Taarifa kwa Vyombo vya Habari
- Ni kupitia huduma ya M pesa
- Watu wazima kulipa 2500/- kwa siku na watoto 500/-
- Tiketi za kupaki magari madogo kwa siku ni 4000/- maroli ni 40000/-
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bi. Anna Florence Bulondo amesema viingilio vya mwaka huu havina tofauti na vya mwaka jana lakini sasa yamefanyika maboresho ikiwa ni pamoja na ukataji wa tiketi kwa njia ya Kielectroniki na kwa njia ya M -pesa.
"Viingilio vya mwaka huu ni Shilingi elfu 2500 kwa watu mzima na shillingi 500 kwa watoto kila siku isipokuwa siku maalum ya tarehe 7 ambapo viingiio vitakuwa shilingi 3000 kwa watu wazima na watoto shilingi 1000." Alisema Bulondo.
"Kwa watakao hudhuria maonyesho hayo na magari madogo watatakiwa kununua tiketi kwa shilingi 4000, kama ambavyo mchanganuo wa malipo unavyobainisha malipo ya huduma nyingine zikiwemo za kupaki magari kama malori na magari makubwa pamoja na huduma nyingine."
Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo aliongeza kuwa, katika maonesho ya Mwaka huu, Usalama umeimarishwa kwa kiasi kikubwa na kutakuwa na Ulinzi wa Uhakika pamoja na Camera maalum zitakazo wekwa katika mageti na sehemu mbalimbali kuzunguka maeneo yote ya maonesho.
Kwa Upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, amesema kwa mwaka wa pili sasa wameendelea kuwawezesha watu, kufanya malipo ya tiketi kwa njia ya M pesa.
"M pesa inaendelea kurahisisha maisha ya Watanzania na mwaka huu, watu wote watakao kuja katika maonesho haya tumewawezesha kulipa viingilio kupitia M pesa na pia kufanya manunuzi na kulipa kwa M pesa katika banda letu la Vodacom." Alisema Twissa.
Malipo ya ada binafsi.
- Kwa siku - watu wazima (siku za kawaida) – 2,500/-
- Kwa siku- watoto (siku za kawaida) – 500/-
- Kwa siku – watu wazima (siku ya SabaSaba) – 3,000/-
- Kwa siku – Watoto (siku ya SabaSaba) – 1,000/-
- malipo kwa kipindi chote cha maonyesho - Beji kwa wahusika wa maonyesho - 20,000/-
- Beji kwa wahusika wa maonyesho (maeneo) – 3,000/-
- Kwa siku (magari madogo) - 4,000/-
- Kwa kipindi chote cha maonyesho – 30,000/-
- Malipo kwa pamoja – 200,000/-
- Tiketi za maegesho maalum – 400,000/-
- Malori na magari makubwa – 500,000/-
- Malipo ya kuegesha magari nje ya viwanja vya saba saba – 1,500/-
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment