Kuna tatizo la msingi katika jinsi yetu ya kufikiri. Wakati naamini umuhimu na haki ya wananchi kuhabarishwa, siungi mkono gharama zisizo za lazima kwa sababu tu nataka kuhabarishwa. Juzi tulilalamika kwa TBC kurusha harusi live, watetezi wa TBC walisema TV hii inahitaji kujiendesha, ruzuku wanayoipata ni ndogo. Sheria ya TCRA pia hairuhusu TV kuuza matangazo wakati wa wanarusha shughuri za Bunge. Katika hali hiyo hivi kweli hatuoni bajeti ya billioni 4 ingefanya nini kuboresha TBC kwa kutopeleka matangazo hayo live? Kama redio zinaweza kutangaza moja kwa moja na tukaweza kusave hiyo pesa, ni kitu gani kinawafanya wabunge wetu kufikiria kuwa tunaweza afford hiyo anasa? Angalizo, serikali imeona kuachana na live coverage ni njia mujarabu ya kubana matumizi, na kama kweli tunafikiria ni suala muhimu, basi ni jukumu letu kama wananchi kuunga jitihada hizi, tukisubiri wanasiasa wataendelea kubariki matumizi yasiyo ya lazima ya serikali kwa kisingizio cha kulinda "haki ya wananchi".
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment