele kuachangia.Mfano;waziri wa ujenzi Dr.Magufiri anajiamini,na aliisha jua njia sahihi ya kutoa taarifa na pia kuwajibu na kuwaambia watu hasa waandishi wa habari...ni kutumia LOGIC ZA taaluma yake na hapo watu wana kaa kimya na kuendelea kumsifia kwa yale ayasemayo.Japo anafanya kazi vema,je hakuna hata wataalaamu wa kutegua LOGIC ZAKE kweli au hadi afe au atoke wizara moja aingie wizara nyingine?Ndugu zangu.Dr.Magufuri huwa ninampenda sana na kumuamini kwa mambo mengi anayofanya,na hii ni kwa sababu ninaona matokeo ya mambo ya misimamo yake na faida kwa Taifa.Ila kuna baadhi ya watu huwa tunaogopa kuokosoa mambo kwa kushindwa LOGIC SETTNG hasa waandishi na pia kuogopa kuwa responsible kwa wahusika pale tukipata nafasi ya kugundua maovu yao.
Suala la Marehemu Mawala limenifumbua macho na kuona udhaifu wa Manyerere.Manyerere aliogopa LOGIC za Mawala na akakaa kimya hadi siku ya kifo chake.Aliogopa LOGIC ZA LAW hadi TAIFA likaingia kwenye janga hili ambalo kila mwenye dhamana ya nchi,na hasa wale wanaolewa mambo ya kuendeleza uchumi wa nchi yetu.Manyerere alishindwa nini kutueleza haya kabla ya Mawalla kuaga dunia.Naweza kusema,Mawala wengine wapo wengi ambao Manyerere anawafahamu,ila anasubiria wafe ndiyo aonekane yeye ndiye nabiii wa yake yaliyopita na wala si wa yale yajao.

NAULIZA,Hasa kama Manyerere angejibu haya kama yumo humu,au rafiki amtumia ili tupate pa KUMSHKURU KWA HILI.Vinginevyo tufahamu kuwa hakuna anayeshukuriwa kwa UNAFIKI.
1.Je,kama Mawalla angeendelea kuishi kwa staili hii je,Manyerere angesema haya?
2.Je,Manyerere alifahamu hili mapema?Kwanini hakutariifu mamlaka zinazohusika?
3.Je,Manyerere kwa nini atokezee hadi baada ya kifo hiki?

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


Read More :- "[wanabidii] Re: TANZANIANS AND FEAR TO SYSTEMATIC ANSWERS"

[wanabidii] The simplicity of China-Africa relations: HIVYO NDIVYO INAVYOTAKIWA

Ninakubaliana na Kamala
Na kuwa, mtani wangu Matinyi, AMEANDIKA kwa ufasaha akionesha ukweli wa mambo.
Hivyo ndivyo inavyotakiwa.

Aldin
 
Aldin K. Mutembei   (PhD)                         Aldin K. Mutembei (PhD)
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili                  Institute of Kiswahili Studies
Kampasi ya Mwalimu J.K. Nyerere             Mwalimu J.K. Nyerere Campus
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam                   University of Dar es Salaam, TANZANIA
+255 715 426 162      [Kiganjani]                +255 715 426 162  (Cell)

b-pepe: kaimutembei@gmail.com    
            Alternative e-mail: <kaimutembei@gmail.com>


From: J L Kamala <jlkamala@yahoo.com>
To: Wanazuoni@yahoogroups.com
Sent: Monday, April 1, 2013 1:04 PM
Subject: Re: [Wanazuoni] The simplicity of China-Africa relations

 
For the first time, I read something good about President Xi's Visit to Tanzania which in my view, it is great to strengthen ties with China than the rest of the world.

--- On Sun, 3/31/13, chaggama <chaggama@yahoo.com> wrote:

From: chaggama <chaggama@yahoo.com>
Subject: Re: [Wanazuoni] The simplicity of China-Africa relations
To: Wanazuoni@yahoogroups.com
Date: Sunday, March 31, 2013, 8:50 AM

 
Amen




Sent from Samsung tablet

Mobhare Matinyi <mobhare@gmail.com> wrote:
The
  simplicity of China-Africa relations
  Mobhare
  Matinyi, Washington DC. The Citizen, Tanzania. Thursday, 28 March 2013 20:30.
  Just
  ten days after taking office as the leader of the People's Republic of China,
  President Xi Jinping landed in Tanzania on Sunday to begin his three-nation
  historic tour of Africa that included South Africa and the Republic of the
  Congo. He had just concluded his first foreign tour in Russia.
  President
  Xi's visit to Russia was explicable, but his decision to come to Africa
  before anywhere else stunned and even angered Western capitals and their
  biased press which always sees the worst side of Africa. He didn't care!
  Perhaps
  what was more surprising was Xi's decision to start his visit in Tanzania,
  arguably the real friend of China in Africa for five decades now. Fine, a
  third of Sino-Africa trade is with South Africa, and Congo-Brazzaville
  supplies crude oil, but why Tanzania?
  To
  quickly recap, Tanzania started relations with China immediately after the
  independences of Tanganyika and Zanzibar, and continued after the unification
  in 1964. Tanzania and China signed the Treaty of Friendship in February 1965
  when President Julius Nyerere visited the country in the first of his five
  visits although economic, technical and military relations had already
  started in 1964.
  Several
  agreements and visits by civilian and military leaders of the two countries
  followed including three Tanzanian presidents who came after Nyerere, and
  three Chinese premiers starting with Zhou Enlai in 1965, Zhao Ziyang in 1983,
  and Li Peng in 1997.
  When
  the then Chinese president, Hu Jintao, visited Tanzania in February 2009, the
  leader of the world's most populous nation and the emerging superpower noted
  admirably in his speech that the China-Tanzania relationship had become "a
  model for both China-Africa and South-South cooperation."
  The
  stories of China and Tanzania go centuries beyond modern history, a reason
  why Kilwa archaeological excavations recovered many Chinese coins dating to
  the Song Dynasty which ruled China between 960 and 1279. Yes! That far back!
  The
  Chinese will never forget how Tanzania led other African nations in
  supporting Beijing's efforts to regain its seat at the United Nations,
  kicking out the Taiwan-based Republic of China.
  Between
  the two friendly countries there is a lot to justify their closiness, like
  the Tanzania-Zambia Railway (Tazara), and much more in foreign policy and
  ideological matters to warrant Xi's decision to pay such an honourable visit
  to the United Republic of Tanzania. Putting it short and simple, Tanzania and
  China are friends in need and indeed.
  But
  again, why did he choose to visit Africa after Russia, snubbing the big
  powers? President Xi wanted to send the message that China is serious about
  its relations with Africa. Why Africa? Well, historical ties are there, but
  in addition to that China needs Africa and Africa needs China, and between
  them there is neither hypocrisy nor hidden agenda.
  I like
  the way Tanzanian President Jakaya Kikwete puts it every time the Western
  press bothers him. In one incidence in December 2011 he said: "Africa needs
  markets for its products; Africa needs technology and infrastructure for its
  development. China is ready to provide all that. What is wrong with that?"
  Speaking
  in Washington DC in 2009 at the United States-Africa Business Summit,
  President Kikwete told Americans: "Why complain about China? Just come to
  Africa and invest the way the Chinese are doing."
  There
  is nothing complicated between China and Africa; it is give and take.
  Africans are aware of the situation that exists currently in which China
  seems to benefit more, but these things can be settled out with time and
  without the help of the West. Some of these challenges are counterfeit
  products, the sudden growth of the Chinese diaspora in African cities, and
  the poor quality of Chinese workmanship.
  But I
  don't agree with those who lament that China buys raw materials from Africa
  but brings in finished goods. Come on! Who prevented Africans from doing the
  opposite?
  As we
  speak today, annual China-Africa trade stands at $200 billion, and if the
  trend continues Africa will soon surpass the sluggish economies of the US and
  the European Union. Shockingly, US-Africa trade stands slightly below $100
  billion, while the EU is taking forever to conclude an economic
partnership agreement
  with Africa.
  If that
  is the case then, why should President Xi bother about the "powerful" West?
  Is that difficult to figure out? Again, China has what Africa needs and
  Africa has what China needs, and that is all we need in our mutual
understanding
  and respect as Xi told the world and Africa on Monday. Nothing is complex!
  Probably,
  it is time for those who trumpet aloud about new Chinese colonialism to
  Africa to be realistic. Africans want to move forward and they have no time
  with anyone who wants to impose their will on others. Africans are growing
  tired of receiving charitable donations and being lectured endlessly; let the
  world understand!




http://www.thecitizen.co.tz/editorial-analysis/20-analysis-opinions/30043-the-simplicity-of-china-africa-relations




  

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.

TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl

For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en

---
You received this message because you are subscribed to the Google
Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send
an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


------------------------------------

Yahoo! Groups Links

<*> To visit your group on the web, go to:
    http://groups.yahoo.com/group/Wanazuoni/

<*> Your email settings:
    Individual Email | Traditional

<*> To change settings online go to:
    http://groups.yahoo.com/group/Wanazuoni/join
    (Yahoo! ID required)

<*> To change settings via email:
    Wanazuoni-digest@yahoogroups.com
    Wanazuoni-fullfeatured@yahoogroups.com

<*> To unsubscribe from this group, send an email to:
    Wanazuoni-unsubscribe@yahoogroups.com

<*> Your use of Yahoo! Groups is subject to:
    http://docs.yahoo.com/info/terms/

__._,_.___
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (4)
Recent Activity:
.

__,_._,___


Read More :- "[wanabidii] The simplicity of China-Africa relations: HIVYO NDIVYO INAVYOTAKIWA"

[wanabidii] JESHI HILI JIPYA NI HATARI

'Jeshi' la  bodaboda ni tishio kuliko…

 

Na Joe Beda

UKISOMA kitabu cha historia cha 'Western Civilization' utagundua kuwa ukimya uliofanywa na mataifa ya Uingereza na Ufaransa karibu kwa miongo miwili kuanzia mwaka 1920 ndio sababu ya kuzuka kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Viongozi wa mataifa hayo wa siku hizo walikaa kimya na kuitazama Ujerumani ikifanya mabadiliko ya ndani ya uongozi, ikiimarisha jeshi lake na hata ikianzisha na kutekeleza sera ya kujitanua (kutanua mipaka-expansionism).

Hilo lilikuwa kosa, lakini kosa kubwa ni pale mataifa hayo yaliponyamaza tena wakati majeshi ya Adolf Hitler yalipokwenda Hispania kupigana bega kwa bega na majeshi ya waasi yaliyoongozwa na Jenerali Francisco Franco dhidi ya serikali.

Ama kweli, mzaha mzaha hutumbuka usaha kwani vita hiyo ya Hispania ilitumiwa na askari wa Hitler kama maandalizi ya vita nyingine kubwa iliyokuja kujulikana kama Vita Kuu ya Pili ya Dunia, miongoni mwa majanga makubwa kuwahi kutokea duniani.

Ni wazi viongozi wa mataifa hayo walikiri kuwa walistahili lawama kwa unyamavu wao ambao baadaye ulikuja kupewa jina la 'Appeasement Policy' kwani walipotahamaki waligundua kuwa kitendo cha kumnyamazia Hitler na kumruhusu kufanya atakacho kilimwongezea uchu mbabe huyo wa kivita na sasa Ufaransa na Uingereza walilazimika kumpiga (kama si kupigana naye).

Hali hii ndio kama inayoonekana sasa nchini mwetu ambapo vijana wanaoendesha pikipiki za kubeba abiria wanaojulikana kama bodaboda wanatazamwa tu wakijifanyia watakavyo kana kwamba wanaishi kwenye dunia yao!

Hakuna anayepinga kwamba kwa kiasi fulani pikipiki hizi ni msaada mkubwa kwa wengi huku pia zikiwa ni suluhu kwa tatizo la ajira kwa vijana, lakini kwa mwenendo wanaokwenda nao kwa sasa, ninaamini kuwa hili ni bomu ambalo linaweza kulipuka wakati wowote.

Hapa sizungumzii ajali zinazosababishwa na waendesha bodaboda kwani ninaamini hilo limeshasemwa kiasi cha kutosha, lakini lipo jingine ambalo hakika linatisha, linakera na kusikitisha sana.

Waendesha bodaboda karibu wote wanafanana wakiwamo wa Dar es Salaam, Mbeya na Arusha. Inavyoonekana vijana hawa wamejiundia 'jeshi' lisilo rasmi na wakati wowote mmoja wao akikosewa iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya, hujikusanya na kulipa kisasi papo hapo!

Si ajabu kwa sasa kuwaona bodaboda wakimshambulia dereva wa gari na hata kutishia kuchoma moto gari kisa, dereva huyo kamgonga mwenzao. Hapo hawatazami nani mwenye kosa ila ni kulipa kisasi tu.

Si ajabu hata kidogo kuona gari likipewa 'escort' na waendesha bodaboda hata 100 kuanzia Kibaha hadi Dar es Salaam kushinikiza dereva ashuke ili wampige! Sasa wamefikia hata hatua ya kuua askari! Jamani, bodaboda hawa wasiachwe hivi hivi.

Mwaka jana nilishuhudia maofisa wa wakala wa kukusanya kodi ya mapato TRA mjini Morogoro wakipata wakati mgumu walipotaka kuwatoza kodi waendesha bodaboda. Vijana wale waligoma, wakajikusanya kama 300 hivi, wakalizunguka gari la mawakala wale wakitishia kuwapiga na kulichoma moto gari lao. Hawataki kutoa kodi hawa, wanavunja hata sheria na haki ya Mungu.

Ilibidi dereva wa lile gari aondoke na maofisa wake, lakini wapi! Bodaboda zile ziliendelea kulisakama gari lile, wakalisindikiza hadi Kituo cha Polisi Morogoro, kisha waendesha pikipiki wale wakaondoka zao huku polisi wakiwatazama tu. Ndio, waliwatazama tu kwani kuwachezea ni sawa na kucheza na moto. Wanaweza hata kuvunja 'armory' ya polisi, usicheze na bodaboda.

Nikajiuliza, jeuri hii wanaitoa wapi? Kwanini wagome kulipa kodi na kulisindikiza gari hadi kituo cha polisi? Ni nani alipaswa kupelekwa polisi, wao kwa kugoma kulipa kodi au mawakala wa TRA kwa kuwataka walipe kodi? Hii ni hatari.

Nililazimika kuzungumza na askari mmoja ambaye alikiri kuwa kwa sasa bodaboda hao ni jeuri na tishio hata kwa maisha ya walinda amani, lakini yeye akawatupia lawama wanasiasa.

Kwamba wao ndio wanaowalinda kwa kuogopa kuwa 'jeshi la bodaboda' likiwa tofauti na vyama vyao huenda wakakosa kura kwenye uchaguzi wowote ujao.

Nilijiridhisha baada ya muda mfupi niliposhuhudia waendesha bodaboda wakitumiwa kwenye maandamano ya kisiasa na kiongozi wao mmoja alikiri kuegemea upande wa chama fulani.

Mimi sina tatizo kwa wao kuwa na upande wa kisiasa, lakini wasiwasi wangu ni kwamba jeuri waliyo nayo inatisha na wanaweza kuamua kufanya lolote na chochote wakati wowote bila kuogopa sheria wala walinda sheria.

Kingine kilichozuka ni matumizi ya silaha na vitendo vya mauaji vinavyofanywa na waendesha pikipiki. Wiki kadhaa zilizopita, waendesha bodaboda wamehusika kwenye mauaji ya madereva kwa kutumia silaha!

Inakuwaje bodaboda wanamiliki silaha? Lakini pia waendesha pikipiki hawa wamekuwa wakishiriki vitendo vya uporaji kwenye benki, mawakala wa vocha na hata watembea kwa miguu na kisha kutokomea zao.

Nchi haiwezi kuendeshwa namna hii. Ni lazima itafutwe namna ya kuwadhibiti waendesha bodaboda kwani umoja wao ni tishio kwa usalama wa raia na hata wa taifa zima.

Kwanini hawataki kushirikiana na polisi na kuwakamata madereva wa magari yaliyowasababishia ajali? Jibu ni kwamba, wao pia wana makosa mengi na wakifika kituoni lazima kibao kitawageukia.

Wengi wao hawana leseni za kuendesha vyombo vya moto, wengine pikipiki zao hazina bima, wapo ambao vichwa vyao vina mzio (allergy) ya kofia (helmet) na wapo ambao hawalipi na hawataki kulipa kodi ya mapato.

Na hili la kodi si la kuachwa hivi hivi. Iweje idadi kubwa namna hii ya vijana wafanye kazi bila kulipa kodi? Nani awalipie? Ni kodi hizi ndizo zinazosaidia kupatikana huduma za kijamii na maendeleo ya nchi kwa ujumla, na ni wajibu wa kila Mtanzania kulipa kodi.

Lakini ni nani anayewalemaza vijana hawa? Ni Serikali? Ni jeshi la polisi? Ni vyama vya siasa? Au ni jamii nzima?

Hakika kuendeleza 'Appeasement Policy' kwa hawa bodaboda kutaitokea puani serikali yetu pale itakapobidi kutumia nguvu ya ziada kurekebisha mienendo yao.

Lazima sote kwa pamoja tutafute suluhu ya ubabe wa mabodaboda.

0684 419 506 rupia.joseph@gmail.com

Mwisho

 

chanza: Gazeti la Rai; Machi 28-Aprili 3, 2013

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
Read More :- "[wanabidii] JESHI HILI JIPYA NI HATARI"

[wanabidii] WATANZANIA TUCHAPE KAZI TUACHE POROJO

Ndugu zangu

Sijui kama mmegundua kwamba Katika Afrika mashariki nchi ya Tanzania ndio inayoongoza kwa watu haswa vijana kurandaranda kwenye mitandao haswa ya kijamii zaidi Facebook , katika kutumiana salamu , mazungumzo tu na masuala mengine binafsi kuliko kujadili masuala mbalimbali haswa yale yanayogunsa maisha yao kama elimu , ulinzi , usalama ,kilimo .

Tabia hii imekuwa kubwa na inaleta janga lingine kwa taifa ambalo pengine limeanza kuchomoza katika utendaji kazi wa baadhi yetu haswa kule maofisini , mashuleni , vyuoni na katika baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama .

Kwa viongozi wa idara kama ni mashuleni basi wabadilike , kwa serikalini watengeneze miongozo kwa majumbani wazazi waangalie mienendo ya watoto wao katika matumizi ya vyombo hivi .

Kwa sisi tuliojiajiri haswa kwenye fani hii ya TEHAMA kama mimi nawaomba haswa vijana wenzangu tubadilike , tusiendeleze sana tabia hii , tuwe na muda maalum kwenye mitandao hii angalau tusipoteze nguvu ya taifa kubwa kwenye mitandao ya kijamii .



--
www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
Read More :- "[wanabidii] WATANZANIA TUCHAPE KAZI TUACHE POROJO"

[wanabidii] UVURUGWAJI WA MAKUSUDI ULOFANYWA NA MASHEHA KWA MCHAKATO WA KUYAPATA MABARAZA YA KATIBA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UVURUGWAJI WA MAKUSUDI ULOFANYWA  NA  MASHEHA KWA MCHAKATO WA KUYAPATA MABARAZA YA KATIBA

Leo nchi imeingia katika mchakato muhimu wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya kama sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 inavyoelekeza. Umuhimu wa kuwapata wajumbe hawa utakamilisha hatua ya tatu ya mchakato huo kabla ya hatua ya Bunge la katiba. Kwa uzito ulio mkubwa baada ya kukamilika hatua za kabla za utowaji wa maoni kwa njia mbali mbali hatua hii ni muhimu sana kwani inaweka msingi mkubwa wa kuupa uwakilishi wa wanachi kwenda kuipitia rasimu ya katiba iliyotokana na maoni yao.

Jambo la kusikitisha na kuhuzunisha ni kile kinachofanyika hivi sasa hapa Zanzibar cha kuuvuruga mchakato huu kwa makusudi na masheha ambao tume imewaachia  kufanya walitakalo kinyume na muongozo wa mchakato huu.

Kwamuhibu wa muongozo huo wa tume wajibu na majukumu ya sheha ni kama ifuatavyo:

  1. Kifungu cha 9.2.3.1. Kupokea majina ya wananchi wanaoomba kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.
  2. Kifungu cha 9.2.3.2. Kubandika katika maeneo ya wazi / matangazo majina yote ya watu walioomba kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.
  3. Kifungu cha 9.2.3.3. Kuitisha Mkutano wa Shehia utakaochagua Mwenyekiti na Katibu wa Mkutano.

Pamoja na Chama cha wananchi CUF kutoa angalizo kwa Tume mapema sana juu ya hatari ya kushirikishwa masheha na kuwalalamikia viongozi hawa wa serikali za mitaa kwa maandishi lakini Tume haikuchukua hatua. Tayari kile ambacho CUF kiliitahadharisha Tume kuhusiana na mamlaka ya viongozi hawa wa serikali za mitaa kimeshachukua nafasi yake kwa viongozi hawa kuuingilia kati na kuuharibu mchakato huu. 

Baadhi ya matukio machache tu katika mengi ambayo yameshuhudiwa hivi asubuhi yakionyesha jinsi masheha hawa wakishirikiana na wajumbe wao na viongozi wa CCM wakifanya vitendo vya kuuvuruga mchakato huu ni hivi vifuatavyo:-

  1. Katika vituo vyote vya Unguja, sheha na wajumbe wake ndio walioendesha na kuratibu zoezi hilo huku wakichukua mamlaka kadhaa kinyume na muongozo wa Tume.
  2. Katika shehia ya Chumbuni, sheha aliandaa vipande maalum na kuwapa watu wake maalum kama ndio utambulisho wa kushiriki katika mchakato huu kinyume na muongozo wa Tume.
  3. Katika Shehia ya Migombani, sheha ameamua kughairisha mchakato kwa siku ya leo baada ya watu kufika kwa wingi katika kituo akidai amapokea amri ya kufanya hivyo kutoka juu.
  4. Katika shehia ya Meya, sheha amegawa karatasi za kupigia kura zisizokuwa za kituo hicho huku akiwatoa wagombea watatu (3) walioomba nafasi hizo na na ambao walikuwemo katika orodha ya wagombea tokea awali. 
  5. Katika shehia nyingi ikiwemo ya Nyerere, sheha amelazimisha kutumiwa kwa ZAN ID kama shahada ya kushiriki mchakato huo ikiwa ni kinyume na muongozo wa Tume.
  6. Katika shehia ya Kiembe samaki, sheha amechukua mamlaka ya kuteua katibu wa mkutano wa shehia kinyume na muongozo wa Tume.
  7. Katika shehia ya Dimani, sheha ametangaza kumalizika kwa mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya katiba kwa madai ya kuishiwa na karatasi za kupigia kura.
  8. Katika shehia ya Kihinani, sheha amewataka wagombea kuondoka katika kituo na yeye peke yake akichagua Mwenyekiti na Katibu wa Mkutano wa shehia.
  9. Katika shehia ya Kibweni, sheha ndie aliyechagua Mwenyekiti na Katibu wa Mkutano wa shehia. Halkadhalika watu wengi kutoka nje ya shehia hiyo wamekuwa wakiorodheshwa na kushiriki upigaji kura.
  10. Katika shehia ya Kwerekwe, sheha amelazimisha uchaguzi ufanyike ndani ya nyumba yake badala ya kituo kilichopangwa kwa ajili hiyo jambo ambalo ni kinyume na muongozo wa Tume.
  11. Katika shehia ya Kwamtipura, sheha ametoa orodha ya watu wasio wakaazi wa shehia hiyo kushiriki katika uchaguzi huku akiwaacha wakaazi halali wa shehia hiyo.
  12. Katika shehia ya Mlandege, sheha ameteua Mwenyekiti na Katibu wa mkutano wa shehia kinyume na utaratibu, amewafuta wagombea anaodhani ni wa mrebgo kinyume na wake na kubakisha wagombea watatu (3) ambao ni wa mrengo wake. Pia sheha huyu amekua akiwakatalia wakaazi halali wasishiriki kuchaguliwa wala kuchagua kwa kisingizio si wakaazi huku akiruhusu watu wasio wakaazi kushiriki zoezi hili.
  13. Katika shehia za Kibweni na Kama masheha wakiwaruhusu askari wa KMKM kushiriki upigaji kura huku wakiwaacha wakaazi halali wa shehia hizo.

Kutokana na hali hii inavyoendelea ni uhalkika zoezi hili limekwisha kuharibiwa na huku ikizingatiwa Tume ina jukumu la kulinda na kusimamia haki za wananchi wote. Ili sheria ichukue nafasi yake na haki itendeke Tume lazima iliratibu upya suala hili na kuchukua mamlaka yake ili kuweza kuhakikisha zoezi linafanyika kwa taratibu zilizopo, kwa uwazi na kwa haki  bila ya wanachi kubaguliwa,  na  kuwapata  wajumbe   halali  kama  muongozo  wa  tume  ulivyoelekeza kushindwa  kuyasimamia haya hivi sasa ni  kuhakikisha  uchafuzi ambao  utaleta  dosari   kubwa katika  hatua   ya  kuwapata   wajumbe   wa  baraza   la  Wilaya   la  katiba .

HAKI SAWA KWA WOTE

………………………………

SALIM BIMANI
MKURUGENZI WA HAKI ZA BINADAMU, HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA

Headquaters P.O.Box 3637, Zanzibar, Tanzania Tel 024 22 37446 Fax: 024 22 37445
Main Office: P.O Box 10979, Dare s salaam, Tanzania: Tel 022 861009 Fax: 022 861010


Source: http://www.wavuti.com/4/previous/2.html#ixzz2PC9dQZNr

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
Read More :- "[wanabidii] UVURUGWAJI WA MAKUSUDI ULOFANYWA NA MASHEHA KWA MCHAKATO WA KUYAPATA MABARAZA YA KATIBA"

[wanabidii] Taarifa ya CCM-SA kuhusiana na tuhuma za utapeli wa Paul Mkoba

KUKANUSHA  TAARIFA ILIYOCHAPISHWA NA  JAMII FORUMS (TAREHE 28 MARCH 2013) KUHUSU UTAPELI ULIOFANYWA NA ALIYEHAWI KUWA KATIBU WA CCM, TAWI LA SOUTH AFRICA, NDUGU  PAUL PIUS ALBINO MKOBA

Mimi, kama mwenyekiti wa CCM, tawi la Afrika Kusini,  Ndugu, Kelvin Nyamori, nimesikitishwa na Habari, zilizochapishwa kwenye blogsite mbalimbali, pamoja na Jamii Forums, kuhusu utapeli uliofanywa na aliyekuwa katibu wa CCM, tawi la South Africa, Ndugu Paul Pius Albino Mkoba, Wenye Thamani ya Shilingi Millioni 37 za Kitanzania (RAND 200,000).

Napenda kuwaatarifu, Watanzania wenzangu waishio Afrika Kusini na kwengineko Duniani, kuwa taarifa zilizotolewa na vyanzo vya habari si sahihi, kabisa.

Chama hakiusiki kabisa na utapeli uliofanywa na ndugu, Paul Pius Albino Mkoba, ambaye alikuwa ni katibu  wa CCM, ila alikuwa na kampuni yake binafsi ya Investement (Forex & Stock Marketing) aliyokuwa akiimiliki, nchini South Africa, iliyosajiliwa kwa jina la mke wake, Betty Outsource Service.

Ila sisi kama Chama cha Mapinduzi, hatukuhusika na wala wanachama wetu hawakuhusika katika hiyo Biashara, na wala hakuwahi kutumia jina la chama katika kutangaza hiyo kampuni yake ya Investment, kama ilivyoripotiwa kimakosa na Jamii forums, na Blogsite nyinginezo.

Nimesikitishwa zaidi, na watu wa Jamii Forums kuichapisha hiyo habari ya mtuhumiwa huku wakiweka  picha ya mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtuhumiwa.

Ninachojua Rais ni kiongozi wa watu wote hivyo ana haki ya kusalimiana na hata kupiga picha na mwananchi yeyote yule. 

Napenda kuwaatarifu Watanzania wenzangu, sisi kama Chama cha Mapinduzi tawi la South Africa,

Tutawapa ushirikiano wa kutosha, waliotapeliwa na ndugu Paul Mkoba. Tumeshatoa taarifa ubalozini, na kituo cha polisi, tunamtafuta na kumsaka mtuhumiwa ili tumfikishe kwenye vyombo vya sheria, kwa kufanya utapeli kwa kutumia jina la chama kimya kimya. Kamati , Tulishafanya kikao cha dharura kumsimamisha kazi yake ya
ukatibu, baada ya kupata tarifa hizo, kutokana na malalamiko ya waliodhulumiwa, pamoja na vyombo vya habari.

Pia napenda kukanusha, kwa wale wanaosambaza taarifa kwamba mimi Mwenyekiti wa CCM, South Africa, kwamba nahusika na utapeli huo, ama kujua chochote kuhusu utapeli huo wa Mr. Paul Mkoba, uhusiano wangu na
Paul Mkoba ulikuwa ni kwa shughuli za kichama tu, na siyo vinginevyo kama watu wanavyonituhumu.

Hatukanushi tuhuma dhidi ya mtuhumiwa ila tunakunusha utapeli huo kuhusishwa na Chama Cha Mapinduzi, kama ambavyo Jamii Forums walivyoripoti.

Kwasababu kuu mbili.  Mosi  , Ndugu Paul Pius Albino Mkoba aliwadanganya wafanyakazi wa Ofisini kwamba anaenda Capetown kwenye semina ya kikazi (Forex & Stocks  Workshop) badala yake akaenda Tanzania kimya kimya.

Mwaka jana mwezi wa 9 Ofisi  ya Chama iliwahi kuibiwa vifaa vya ofisi vyenye thamani  karibu ya shilingi Millioni 15.
Ambavyo ni  Laptop  nne (4),  Giant Computers, Apple Macintosh mbili, pamoja na printer.

Wakati huo mimi kama mwenyekiti wa chama sikuwepo Johannesburg, nilienda kwenye shughuli za kichama   Western Cape. Nikaja kupokea simu kutoka kwa aliyekuwa katibu (Paul Mkoba) kwamba vifaa vya ofisi vimeibiwa.

Na yeye mwenyewe  ndugu Mkoba ndiye aliyezisambaza taarifa za ofisi za chama  kuibiwa kwa kutumia BBM na Facebook Page ya CCM. Ila uchunguzi wa polisi ulifeli, kutokana na mazingira ya wizi ulivofanyika. Napenda kuhitimisha kwa kuwaomba, Watanzania wenzangu waishio South Africa na Kwengineko, Wasipotoshwe na ripoti zisizo sahihi zilizotolewa na Jamii Forums na blogsite mbali mbali za nchini Tanzania.

Hawakufanya sahihi kumhusisha mtuhumiwa na Chama, kama alifanya dhuluma hiyo aliifanya kwa dhamira na hulka yake yeye mwenyewe na wala siyo Chama cha Mapinduzi.

Kwani inaonekana baadhi ya watu wanataka kuitumia habari hiyo kiuchochezi  zaidi.

Nawathibitishia Watanzania na wana CCM, wenzangu tuko  pamoja kumsaka na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria mtuhumiwa, kwa kutapeli kwa kutumia jina la chama kimya kimya, ambacho ni kinyume na taratibu na kanuni, popote duniani. Kwani kwa sasa hata Chama , hakijui wapi alipo mtuhumiwa.

Kwa ushirikiano zaidi kwa mtu atakayejua wapi alipo Ndugu Paul Pius Albino Mkoba asisite kuwasiliana na Chama Cha Mapinduzi South Africa, au kutoa taarifa kituo chochote cha polisi nchini Tanzania au South Africa

Tunaambatanisha picha ya mtuhumiwa kwa ushirikiano zaidi, Asanteni sana.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.

Mwenyekiti wa CCM Tawi la South Africa
Kelvin. A .Nyamori
Johannesburg  HQ
Phone: +27731688316
Email: Kelvinmartin39@hotmail.com
Or:  Mwenyekiti@ccmza.org

Source: http://www.wavuti.com/4/previous/2.html#ixzz2PC9KCzA9

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
Read More :- "[wanabidii] Taarifa ya CCM-SA kuhusiana na tuhuma za utapeli wa Paul Mkoba"

[wanabidii] Mtuhumiwa wa mauaji ya Padre Mushi ni CUF aliwahi kugombea ubunge 2010

IMEELEZWA kuwa, mtuhumiwa Omar Mussa Makame (35) anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kumuua Padri Evaristus Mushi ni mwanachama wa CUF ambaye aligombea nafasi ya uwakilishi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 katika Jimbo la Rahaleo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF).

Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Hamad Masoud alithibitisha jana kuwa, mtuhumiwa huyo ni mwanachama wao na alishiriki katika mchakato wa uchaguzi mkuu na kusimamishwa na chama katika kampeni za Uwakilishi Jimbo la Rahaleo.

"Ni kweli mtuhumiwa anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Padri Mushi ni mwanachama wetu na alishiriki katika mchakato wa kuwania Uwakilishi Jimbo la Rahaleo mwaka 2010.

Hata hivyo, Hamad alisisitiza na kusema suala la Omar kamwe lisihusishwe na CUF na kusema suala hilo watalitolea tamko baadaye.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ripoti ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Jimbo la Rahaleo, mgombea wa CCM, Nassor Salim Ali maarufu kama Jazirra aliibuka na ushindi kwa kupata kura 3,952 sawa na asilimia 63.10, wakati mgombea wa CUF, Omar Mussa Makame alipata kura 2,310 sawa na asilimia 39.9 na kushika nafasi ya pili.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Jeshi la Polisi, Mussa Ali Mussa mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kukamatwa kwa Omar kunatokana na michoro ya teknolojia ya kisasa chini ya msaada wa upelelezi wa makachero kutoka FBI ambayo iliweza kutambua sura yake.

Uchunguzi zaidi uliofanywa na gazeti hili (HabariLeo) umegundua kwamba mtuhumiwa huyo licha ya kuwa mfuasi wa CUF, mama yake mzazi ni kada wa CCM. Mama yake, Tatu Sheha mkazi wa Mkele, Unguja ni Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi wa CCM katika Jimbo la Kwamtipura. Tangu kuibuka kwa kadhia hiyo inayomhusu mtoto wake, mama mzazi amekosa raha na faraja kiasi ya kushindwa kuhudhuria vikao vya chama kwa takribani wiki mbili sasa.

Baadhi ya wananchi Zanzibar wamepongeza juhudi za Jeshi la Polisi za kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, wakisema ni dalili njema za kutaka kukomesha matukio ya mauaji kisiwani Zanzibar.

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2PC8ymBTp

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
Read More :- "[wanabidii] Mtuhumiwa wa mauaji ya Padre Mushi ni CUF aliwahi kugombea ubunge 2010"