Tuesday, 21 June 2016

[wanabidii] MERCY KITOMARI: MJASIRIAMALI KIJANA ANAYEFIKIRIA MAKUBWA

Habari za asubuhi,

Tafadhali pokea CODES hapa chini.

Mjasiriamali kijana Mercy Kitomari akiwa ofisini kwake wakati wa mahojiano.

Modewjiblog ilipata bahati ya kuzungumza ana kwa ana na Mercy Kitomari mmoja wa wajasiriamali wanawake vijana ambaye anafikiria kuwa na kiwanda kikubwa cha ashkrimu (ice cream) ifikapo mwaka 2020 akizisafirisha na kuziuza Tanzania nzima na Afrika Mashariki. Wapi alipotokea, yuko wapi kwa sasa, ni machungu gani aliyokumbana nayo na anaishauri nini serikali na wajasiriamali wenzake. Haya yote utayajua katika mahojiano haya .Soma…

MODEWJI BLOG: Role model wako nani?

MERCY: Magufuli. You know why?(unajua kwanini?) ametuweka wazi kabisa kwamba maisha ni changamoto na tusikubali kushindwa ni lazima kupambana na kufanyakazi kwa bidii na maarifa kuondoa vigingi vyote vinavyotukwamisha. Amenifanya nifanye kazi kwa bidii. Nataka kuwa mwanamke anayefanya mabadiliko. Hakuna kitu kinachokuja kirahisi. Nataka kuwa mwanamke yule ambaye anaonesha tofauti nataka kuifanya nchi yangu iniringie.

Sijisikii vibaya kwa kuwa niko mpweke, kitu cha kwanza ni kazi, nataka kuifanya mwenyewe ili wanawake wenzangu watambue kwamba tunaweza kufanya wenyewe, bila msaada wa mwanaume. Ndio unahitaji mume lakini si katika hili suala la ujasiriamali, mwanamke peke yako unaweza kuleta mabadiliko.

Nataka kuwa mwanamke ambaye Afrika itaniringia na taifa langu litanichekelea kwamba mimi ni binti yao.

MODEWJI BLOG: Turejee katika masuala ya kodi. Kodi ni muhimu sana kwa mapato ya serikali. Je Kodi zinazowatoza zinawasaidia au zinawavunja moyo?

MERCY: To be honest (kusema ukweli) zinatuvunja moyo. Nyingi ya hizi kodi hazitusaidii sisi watu wa hali ya chini kunyanyuka, zinatukwamisha.Kodi zimewekwa bila kujali madaraja. Anayeanza na aliyemo, mwenye kipato kidogo na kikubwa. Na yote hayo yanafanyika bila kuzingatia kwamba kuwapo kwa wajasiriamali wengi ndio kuchangamka kwa soko la wakulima na pia ajira viwandani.

Mimi ninayetengeneza ashkrimu natengeneza ajira; ninatengeneza soko kwa yule anayeleta matunda sokoni kwani naenda kununua matunda kwa ajili ya ashkrimu. Kodi nyingi zinakandamiza, haziangalii ukubwa na udogo wa biashara. Mtu anabiashara inayoingiza mamilioni kwa siku anawekwa kundi moja na anayeingiza laki moja.

Muonekano wa nje wa duka la Ice Cream la Nelwa's Gelato la Mercy Kitomari lililopo ndani ya Petrol Station ya SOPCO barabara ya Morogoro-Magomeni Mwembechai karibu na kwa Sheikh Yahya.

MODEWJI BLOG: Ukikutakana na role model wako utamuomba nini?

MERCY: Nikikutana na Magufuli? Kwanza naomba nikutane naye! Nikikutana naye nitamwambia ofisi zote za huduma kwa wananchi ziwe katika mtandao (online) watu tuweze kufanya kila kitu katika mtandao. Na Serikali za mitaa lazima zirejeshe faida kwa wananchi kwa kodi zao.

Wanatakiwa watufundishe vitu vingi. Watufundishe kuwa wajasiriamali namna ya kufunga na kuuza bidhaa zetu wasifanye tu shughuli za kukusanya ushuru na kodi, watuambie namna ya kuendelea mbele ili waendelee kukusanya ushuru na kodi au hawatakusanya kitu tukikwama.

Ni lazima wawekeze kwa wajasiriamali ili kuwepo na hali bora zaidi.

Ukitazama soka katika televisheni unaona matangazo mengi ya krisp hapa kwetu wapo wadada wanaotembeza za ndizi au viazi hawa wakifundishwa namna nzuri ya kuweka chakula chao ni dhahiri tutakuwa na wajasiriamali wengi. Wanatakiwa watuelekeze mambo mengi bidhaa za kwenye 'super market' zinakuaje na kadhalika wasibaki kudai na kuvuna hela tu watusaidie tuweze kuwapatia fedha zaidi. Lakini nambieni lini nitakutana na role model wangu huyu…….ha ha ha ha….kicheko….!

MODEWJI BLOG: Wasaidizi wake wakisoma makala haya watajua nini unahitaji na pasi shaka watakukutanisha naye.Ni watu wema hawa, hawawezi kukosa kukupangia muda wa kumuona Role Model wako umweleze mambo ya kukusaidia wewe na wengine wa aina yako.

MERCY: Nakudai hilo kwani natamani sana atukutanishe wanawake vijana wajasiriamali ili azungumze nasi. Najua ameshazungumza na wafanyabiashara wakubwa, lakini akituona na sisi atatambua uwezo wetu na namna ambavyo angetusaidia tungeibuka wengi na kuweka ndoto ya Tanzania ya viwanda katika ukweli.

You know (unajua) nilikutana na wanawake wenzetu wajasiriamali kutoka Uganda na Rwanda naona wameendelea kwelikweli na siri ni serikali zao kuhakikisha kwamba wanaendelea.

Wapo wanawake waliokata tamaa hapa, nimekutana nao nikasema tusichoke hata kidogo serikali ya sasa inataka viwanda ni lazima kuisaidia kujua tunawezaje kufikia ndoto hiyo, kuna vizingiti hapa wakiviondoa tutaweza.

Hatupaswi kukata tama hasa kutokana na serikali ya sasa kutaka kuwapo na viwanda.

Kusoma mengi na mengine kuhusu safari ya Mjasiriamali Mercy Kitomari bofya link hii

Zainul A. Mzige,
Operation Manager,
MO BLOG,
+255714940992.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment