Tuesday, 21 June 2016

RE: [wanabidii] Ukawa wanavyodharau Bunge, Viongozi wake

Demokrasia huanzia ndani ya vyama. Huku kwenye wakawa miaka Nenda miaka rudi sterling ni wale wale, wabunge Wao, wenyeviti Wao na Mara nyingine likija la Urais wagombea ni Wao wale wale kwa miaka kadhaa. baadhi ya nafasi ziko special kwa wenyewe tu! Wakati Chama kikubwa wanaendelea na mchakato wa kukabidhi madaraka kwa mwingine au kwa namna ambavyo tumekuwa tukishuhudia wakikabidhi madaraka katika nyadhifa mbalimbali, hutokaa ulione CUF NCCR au CDM maana huko wenyeviti ni miungu watu! Wanaamini wakiondoka kwenye nyadhifa hizi vyama vyao vitakufa  na wamewekeza nguvu nyingi kuzilinda nafasi hizi. Mwenyekiti ndiye mwenye mamlaka kuamua nani agombee nini na wakati gani km tulivyoona kwenye uchaguzi uliopita. Kumpitisha ENL hayakuwa maamuzi ya wote ila wachache kwa maslahi Yao. Hii ilitufanya tulio wengi tukengeuke tumchague mtu badala ya Chama. Ile dira ya mabadiliko tuliyokuwa tukiiamini ilibadilika ghafla. Leo hii ikitokea muumba akamchukua mmojawapo wa wenyeviti Hawa tutashuhudia madudu sababu Hakuna succession planning kwenye nafasi za juu kwao vyama hivi ni more of personal properties ambako power iko vested kwa wachache tu. Ni vyama vya watu Fulani Fulani na huu ni uhuni tu!

From: 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii
Sent: ‎22/‎06/‎2016 05:19
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Ukawa wanavyodharau Bunge, Viongozi wake

Kamala. Kosa halikuwa la CHADEMA kama chama. Kosa lilikuwa kumwachia mfanya biashara (Mbowe) kumuuzia Lowasa chama na wenye akili kama Lipumba na Slaa wakaamua kuupisha upuuzi. Japo wanasema wanatetea demokrasia kila mtu aliona ambavyo waqla demokrasia haikutumika kuwaleta wahamiaji haramu na ikabidi wenye akili (Lipumba na Slaa) wajiengue. Lesian haelewi kitu. Yeye ni Edo mwendo mdundo. Hypnosis aliyoipata kwa edo inahitaji wataalau wasiopatikana nchini kumtibu
--------------------------------------------
On Sun, 6/19/16, 'Lesian' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Ukawa wanavyodharau Bunge, Viongozi wake
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, June 19, 2016, 9:39 PM

Slaa hana tofauti na
lipumba wana njaaa...cdm iliwaza mbli sana kuliko mnavyoona
nyie, ni chama dedicated kuongoza dola na sio kulete
upinzani toka miaka nenda rudi ka a akili za slaa na lipumba
zilivyoo mzee mhingo
Unaoelewwa
politics,cdm imecheza sana kuwakubali hawa jamaa ni sawa
kusajili  messy na ronaldo  yanga....ndio maana mnaumia sana
mioyo.....
  Ndio maana serikali ya leo
inatumia nguvu nyiingi sana kuongoza than kutumia akili
kidogo tu,tena wana miss use jesho letu la polisi kila simu
wakiona bebdera tu ya cdm wanapeleka police,why simply ni
chama tishio kubea dla 2020
So walionabali
sana kuliko nyie msivyoweza kung'amua mzee elisa na kina
kamala kwa kua mmekunya maji ya bendera ya ccm na hata mkifa
njaa mko tayar kutetea

J L
Kamala <jlkamala@gmail.com> wrote:

Mzee muhingo.
Asante kwa clarification "chadema
iliyokuwa inaongozwa na Dr Slaa" sijui waliwaza nini
kukubali kumpoteza huyu mtu na kutuletea akina Sumaye na
Lowasa
On Jun 19, 2016 12:37 PM,
"'ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Kama
watanzania wangefanya kosa tarehe 25 October na kukiweka
madarakani chama chenye wabunge kama hawa. na hawa wakatokea
kuwa mawaziri. Nchi ineelekea wapi. Tunahitaji kujifunza
namna nyingine ya kuvilea vyama vya siasa vifikie kuweza
kuongoza. CHADEMA iliyokuwa ikiongozwa na Dr. Slaa
imeporokoka na kukosa nidhamu kiasi hiki. Tunayo safari na
si fupi.

--------------------------------------------

On Sun, 6/19/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:



 Subject: [wanabidii] Ukawa wanavyodharau Bunge, Viongozi
wake

 To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>

 Date: Sunday, June 19, 2016, 9:40 AM



 WAKATI

 Bunge likitarajiwa kupitisha Bajeti ya Kwanza ya Serikali
ya

 Rais

  John Magufuli kesho, bila uwepo wa Kambi ya Upinzani,

 gazeti hili

 limefanya tathmini ya baadhi ya matukio yaliyoanza

 kuongezeka

 kutoaminiana kati ya kambi hiyo na uongozi wa Bunge,
hasa

 Naibu Spika,

 Dk Tulia Ackson.







 Ingawa taarifa nyingi zimekuwa zikieleza kuwa Dk Tulia
ndiye

 mbabe,

 taarifa za uendeshaji wa shughuli za Bunge tangu
mwanzoni

 mwa mwaka huu,

  zinaonesha namna wabunge wa Ukawa, walivyoonesha
kutojali

 heshima ya

 chombo hicho na viongozi wake.







 Taarifa hizo za Bunge zilizopitiwa na gazeti hili wiki
hii,

 zimeonesha

 bila kuacha shaka namna baadhi ya wabunge wa kambi
hiyo,

 wanavyodharau

 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mtu yeyote

 aliyekalia Kiti

 cha Spika, achilia mbali Dk Tulia ambaye ndiye
anayetajwa

 zaidi kuwa

 mbabe.







 Mbali na dharau kwa Bunge na viongozi wake, wabunge hao

 wameonesha namna

  walivyotayari kutumia ubabe ndani ya Bunge ikibidi

 kupigana, huku

 wengine wakitumia uongo kwa nia ya kuichafua serikali
na

 viongozi wake

 kwa umma.







 Dharau za Bulaya







 Mbali na matukio ya mara kwa mara na ya kawaida ya
wabunge

 hao wa Ukawa

 kukaidi agizo la kutakiwa kukaa chini au kukaa kimya
kutoka

 kwa

 aliyekalia Kiti cha Spika, ambaye ndiye anakuwa na
Mamlaka

 ya Spika,

 dharau kubwa iliyosikitisha viongozi wa Bunge, ilioneshwa
na

 Mbunge wa

 Bunda Mjini, Esther Bulaya.







 Mbunge huyo baada ya kuonekana kushiriki kufanya vurugu

 Januari 27, 2016

  wakati wabunge hao wa Ukawa walipozuia shughuli za Bunge
za

 mchana na

 jioni kutofanyika kwa kusimama na kupiga kelele
mfululizo,

 yeye na

 watuhumiwa wenzake walitakiwa kufika mbele ya Kamati ya

 Haki, Maadili na

  Madaraka ya Bunge, kutoa maelezo kuhusu tuhuma
zilizokuwa

 zikiwakabili.







 Watuhumiwa wengine walioitwa mbele ya kamati hiyo Machi
9

 mwaka huu, kwa

  kutumia hati ya wito yenye nguvu sawa na ya Mahakama,
ni

 Mbunge wa

 Singida Mashariki, Tundu Lissu; Mbunge wa Arusha Mjini,

 Godbless Lema na

  Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul. Pamoja na

 kuthibitisha kuwa

 Bulaya na watuhumiwa wenzake walipokea hati hiyo, ni
mbunge

 huyo pekee

 wa Bunda ambaye hakufika na wala hakuona umuhimu wa
kutoa

 taarifa yoyote

  ya kutofika kwake.







 Kwa kutumia nguvu ya kisheria ya kamati hiyo ambayo ina

 hadhi sawa na ya

  kimahakama, Kamati hiyo ililazimika kumwandikia Spika
barua

 kumjulisha,

  kuhusu hatua ya Bulaya kukaidi wito wa kamati.







 Kukamatwa kwa Bulaya







 Spika wa Bunge, Job Ndugai, hakuwa na namna bali kutoa

 kibali chake cha

 kukamatwa kwa Bulaya, kilichokabidhiwa kwa Inspekta
Jenerali

 wa Polisi

 (IGP) na polisi walifanya kazi yao, walimkamata Mbunge
huyo

 akiwa katika

  Hoteli ya Gold Crest, Mwanza.







 Akiwa chini ya ulinzi wa Polisi, Bulaya alipandishwa
ndege

 na kupelekwa

 jijini Dar es Salaam Machi 11, 2016 kwenda kujibu
tuhuma

 zilizokuwa

 zikimkabili.







 Utetezi wa Bulaya







 Taarifa za Bunge zinaonesha Bulaya alipewa fursa ya

 kujitetea kwa nini

 hakutii wito wa Kamati ya Bunge, kama walivyofanya

 watuhumiwa wenzake

 ambao nao ni wabunge kama yeye, ambapo mbunge huyo
alitoa

 utetezi wa

 aina mbili uliokuwa ukipingana.







 Kwanza Bulaya alidai kuwa alikuwa anaumwa na kwamba
kwake

 yeye suala la

 afya yake, lilikuwa muhimu zaidi kuliko kutii wito huo
wa

 kamati. Katika

  utetezi wa pili alioutoa baada ya Kamati hiyo
kumdadisi,

 alijikuta

 akiacha hoja ya ugonjwa na kukiri kuwa alikuwa Mwanza

 kuhudhuria mkutano

  wa Kamati Kuu ya Chadema, kama mjumbe mwalikwa.







 "Kamati ilisikitishwa na kitendo cha Mheshimiwa
Bulaya

 kudharau wito wa

 Kamati," taarifa rasmi za Bunge zimemnukuu Mwenyekiti
wa

 Kamati hiyo,

 Mbunge wa Newala, George Mkuchika (CCM).







 Dharau zaidi, busara ya Bunge Pamoja na Lema, Lissu na
Gekul

 kutii wito

 wa kwanza ambao Bulaya alikaidi, katika tukio
lililoonesha

 dharau

 nyingine kwa Bunge, ni pale wabunge hao waliotii wito
wa

 kwanza

 walipoomba kupewa muda ili washauriane na mawakili wao,

 kabla ya kujibu

 tuhuma zilizokuwa zikiwakabili.







 Kwa busara, Kamati hiyo iliamua kuwapa wabunge hao haki
yao

 ya

 kusikilizwa iliyotimia kwa kuwapa muda wa siku mbili
zaidi,

 ili

 wawasiliane na kupata ushauri wa mawakili ambapo
walitakiwa

 kurudi

 katika Kamati Machi 11, 2016 ili kujibu tuhuma zao baada
ya

 kupata

 ushauri wa mawakili.







 "Kamati iliamua kutoa fursa kwa mashahidi walioomba
kupewa

 fursa ya

 kupata mawakili. Mashahidi hao ni Tundu Lisu, Godbless
Lema

 na Pauline

 Gekul. Kamati iliwapa muda wa siku mbili toka Machi 9
hadi

 Machi 11,

 2016 ili kuwawezesha kupata mawakili kama
walivyoomba,"

 ilieleza taarifa

  hiyo ya Bunge.







 Katika tukio linaloonesha dharau 'iliyopangwa' kwa

 Bunge, wabunge hao

 watatu waliamua kutofika kati tarehe waliyokubaliana
kuwa

 wangefika

 mbele ya Kamati na hawakuwahi kuwasilisha maelezo
yoyote

 mbele ya

 Kamati, kuhusu sababu za kushindwa kufika.







 Busara ya Kamati hiyo, haikuelekeza kutumia kibali cha

 kuwakamata, bali

 ilielekeza kwamba kwa kuwa walipewa fursa ya kutosha ya

 kusikilizwa na

 walifahamishwa kuwa wakishindwa kufika, kamati itaendelea
na

 kazi zake,

 Kamati hiyo ikaendelea kujadili tuhuma zao bila kupata

 utetezi wao.







 Ubabe







 Wakati anayetajwa zaidi kwa ubabe ni Dk Tulia, lakini

 wabunge hao wa

 Ukawa na hata Kabwe Zitto wa ACT, mbali na kuonesha
dharau

 iliyolazima

 viongozi wa Bunge kutumia busara kuwa nao, wamekuwa

 wakitumia ubabe na

 kelele zenye lengo la kuzuia Bunge kufanya shughuli zake
na

 dhidi ya

 aliyekalia Kiti cha Spika.







 Ubabe wa hali ya juu uliowahi kuoneshwa ndani ya Bunge
hilo,

 ulifanywa

 na Lema, ambaye aliwahi kabisa kuvua koti na tai tayari

 kupigana, huku

 akisema yuko tayari kuuawa akigombea haki.







 Taarifa za Bunge zinaonesha siku waliyofanya vurugu,
Lema

 "alivua koti

 na tai, ikiwa ni ishara ya kujiandaa kupigana, jambo
ambalo

 halitegemewi

  kufanywa na kiongozi wa hadhi ya Mbunge.







 "Mimi wataniua, hapa tunagombea haki," alisikika
Lema

 akisema huku

 amevua koti na tai hatua ambayo imetafsiriwa kuwa
"utovu

 wa nidhamu wa

 hali ya juu kwa Mamlaka ya Spika ambao haupaswi
kuvumiliwa

 kwa vyovyote

 vile…" Mbali na Lema, Zitto alionekana akipiga kelele
na

 kubishana na

 Spika mfano: Spika: Naomba waheshimiwa mkae.







 Zitto: (Akikaidi agizo la Spika) Mheshimiwa Spika, Hoja
ya

 hadhi ya

 Bunge. Spika: Naomba sana mkae, naomba nichukue nafasi
hii

 kumkaribisha

 Mwenyekiti, Mheshimiwa Andrew Chenge, ili aendelee na
ratiba

 iliyoko

 mezani. Mheshimiwa Chenge.







 (Anaita Spika) (Makofi).







 Zitto: (Akitumia ubabe) Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya

 kuahirisha

 mjadala… Mwenyekiti: Mheshimiwa Zitto nakusihi sana,
hiyo

 Kanuni ya Haki

  za Bunge, hailazimishi Kiti kukubali kama ilivyo,
nakusihi

 isome

 vizuri. (Makofi).







 Zitto: Kanuni ya 69 hoja ya kuahirisha mjadala
Mheshimiwa

 Mwenyekiti.

 Taarifa za Bunge zinaonesha kuwa matukio kama hayo

 yamefanywa pia na

 Mdee na Lissu, ambaye wakati fulani alikuwa
akihamasisha

 wabunge wote wa

  Ukawa wasimame, wakati aliyekalia Kiti cha Spika,

 amekataza.







 Lissu: Mwongozo wa Mwenyekiti… Simameni basi.







 Mwenyekiti: Ni mwongozo tu, wote mnataka mwongozo?







 Wabunge wengi: Ndiyo.







 Mwenyekiti: Unafanana na hili alilosema Mheshimiwa
Heche?







 Lissu: Si mnataka mwongozo, simameni muombe mwongozo.







 Mwenyekiti: Waheshimiwa wabunge, naona sasa tunataka
kutumia

 utaratibu wa kuchelewesha shughuli za Bunge.







 Lissu: Mwongozo, mwongozo, tunataka mwongozo.
Mwenyekiti:

 Nimesimama (Kanuni inataka wote wakae).







 Lissu: Mwongozo (anakaidi).







 Mwenyekiti: Nimesimama. (Akisihi). Matumizi ya uongo
Mbali

 na dharau,

 vurugu na ubabe juzi taarifa nyingine ya Bunge
iliwashika

 wabunge wa

 Viti Maalumu wa Ukawa, Susan Lyimo na Anatropia Theonest
kwa

 kusema

 uongo.







 Susan alipokuwa akichangia mjadala wa Hotuba ya Wizara
ya

 Afya,

 Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mei 11
mwaka

 huu, alidai

 kuwa Serikali imenunua magari 777 ya 'washawasha',

 ambapo alidai kuwa ni

  magari 50 tu yaliyotumika kwenye uchaguzi.







 Alipotakiwa kufuta kauli alionesha kuwa anao ushahidi,

 alipotakiwa

 kuupeleka, alitumia ushahidi aliodai ni wa Mwananchi
Online,

 taarifa

 rasmi za Bunge, taarifa za mtandao wa Alibaba na
kielelezo

 kutoka

 Habarikablog. blogspot.com.
Hata hivyo vielelezo hivyo,

 vilipofanyiwa

 uchambuzi hakukuwa na kielelezo cha Mwananchi Online,
bali

 cha

 Mwanahalisi Online na pia kielelezo cha Habarikablog.

 blogspot.com

 hakikuainishwa.







 Pili hakukupatikana kielelezo hata kimoja
kilichothibitisha

 kuwa

 Serikali imenunua magari hayo 777 ya 'washawasha'.

 Anatropia Anatropia

 yeye katika kusema uongo, alidai bungeni kuwa Waziri wa

 Ardhi, Nyumba na

  Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipokuwa Mkuu wa
Mkoa

 mwaka 2011,

 alihusika na uporaji wa maeneo ya wananchi yaliyopo

 Tegeta.







 Mbunge huyo wa Ukawa alidai kuwa maeneo yaliyoporwa na

 Lukuvi, yalikuwa

 ya wananchi waliokuwa wakiishi mabondeni, wakiwemo wa
Jimbo

 la Segerea

 na wananchi wa Ilala, ambao sasa wanataka maeneo yao
huku

 wakidai kuwa

 Lukuvi alihusika kuyapora.







 Kutokana na uongo huo, Lukuvi alilalamika kuwa mwaka
2011,

 alikuwa

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na
Bunge

 na si Mkuu

 wa Mkoa wa Dar es Salaam na wala hakuhusika na tuhuma

 hizo.







 Katika malalamiko yake, taarifa za Bunge zinaonesha
kuwa

 Lukuvi alisema

 tuhuma zilizotolewa na Anatropia, si tu kwamba zilikuwa
za

 uongo, bali

 pia zimemfedhehesha kwa kumhusisha na uporaji wa viwanja
vya

 watu

 wanyonge.







 Akiri ni muongo Alipoitwa Anatropia taarifa za Bunge

 zinaeleza; "alikiri

  mbele ya Kamati kuwa alisema uongo bungeni kwa kuwa ni

 kweli Lukuvi

 hakuwa Mkuu wa Mkoa mwaka 2011, hivyo asingeweza kuhusika
na

 uporaji wa

 viwanja vya waathirika wa mafuriko."







 Anatropia ameelezwa katika taarifa hiyo kuwa, iwapo

 angeambiwa jambo

 hilo akiwa bungeni, kuwa kauli aliyokuwa ameitoa siku
hiyo

 ilikuwa ya

 uongo angeifuta.







 Kutokana na vitendo hivyo, ingawa wabunge wa Ukawa
wanasema

 Bunge

 linaongozwa kibabe, lakini ilibidi Bunge litoe adhabu

 mbalimbali za

 kinidhamu kwa wabunge saba wa Ukawa na Zitto wa ACT.
Mbali

 na Zitto,

 wengine waliopewa adhabu ni Susan, Anatropia, Lema,
Heche,

 Mdee, Gekul

 na Bulaya.







 Chanzo habari Leo

  







 --



 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com



  



 Kujiondoa Tuma Email kwenda



 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya

 kudhibitisha ukishatuma



  



 Disclaimer:



 Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility

 for any legal consequences of his or her postings, and
hence

 statements and facts must be presented responsibly.
Your

 continued membership signifies that you agree to this

 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.



 ---



 You received this message because you are subscribed to
the

 Google Groups "Wanabidii" group.



 To unsubscribe from this group and stop receiving
emails

 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.



 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com



Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma



Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree

[The entire original message is not included.]

0 comments:

Post a Comment