Sunday, 1 June 2014

[wanabidii] Sitisho la shindano la TMT kutokana na msiba wa George Tyson

TAARIFA KWA UMMA

Kampuni ya Proin Promotions Limited ambayo ni waandaaji na waendeshaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents inapenda kuutangazia umma wa Watanzania na wadau wote wa tasnia ya maigizo Tanzania kuwa imepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za msiba wa Mtayarishaji na Muongozaji mahiri wa vipindi vya runinga na filamu, Ndugu George Tyson ambaye alifariki dunia tarehe 30 Mei 2014 kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Gairo mkoani Morogoro akiwa njiani kurudi Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa kabla ya taarifa hizo za msiba kupatikana, Shindano la Tanzania Movie Talents lilikuwa linaendelea katika Kanda ya Pwani ambapo usaili ulianza tarehe 30 Mei 2014 saa mbili asubuhi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo Jijini Dar es Salaam. Kutokana na msiba huu ambao pia umemgusa

moja kwa moja mmoja wa majaji wetu katika Shindano hili Bi Yvonne Cherry au Monalisa ambaye marehemu alikuwa mzazi mwenza, na walibahatika kupata mtoto mmoja aitwaye Sonia, tunapenda kuutangazia umma na wadau wa tansia ya filamu Tanzania kuwa, sisi kama wadau wa filamu Tanzania tumeamua kusitisha usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents kwa Kanda ya Pwani mpaka pale msiba utakapomalizika.

Tunapenda kutoa pole kwa familia ya marehemu George Tyson, kwa Jaji wetu Yvonne Cherry
na kwa wadau wote wa tasnia ya filamu Tanzania. Hakika tumempoteza mtu mahiri katika tasnia hii ya filamu na vipindi vya Televisheni. 

Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi.

Amina.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment