JORUM ABDALLAH MBOGO
MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA
S.L.P 63010
DAR ES SALAAM
TANZANIA
Ndugu,
YAH: MAOMBI YA UFAFANUZI WA KIKATIBA JUU YA UVUNJIFU WA KATIBA NA YA CHAMA UNAOFANYWA NA VIONGOZI
Mheshimwa Msajiri, Somo hapo juu la husika.
Mimi ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,
Kwa niaba ya wanachama wenzangu, tunaleta kwako malalamiko ya uvunjifu wa katiba ya chama Yanayotokana na matamko yanayoendelea kutolewa na viongozi wa kitaifa juu ya kuungana na UKAWA yenye tafsiri kwamba wataachiana majimbo ya kugombea ili waweze kuingia madarakani na kuunda serikali ya pamoja.
kama hivyo ndivyo wanakiuka SURA YA TISA. IBARA YA 9.3.1 ya KATIBA YA CHADEMA inayosema ''chama kinaweza kuunda mseto na chama au vyama vingine vyenye madhumuni na malengo yanayofannaili kuimarisha iwezo wa kushinda uchaguzi mkuu au wa serikali moja ya mtaa kwa lengo la kuunda utawala wa pamoja''
Kwa kuwa viongozi wa CHADEMA na CUF na NCCR wameungana na kuunda chama kingine cha UKAWA kwa mujibu wa SURA YA TISA ibara ya 9.3.3 ''chama kinaweza kuungana na chama ama vyama vingine kuunda chama kipya'' hivyo wamevunja SURA TISA, Ibara ya 9.3.4 inayosema ''Uamuzi kuhusu vipengere 9.3.1, na 9.3.3 utafanywa na mkutano mkuu wa Taifa na kuhusu kipengere 9.3.2 na Baraza KUU''.
Na hivyo sisi kama chama hatujakaa BARAZA KUU ili kupitisha AGENDA za huo mkutano mkuu na wala MKUTANO mkuu haujaitishwa kujadili maamuzi hayo yaliyofikiwa na viongozi wetu.
Mheshimiwa Msajiri, Tunafahamu kwamba KANUNI za chama SURA YA TISA kuanzia ibara ya 9.0 Mpaka ibara ya 9.7 zinatoa uhuru wa chama kuungana na kufanya ushirika na vyama vingine kwa kadri itakavyoona inafaa.
Ila kanuni hizi zinaweka mkanganyiko wa kitafsiri, na hivyo zinazuiwa na kuuliwa nguvu na Ibara ya 9.2.3 yaKATIBA YA CHAMA Inayosema ''kukitokea migongano kati ya kipengele cha katiba na kile cha kanuni, kipengele cha katiba kitatawala''. Hivyo kanuni zinazotoa uhuru huo haziwezi kutumika hapa.
Mheshimiwa msajiri, kwa kuwa wewe ndio mlezi na msimamizi wa vyama vyote vya siasa, na kwa kuwa hakuna chama cha siasa kilicho juu ya katiba yake, hivyo tunakuomba uingilie kati mgogoro huu wa uvunjifu wa katiba unaofanywa kwa makusudi na viongozi wa chama.
Tunakuomba pia uuagize uongozi wa kitaifa uitishe haraka kikao cha baraza kuu, kwani tumeshapitisha miezi mi nne sasa ya kisheria ambayo baraza kuu lilipaswa kukaliwa, mara ya mwisho tulikaa kikao cha baraza kuu mwezi febryary mwaka 2013, hivyo tulitakiwa tena tukae baraza kuu mwezi February mwaka huu. Hatujaitwa, wala hatujapewa sababu yoyote yenye mantiki.
Vile vile tunakuomba uwaagize viongozi wa chama waitishe chaguzi halali za zhama na waache kuchomeka watu wao wanaowataka kwa hila, kwa mujibu wa ratiba tulizozipitisha uchaguzi ulupiswa kuwa umeshafanyika kufikia December 2013, na baadae june 2014, lakini mpaka tunavyokuandikia leo, hakuna lililofanyika.
Tunakutakia kila la heri katika kutusaidia ufafanuzi huu.
Tunatanguliza shukrani za dhati na tukiamini swala letu litafanyiwa linavyostahili.
Wako katika ujenzi wa Taifa.
JORUM ABDALLAH MBOGO
………………………………………..
MWANACHAMA WA CHADEMA
MWENYEKITI WA CHA CHADEMA WILAYA YA KALIUA
MJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA TAIFA.
Nakala :- Vyombo vya habari
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment